No! Hapana! Umasikini wa Afrika haukutokana na ukosefu au kutokuwepo kwa demokrasia BALI umetokana na WIZI, UPORAJI NA UNYONYAJI ULIOKITHIRI wa mali na rasilimali za Afrika by hao Wazungu na Wasia kwa kutumia nia nyingi nyingi ikiwa ni pamoja na mikataba ya kinyonyaji dhidi ya akina Chief Kimweri na wenzao ZAMA ZA KALE.
Leo kuna wizi wa wazi wazi wa rasilimali zetu ikiwa ni pamoja na madini yetu (almasi, dhahabu, shaba, chuma, tanzanite na mengineyo), mali asili ikiwa ni pamoja na mbao za thamani sana kama mninga au mitiki na mengineyo na hata wanyama wetu ZAMA ZA LEO! Na kwa karibuni na hata sasa ni kwa kutumia misaada wanayotupa. Say wanakopesha $1.0bi/= lakini at the end of the day unaishia kulipa hata say $2. 0bi/=! Kwani utalipa riba, service charges kwa ajili ya huo mkopo, na zaidi ya hayo, utalipa mishahara na migharama mingine mingi kwa ajili ya "wataalamu" wanao ambatana na huo mkopo! Achilia mbali kuwa utanunua hata vifaa vingine vya hiyo miradi kutoka kwao kwa bei za KURUKA! Kwa njia hiyo mipesa inarudi kwa hao waliotukopesha!
Chunguzeni mikopo hii mtaona kuwa kuna njia nyingi za kinyonyaji na wizi ndani yake na hivyo kuufanya huo mkopo au hata msaada usiwe na manufaa kwetu na hivyo kuzidi kutufanya kuwa masikini! Kuna mtu mmoja aliwahi kusema "mikopo inatufanya tuzidi KUSIKINIKA na watoa mikopo na wazidi KUTAJIRIKA!