View attachment 2891931
S2kizzy aka Zombie ni producer mkali kuliko Master Jay.
Zombie ambaye ni Grammy nominated mara kadhaa na kafanya nyimbo ambazo ana international hits kuzidi Master Jay ambaye alikuwa akimiliki studio ya MJ production ambayo alitumia wataalam wa kutengeneza muziki kama Maron linje, Profesa Ludigo, Maundi na wengine kadhaa uku akiweka sign yake kwenye nyimbo aonekane kazitengeneza yeye.
Naandika haya ili kumpa maua yake S2kizzyy ili jamii ijue ukubwa alionao kuzidi mkongwe Master Jay ambaye tunamheshimu licha ya kuwa mzee mwenye mihemko sana anaependa kutrend ambae ana historia mbaya ya kutumia wasanii wa kike kama Shaa akiwarubuni kwa studio time.
Zombie apewe heshima yake sio kila aliyetangulia anamzidi wa sasa lazima tuelezane ukweli.
Mkuu,
Kanuni muhimu ya kulinganisha mambo ni kulinganisha vinavyolinganishika.
Ndiyo maana hata kwenye ndondi watu wanapiganishwa kwa uzito sawa, si kupiganisha mpiganaji ndondi yeyote kwa yeyote tu.
Huyo S2kizzy kafanya kazi mwaka gani mpaka mwaka gani? Master J kafanya kazi mwaka gani mpaka mwaka gani?
Katika miaka yao ya kufanya kazi, kuna miaka imeingiliana?
Nasema hivi ili ulinganishe vitu vinavyolinganishika, usije kulinganisha watu wawili waliofanya kazi katika masoko tofauti, teknolojia tofauti, miaka tofauti, mpaka ule ulinganisho wako ukakosa maana.
Yani usije kufanya kosa la kumlinganisha baba ambaye hajui kusoma ambaye amemsomesha mtoto shule mpaka mtoto akajua kusoma, halafu ukasema huyo mtoto ni zaidi ya baba, kwa sababu mtoto anajua kusoma, bila kujali kwamba mtoto huyo anayejua kusoma, kakua katika mazingira ya watu wote kujua kusoma, na asingeweza kujua kusoma bila kusomeshwa shule na baba asiyejua kusoma ambaye alikua katika mazingira ambayo karibu watu wote hawakujua kusoma.
Master J ni mtu wa kulinganishwa na Mika Mwamba, P Funk Majani, Marlon Linje, Bonny Luv, Enrico Figueiro, Roy Bukuku.
Unawajua hao watu?
Hao ndio watu waliokuwa wanafanya kazi siku hizo za Master J.