Hakuna Usafiri wa Umma wa ovyo na Hatari Duniani kama Mwendo kasi Tanzania

Kuna uwezekano viongozi wa juu hawajui juu ya hiyo kadhia ama lah wanajua ila wanafanya kusudi kukaa kimya kwa madhumuni fulani fulani ya kisiasa.

Maana wao wanapita mwendo wa ngiri mkia juu, barabara nyeupee hamna foleni, hamna kelele, vioo viko juu ni kiyoyozi tu, si ajabu mitandaoni nako anapitishwa accounts za chawa wake tu, wale wanaosifia.
Akisema asikilize redio ni chawa, tv ndo chawa pro max, tarifa za habari nyingi ni za kuwasifia na nyingine viongozi waliochaguliwa wakimulikwa na camera huku wakitatatu changamoto hewa.
 
Umezunguka dunia nzima?
 
Sitaki kuharibu mada yako mkuu, ila sisi tunaishi peponi compare na usafiri wa umma wa South Asia,


 
Umewahi kufika India? Ht youtube huoni watu walivyojazana mpk kwenye keria ya treni? Tembea uone hapo ndio umetoka kwenu Mahenge safari bado
 
Ni utetezi wa Kijinga na kutafuta justification ya uzembe wa serikali ya Tanzania.
 
Rais nj Samia ambae anategemea machawa wanasema nini unategemea mabadiriko kweli?
.
Hapo si ajabu taarifa alizinazo ni kwamba mwendo kasi mambo yako poa abiria hawakai zaidi ya dakika 5 kituoni
🤣🤣🤣
 
Usifanye jambo bovu halafu ufurahi eti kisa mwenzako anafanya vibaya zaudi yako. Mwendokasi zinavuja! Maboresho ni ya lazima hata kama mumbai kukoje sijui
Huyo ni mpuuzi..mUnajilinganishaje na failures???
 
Sikiliza wewe kunguni.

Mtoa mada amedai kuwa mwendokasi ni usafiri wa hovyo na hatari kuliko yote duniani.

Amefanya comparison wapi na wapi?
Kama hoja zako zingeweza kujieleza zenyewe, usingehitaji matusi wala dharau. Bahati mbaya ni kwamba unajaribu kufunika udhaifu wa point zako kwa makelele , lakini hata ukipiga kelele, hoja dhaifu zitabaki kuwa dhaifu. Si ajabu, jina lako lenyewe linatuonya mapema: Mlolongo , huenda hata fikra zako zimepotea njiani kwenye huo mfululizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…