Hakuna umeme toka asubuhi, tatizo ni nini?

Kukosekana kwa umeme siku ya Jumapili huleta kadhia kubwa kwa wanaume waliokuwa wengi!
  • Kelele nyingi na malalamiko kuhusu kuchelewa kurudi nyumbani siku ya Jumamosi usiku, licha ya uwepo wa fainali ya UEFA League
  • Kulishwa pilau "full suit" kisa eti kumpumzisha binti wa kazi
  • Sebuleni hakufai chumbani nako hakufai
  • Ukitaka kuondoka lawama zinakuja unataka kurudi kwa yule uliyekuwepo naye jana

😫😫😫😫
 
Sababu ya msingi ni kupungua kwa maji kwenye bwawa la Nyerere
 
Jana ilikuwa hivyo huku nilipo,umekatwa asubuhi ukarudi jioni.

Wadau wakawa wanadai et vichaa huwa hawaponi kwa 100%
 
Lazima kutakuwa na shida, kwa maana kwa siku za hivi karibu haijawahi kutokea. Lakini suala la utoaji wa taarifa kwa wakati kutoka katika uongozi wa TANESCO, hicho sasa ni kipengele kingine!
Huu ni uhujumu wa uchumi au hujuma dhidi ya Mama. Mmmm, hivi si Januari alishatoka huko? Maana zile mashine za Bwawa la Nyerere nasikia zinatoa megawat 250 kama kawaida.
Hii ni mpya! Ngoja muenezi wa chama aje atudanganye kidogo, ili turidhike.
 
nchi kwa sasa umeme ni walawala

nafikiri ni hitilafu ndogo tuh
 
Hata mkoa wa Tabora hasa wilaya ya urambo tuna mwezi mzima umeme unakata asubuhi na kurudi ni usiku wa manane,nahisi mgao umerudi japo hawataki kusema
 
Hapa Goba njia nne, walikata asubuhi, wakarudisha jioni, ila wamekata tena sahv
 
Hivi sasa ni saa mbili kasoro dakika nne hakuna umeme Mbagala, eti nasikia tope la Hanang'i limeingia kwenye waya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…