Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Matendo yake ni matendo ya kibinadamu na makosa ya kibinadamu kama binadamu wengine.

Si kwamba ni shetani ndio alimtuma au alimfanya afanye vile.

Ni tamaa zake za kibinadamu wala hakuna shetani yeyote yule.
Sasa hapa ndio nimezielewa akili zako...

Mimi naishia hapa kujadiliana na wewe kwenye mada hii.

Kama ningekuwa nakufahamu ningejiridhisha wewe ni mtu wa aina Gani.

Hiki unachokiandika humu huenda ni campaign za kuwafanya watu wasiamke.

Kwa hivyo sijui lengo lako, na nadiriki kusema huenda ikawa unaujua ushirikina kuliko hata wengine wetu humu...
 
Umeshatembea nchi ngapi au hata mikoa mingapi hapa tz bwana mdogo?
Jibu swali acha kukwepa swali.

Nitajie nchi yeyote duniani iliyotajirika kwa uchawi au ushirikina?

Nitajie tajiri yeyote mkubwa duniani aliyetajirika kwa uchawi au ushirikina?
 
Waafrika wengi hasa watanzania wamekuwa wakiamini kwa muda mrefu kwamba kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina. Cha kushangaza hali zao za kiuchumi ziko vilevile miaka nenda rudi.

Kama kweli kwa hakika unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote uwe tajiri mkubwa nchini Tanzania, Afrika na duniani?

Kwa nini ujihangaishe kufanya kazi na kuchoka ilhali unajua kuna utajiri wa kishetani?

Kamtumie huyo shetani akutajirishe kama ni rahisi hivyo!!

Katoe kafara za kutosha ikiwezekana hata ukoo wako wote tuone kama biashara yako itakuwa kubwa au utaweza hata kufikia utajiri wa Bakhressa.

Kama kweli kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa Afrika kama Aliko Dangote, Bakhressa, Mo Dewji na matajiri wengine wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos?

Kama kweli unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini hujautumia huo uchawi, ushirikina, uganga angalau ufike hata level za utajiri wa Mo Dewji?

Kama unaamini kuna Shetani akitolewa kafara anatoa mali au atakupa mali za kukutajirisha, Katoe kafara wazazi wako au wanao wote tuone kama hata utafika level za utajiri wa Dangote.

Au kama unaamini kuna utajiri wa ndagu, uganga, ulozi n.k
Mwambie huyo mtoa ndagu au mganga, Akupe utajiri angalau umfikie au umzidi Bakhressa kama ana huo uwezo.

Au mwambie huyo mganga akuwezeshe umiliki private jet ✈️, Kiwanda kikubwa cha uzalishaji, Magari makali ya kifahari kama Rolls-Royce Boat tail, Mercedes Maybach, Buggati, Lamborghini, Cadillac escalade au akishindwa sana angalau akupe Range rover sport kwa uganga wake tu.

Waafrika wengi hasa watanzania wana amini kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina lakini bado maisha yao ni ya kimaskini, kikapuku, kifukara pangu pakavu tia mchuzi.

Kama unaamini au unajua kuna Shetani anatoa utajiri, Kamtumie kwa nguvu zako zote akutajirishe na uwe tajiri kweli, Angalau ufike level za utajiri wa kina Dangote.

Kisha ndio uanze kusema kwamba kuna utajiri wa kishetani.

Habari za utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina, Husikika tu kwa waafrika maskini choka mbaya, wajinga, wavivu, makapuku, makabwela na mafukara ambao wanashinda vijiweni na vilabuni waki danganyana na kupeana matumaini uchwara ya utajiri wa kufikirika.

Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani kinacho toa utajiri. Utajiri na pesa hutoka kwa binadamu. Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani chenye pesa.

Pesa ni za binadamu, Si za Mungu wala Shetani.

Hakuna Mungu, Shetani, Jini, Pepo au nguvu yeyote ile ya kimiujiza inayotoa Utajiri.

Pesa, Mali na utajiri hupatikana kwa nguvu za kibinadamu na wanadamu.


Ni wajanja wachache tu huwalaghai na kuwadanganya watu wengine kwamba kuna shetani anatoa utajiri ili kuwahadaa na kuwapumbaza watu wajinga wasiotaka kuhustle wenyewe wakitegemea mafanikio ya kuletewa.

Ndio maana unakuta wanawekewa masharti makali ya kupata pesa hizo ambao wao hudhani ndio masharti ya kishetani ya huyo shetani, Kumbe ni masharti ya binadamu wajanja tu.

The supernatural power is You, Yourself.

Hakuna Mungu wala Shetani anayetoa utajiri, pesa au mali.

