Hakuna umeme toka asubuhi, tatizo ni nini?

Hakuna umeme toka asubuhi, tatizo ni nini?

mbenge

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
4,864
Reaction score
10,483
Baadhi ya maeneo ya Kinondoni Kaskazini yamekosa umeme toka saa tatu asubuhi mpaka ninapotuma huu uzi hivi sasa.
Je! Kuna changamoto yoyote ile iliyojitokeza, na pengine imekwisha kutolewa taarifa hapo kabla na uongozi wa TANESCO siku ya leo ya tarehe 02-06-2024. Pengine taarifa hiyo imenipita huku baadhi ya wadau wameisikia.

Kwa muda sasa kulikuwa hakuna tena tatizo katika katika umeme ya muda mrefu kama huu, na hata kama iliwahi kutokea basi ilikuwa kwa kipindi kifupi, ama taarifa kutolewa kabla endapo changamotp ilikuwa ni kubwa, hasa ikitokea katika Grid ya taifa.

Sasa leo kwa upande wangu sina taarifa yoyote ile, na kila nikijaribu kupiga katika namba zao, napata majibu kuwa simu yako itapokelewa hivi punde, kwani watoa huduma wao kwa sasa wanaongea na wateja wengine.

Kama kuna mwanajukwaa anatambua uwepo wa changamoto yoypte ile ambayo imejitokeza tafadhali naomba anijuze.
 
Siyo kinondoni tu.... Hadi baadhi ya maeneo ya Kilimanjaro
Lazima kutakuwa na shida, kwa maana kwa siku za hivi karibu haijawahi kutokea. Lakini suala la utoaji wa taarifa kwa wakati kutoka katika uongozi wa TANESCO, hicho sasa ni kipengele kingine!
 
Kibongobongo msipokosa kitu huwa hamna shukran

Acha muwe mnapewa sessions za kukosa huduma ili muwe mnaheshimu watoa huduma
 
Back
Top Bottom