Hakuna uhusiano wowote kati ya demokrasia na maendeleo

Kama bado tuna utamaduni wa kumchangia mtu aweze kufanya sherehe ya harusi yenye thamani hata kununua magari matatu ila huyo mtu mwenyewe hana hata uwezo wa kumudu kununua pikipiki, sidhani kama ni ajabu kwa hao viongozi kuwa hivyo walivyo. Si la ajabu kwao kununua midege,kujenga midaraja, kutoa mihela ya kujenga soko na kuacha changamoto za miaka yote kama shida za maji kwamba hadi leo bado watu wanakunywa maji yasio salama.
 

Hawa watawala wetu muda mwingine ukiwaza kwa umakini unaona hawana lengo kabisa la kuwasaidia wananchi masikini kujikwamua kiuchumi.

Wabunge wanajiuzuru wenyewe bila sababu ya msingi,wanaenda rudia uchaguzi wa majimbo kwa mabilioni ya pesa,afu vijijini huko wananchi masikini kabisa wanachangishwa michango ya ujenzi wa shule,zahanati n.k
 
Tatizo sio dictator shida ni ubinafsi mbona libya waliongozwa na dictator ila walikua na hali nzuri Hadi kufikia hatua ya kufadhili umoja wa africa!?
Shida ya libya unaijua angeishi vizuri na watu wake wasingemuuza
 
Mleta, Kwa hiyo Tanzania kuna udikteta na ni Faida?

Au unataka kusema hizi juhudi za kuuwa Demokrasia Tanzania unazibariki?
Unadhani kama pangehitajika demokrasia ingewezekana kuwahamisha machinga!? Maana kiufupi demokrasia inataka wengi uwape lakini wachache wasikilizwe!
 
Hata mataifa mengi yaliyoendelea kwa sasa hayakutengeneza hayo maendeleo chini ya tawala za kidemokrasia kihivyo!! Mf ni Africa ya kusini ilipiga hatua kubwa sana chini ya utawala wa kikaburu ambao haukuwa wa kidemokrasia!!
 
Shida ya libya unaijua angeishi vizuri na watu wake wasingemuuza
Hakuwahi kuishi vibaya na walibya kilichotokea ni baada ya wapinzani wachache kuchochewa tokea nje ya nchi, kitu ambacho katika uongozi ni kawaida tu, hata ingekua unakubarika kiasi gani hilo linaweza Kutokea mf ni uasi wa wabunge ndani ya chadema haimaanishi kwamba kuna ugomvi binafsi na mbowe ila ni ushawishi wa nje umechochea huu uasi!!
 
Kuhusu case ya kariakoo ni suala la vipaumbele tu ukiimarisha soko la kariakoo kwa hizi billion 34 inawezekana sana zikakupa miradi mingi sana ya maji pindi maboresho yake yakikamilika!!
 
Demokrasia ni mfumo ambao ufanisi wake utakuwepo endapo tu utatumika kwa jamii yenye upeo mzuri wa kuyatazama maisha, na ambayo ina lengo la pamoja la kuleta maendeleo sio kwa maslahi binafsi.

Kwa nchi zinazoendelea, mfumo unaopendelewa zaidi ni kutawala bila ku-entertain mawazo mbadala. Hali hii inadumaza ushiriki wa raia wenye uwezo wa kuchangia ili kuboresha hali na kusonga mbele.
 
Swali la muhimu ni kwamba chini ya dictator au chini ya demokrasia iliyopo sasa libya ni wakati gani walishuhudia ustawi wa wananchi!?
Kwa taarifa yako hiyo Libya ingeweza kuwa na maendeleo bila hata udictaror. Na hata sasa imevurugika kwakuwa yeye Gadaffi alilazimisha kukaa madarakani kwa shuruti wakati tayari watu walikuwa wamemchoka. Na hata hivyo hiyo Libya pamoja na kwamba haiko stable, bado ina uchumi mzuri kuliko sisi wenye amani ya hofu.
 

ivi bado kuna watu bado wanaamini gaddafi alikuwa dikteta
 
Kwa hiyo unakubaliana na mimi kwamba demokrasia inatuchelewesha!?
 
Kosa la ghadafi kutowaunganisha watu akiamini bunduki zaidi kuliko kuunganisha watu
 
Hatma ya taifa kuiweka mikononi mwa mtu mmoja Ni Jambo hatari sana!Ndio hasara ya utawala wa kudikteta!
 
Kwanza demokrasia ni 'dhahania' tu, ni perception yako ya kutafsiri kua nchi ile ina demokrasia au haina. Hakuna principles za moja kwa moja kwenye kutafsiri demokrasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…