Hakuna Ubishi Mwabukusi ni Mwanaharakati, Je TLS Yake Iwe ya Kiharakati, Au Asilete Harakati Zake kwenye TLS Yetu, Ibaki Kuwa Profesheno Body?

Pamoja na harakati zake ambazo zilimfanya ainekane adui namba moja wa serikali na hata kupewa kesi kadhaa za uchochezi na kufikishwa Mahakamani bado Mahakama ilimheshimu Mtikila, ikamtambua kama rafiki wa Mahakama (enzi hizo Mahakama ilipikuwa Mahakama na kugoma kuruthi maadui wa serikali na kuwafanya kuwa maadui zake), Je, tatizo la harakati ni nini? Maana harakati ni kama kampeni tu zinalenga ku create awareness na kuamsha wahisika, na bodies kama TLS zinategemewa sana kufanya hizi harakati wakitumia professional approach.
Je, kuna wakati Mwabukusi hakutumua professional approach? Ikawaje?
 
Naona upo nyuma ya wakati. Nadhani huna uelewa wa katiba ya Zanzibar, wala huna habari na ufafanuzi uliotolea na Rais wa JMT wakati akiwa madarakani kuhusiana na katiba mbili zinazoongoza nchi ya Zanzibar ( ukiwa ndani ya JMT) na ile ya JMT.

Katiba ya Zanzibar inatamka kuwa Zanzibar ni nchi (ufahamu kuwa hakuna nchi ambayo haina raia wake), na Rais Kikwete alikuja kusisitiza kuwa Zanzibar ni nchi ukiwa ndani ya JMT, ila ukiwa nje ya JMT, siyo nchi. Wewe Pascal unayetamka kuwa Rais Samia siyo mzanzibari, yaani siyo raia wa Zanzibar, unatamka ukiwa wapi? Kama unatamka ukiwa ndani ya JMT, ujue kuanzia lao, kama hukuwa na ufahamu, kuwa Zanzibar ni nchi, ina mipaka yake, ina raia wake, na miongoni mwa hao raia, ni Rais Samia.
 
si ulisema jamaa ni mwanaharakti na kwamba hataimudu TLS? Ndio maana nasema tuwe tunabakiza maneno ya akiba
1. Ni kweli nimesema rais wetu wa TLS ni mwanaharakati.
2. Kuna popote nimesema hataimudu TLS?.
P
 
Ukisoma between the line, unajua kile ulilenga! Tusibishane, ukweli hukuwahi kumkubali Jamaa.
Duh...!. Mimi ni member wa TLS na nimepiga kura!, jee unajua kura yangu nilimpigia nani?.

Jee unajua ile 2015, kuna wana CCM kibao walimpigia kura Lowassa na sio JPM?. Jee unajua kwa mujibu wa matokeo ya NEC ya urais Zanzibar, ENL alimuacha mbali JPM?. Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Umdhaniye ndie sie, na usio mdhania ndiye!. Don't assume!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…