Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Matendo yake ni matendo ya kibinadamu na makosa ya kibinadamu kama binadamu wengine.

Si kwamba ni shetani ndio alimtuma au alimfanya afanye vile.

Ni tamaa zake za kibinadamu wala hakuna shetani yeyote yule.
Sasa hapa ndio nimezielewa akili zako...

Mimi naishia hapa kujadiliana na wewe kwenye mada hii.

Kama ningekuwa nakufahamu ningejiridhisha wewe ni mtu wa aina Gani.

Hiki unachokiandika humu huenda ni campaign za kuwafanya watu wasiamke.

Kwa hivyo sijui lengo lako, na nadiriki kusema huenda ikawa unaujua ushirikina kuliko hata wengine wetu humu...
 
Umeshatembea nchi ngapi au hata mikoa mingapi hapa tz bwana mdogo?
Jibu swali acha kukwepa swali.

Nitajie nchi yeyote duniani iliyotajirika kwa uchawi au ushirikina?

Nitajie tajiri yeyote mkubwa duniani aliyetajirika kwa uchawi au ushirikina?
 
Usijadili vitu usivyovijua. This world is governed by spiritual powers. Hata wazungu walio matajiri kuna kanuni za kiroho wanazifuata!
 
Jibu swali acha kukwepa swali.

Nitajie nchi yeyote duniani iliyotajirika kwa uchawi au ushirikina?

Nitajie tajiri yeyote mkubwa duniani aliyetajirika kwa uchawi au ushirikina?
Hizo mambo zinaendana na code, kama hauzijui utabaki kuwa mweupe tu kichwani kama ulivyo wewe.
 
Nakwambia hivi kama kuna utajiri wa kishetani nenda kautumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa duniani kama kweli utajiri wa namna hiyo upo.
 
Usijadili vitu usivyovijua. This world is governed by spiritual powers. Hata wazungu walio matajiri kuna kanuni za kiroho wanazifuata!
Kanuni zipi za kiroho ziweke hapa ili baada ya mda kila mtu awe tajiri humu jukwaani.
 
Je unadhani utajiri wa shetani unaupata hivihivi? Kuna masharti magumu wale wenye kuweza kujilipua ndio wanaweza kufuata hayo masharti. Ni mateso tupu!
 
Je unadhani utajiri wa shetani unaupata hivihivi? Kuna masharti magumu wale wenye kuweza kujilipua ndio wanaweza kufuata hayo masharti. Ni mateso tupu!
Masharti yapi? Ya aina gani?

Thibitisha na leta uthibitisho hapa wa hayo masharti.
 
Siwezi kukupinga mr. Maana hata akija mtu akasema ametajirika kwa kutoa kafara bado huwezi kuamini. Upande wangu nmejaribu kutoa mwanga wa uhalisia wa nguvu zisizoonekana zinavyotenda kazi Sasa Ni juu yako kuunganisha dot au kubaki na imani yako. Japo kwa ninavyoelewa mama angetibu kwa mitishamba peke yake bila nguvu flani kusingekuwa na masharti ya usigeuke nyuma, Wala usiongee na mtu. Ni hayo tu.
 
Hizo mambo zinaendana na code, kama hauzijui utabaki kuwa mweupe tu kichwani kama ulivyo wewe.
Kafuate hizo code uwazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk na Jeff Bezos.

Una bwabwaja bwabwaja hapa kuna Code, Halafu hata kwenye Top ten ya matajiri wakubwa Afrika, Haupo.
 
Kanuni zipi za kiroho ziweke hapa ili baada ya mda kila mtu awe tajiri humu jukwaani.
Sharti kuu ni ibada. Kama upo tayari kumsujudia shetani nenda kamsujudie upate utajiri wake lakini utaishia Jehanamu. Kanuni za Mungu ni kutoa Sadaka kwa kazi ya Mungu ya Injili na kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
 
Je unadhani utajiri wa shetani unaupata hivihivi? Kuna masharti magumu wale wenye kuweza kujilipua ndio wanaweza kufuata hayo masharti. Ni mateso tupu!
Wewe umesikia kwa mtu ambae nae kasikia vivyo hivyo, ni kama zile stories za watu kukutana na wadada majini akamwambia awashe taa , akanyosha mkono mrefu ajabu , hizi hadithi zinafanana nchi nzima na kila mtu akisimulia anadai ni rafiki yake katokewa na hilo tukio
 
AJira hazipo lakini kuna mwamba leo ameajiriwa mwenye level moja na ufaulu sawa na amehitimu chuo mwaka huu

Kuna mtu kama yeye amemaliza 2015 hadi sasa kazi yake kuomba ajira kila mwaka bila mafanikio

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…