Hakuna Usafiri wa Umma wa ovyo na Hatari Duniani kama Mwendo kasi Tanzania

Nimecheka huyo jamaa aliyebanwa kisigigo huku gari inaanza kuondoka.

Sema usafiri wa umma unadhalilisha watu sana. Nakumbuka enzi za vi hiece, unakuta mtu kainama tako liko nje konda analazimisha kufunga mlango halafu yeye anatoa kichwa nje anapata hewa safi...
Nyie abiria mnafika mgongo unauma, mnahemeana, majasho yanatiririka...

Bado kadhia ya watu kugombania siti aahahahahaa usafiri wa umma ni kudhalilishana tuu aisee 🀣🀣🀣🀣.

Nilikuwa na tabia ya kuzunguka na gari nakaa siti ya mwisho halafu naanza kupata namna abiria wanavyopeana hekaheka za unanisukuma, unajiegemea sana, nishikie mzigo, unanikanyaga.... Acha tuu maisha hayaa...!
 
Acha upuuzi kuhalalisha uongozi mbovu wa DART na mambo ya India.
Kwamba aliyetoa ushauri kituo kijengwe kwenye mafuriko jangwani sasa amestaafu anakula pensheni na nyumba masaki na kituo kimeoza, aliyenunua magari yasiyi na spea naye anajenga apparment na hajaguswa alafu mnafananisha na india?
Upuuzi mtupu.
 
Sijaelewa kwanini umetoa huu mfano.

Kwamba kwasababu Mumbai hali iko hivyo kwahiyo watu wa Dar hawatakiwi kulalamika au?
Hawo ndo wanaowaza kwa kutumia makalio,.,..badala ya kutatua changamoto, yeye anatoa mfano wa tatizo lingine tena,.....
 
Huu n zaidi ya uharifu dhidi ya utu wa mtanganyika
 
Kwahiyo ndo tuige mabaya!? Ni ujinga kuhalalisha makosa kwa makosa mengine! Kwanini tusijifunze kwa waliofanikiwa?
 
Hii itakuwa ni Bangladesh mkuu
 
Ha haaaa haaa. Mtaniumiza mbavu.
Kwa hio ulirushwa kama mpira!? 🀣🀣🀣
Pale gerezani jioni mlango ukifunguliwa kama sekunde 7 zinapita hakuna aliyefanikiwa kuingia ndani ni pause moment ya msuguano wa maana mlangoni, atakayefanikiwa kuvurumishwa ndani kutokana na msukumo ndo anafungua kuingia sasa, hapo unafika simu huna kiatu kimoja kiko nje, wigi halipo, yaani.
 
Mwendokasi ndio biashara pekee ninayoufahamu ambayo inashindwa kustawi kutokana na wingi wa wateja wake.πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
Ni Biashara yenye faida kubwa kwa gharama ndogo za uendeshaji mkuu..!
Wanapakia watu kama β€œbaro za Mtumba”
 
INdia ndyo nchi yenye population kubwa duniani hivo changamoto kama hiyo haiwezi kukwepeka tofauti na Tz population ndogo lakin Bado tatizo
Very true kwasasq tupo ~6mil kwa Dar .. hii idadi bado ni ndogo kwa jiji kubwa 5yrs lare itakuwaje.?
 
Usifanye jambo bovu halafu ufurahi eti kisa mwenzako anafanya vibaya zaudi yako. Mwendokasi zinavuja! Maboresho ni ya lazima hata kama mumbai kukoje sijui
Ni kweli !
Kujilinganisha na walio fail haina maana
 
Mimi nikiwaambia watu siwezi kupanda mwendokasi wanasema nna maringo. Ila mara ya mwisho nusu nitolewe shingo mlangoni nikajiapiza never ever
Ni kweli hakuna sifa kwenye kufanya jambo la hatarishi kama hili..
Hizo basi za mbezi zikipata ajali jioni tutapoteza watu wengi sana
 
Sasa na hao walio nyoosha mikono juu ni mateka wa ukanda wa Gaza?
Hao ni warefu sasa kuna watoto wa shule za maingi wafupi hawajishikiliii popote wana hang hapo kati

Hizo gari hazina AC, zina poor ventilation system
 
Kwamba watu wa India Population wangekuja hapa Dar na wa Dar wakaenda huko India mambo yangekuwaje.., Ofcourse wa Bongo sio mbaya dunia nzima ila kwa nchi yenye resources na watu ambao sio wengi kama wa kule kinachoendelea hakiridhishi...

Sio vema kujilinganisha na vipofu katika kuona..; Ingawa ukiangalia idadi ya watu sisi we are worse off; and we need to do better
 
Acha ukorofi wee Ngosha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Uje nikutembeze mwendokasi tuzunguke ruti zote, ukichoka nakupeleka ukale mihogo Coco Beach.
Swali langu hujanijibu. Ni swali genuine kabisa nataka kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…