I'm out.
Usijadili vitu usivyovijua. This world is governed by spiritual powers. Hata wazungu walio matajiri kuna kanuni za kiroho wanazifuata!
 
Jibu swali acha kukwepa swali.

Nitajie nchi yeyote duniani iliyotajirika kwa uchawi au ushirikina?

Nitajie tajiri yeyote mkubwa duniani aliyetajirika kwa uchawi au ushirikina?
Hizo mambo zinaendana na code, kama hauzijui utabaki kuwa mweupe tu kichwani kama ulivyo wewe.
 
Sasa hapa ndio nimezielewa akili zako...

Mimi naishia hapa kujadiliana na wewe kwenye mada hii.

Kama ningekuwa nakufahamu ningejiridhisha wewe ni mtu wa aina Gani.

Hiki unachokiandika humu huenda ni campaign za kuwafanya watu wasiamke.

Kwa hivyo sijui lengo lako, na nadiriki kusema huenda ikawa unaujua ushirikina kuliko hata wengine wetu humu...
Nakwambia hivi kama kuna utajiri wa kishetani nenda kautumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa duniani kama kweli utajiri wa namna hiyo upo.
 
Usijadili vitu usivyovijua. This world is governed by spiritual powers. Hata wazungu walio matajiri kuna kanuni za kiroho wanazifuata!
Kanuni zipi za kiroho ziweke hapa ili baada ya mda kila mtu awe tajiri humu jukwaani.
 
Kuna makapuku yako kwenye ule uzi wa " The dark side of business" yanalishana Matango pori na kuaminishana Ujinga.

Yanatetea kuna utajiri wa kishetani, ila kuutumia watajirike hawawezi.

Wanabaki kutetea utajiri wa kufikirika tu. Imaginations just an illusion.
Je unadhani utajiri wa shetani unaupata hivihivi? Kuna masharti magumu wale wenye kuweza kujilipua ndio wanaweza kufuata hayo masharti. Ni mateso tupu!
 
Hapa nimegundua shida ipo kwenye imani ya dini yako na sio uchawi

Mama yako sio mchawi bali anatibu kupitia tiba asilia yani miti shamba huo ugonjwa upo tu siku ukikoma na tiba itakuwa imeishia hapo au zikigundulika dawa nyingine eneo hilo au vinginevyo

Haitoshi kurelate tiba anayotoa bi mdashi na utajiri wa nguvu za giza

Hakuna utajiri wa nguvu za giza ni imani za masikini juu ya matajiri ndio maana wote wanaosema upo wanashindwa kutoa mifano ni nani duniani ana utajiri wa kichawi hakuna
Siwezi kukupinga mr. Maana hata akija mtu akasema ametajirika kwa kutoa kafara bado huwezi kuamini. Upande wangu nmejaribu kutoa mwanga wa uhalisia wa nguvu zisizoonekana zinavyotenda kazi Sasa Ni juu yako kuunganisha dot au kubaki na imani yako. Japo kwa ninavyoelewa mama angetibu kwa mitishamba peke yake bila nguvu flani kusingekuwa na masharti ya usigeuke nyuma, Wala usiongee na mtu. Ni hayo tu.
 
Hizo mambo zinaendana na code, kama hauzijui utabaki kuwa mweupe tu kichwani kama ulivyo wewe.
Kafuate hizo code uwazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk na Jeff Bezos.

Una bwabwaja bwabwaja hapa kuna Code, Halafu hata kwenye Top ten ya matajiri wakubwa Afrika, Haupo.
 
Kanuni zipi za kiroho ziweke hapa ili baada ya mda kila mtu awe tajiri humu jukwaani.
Sharti kuu ni ibada. Kama upo tayari kumsujudia shetani nenda kamsujudie upate utajiri wake lakini utaishia Jehanamu. Kanuni za Mungu ni kutoa Sadaka kwa kazi ya Mungu ya Injili na kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
 
Je unadhani utajiri wa shetani unaupata hivihivi? Kuna masharti magumu wale wenye kuweza kujilipua ndio wanaweza kufuata hayo masharti. Ni mateso tupu!
Wewe umesikia kwa mtu ambae nae kasikia vivyo hivyo, ni kama zile stories za watu kukutana na wadada majini akamwambia awashe taa , akanyosha mkono mrefu ajabu , hizi hadithi zinafanana nchi nzima na kila mtu akisimulia anadai ni rafiki yake katokewa na hilo tukio
 
AJira hazipo lakini kuna mwamba leo ameajiriwa mwenye level moja na ufaulu sawa na amehitimu chuo mwaka huu

Kuna mtu kama yeye amemaliza 2015 hadi sasa kazi yake kuomba ajira kila mwaka bila mafanikio


Ova
 
Back
Top Bottom