Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Huyo anayekupa hayo masharti ya kunywa damu, Kwanza muulize ana utajiri kiasi gani?

Pia muulize utajiri wake umemfikisha wapi?

Muulize ana utajiri wa kuweza kumzidi walau basi Mo Dewji?
Hayo njoo ukamuulize wewe
 
Nimuulize nani?

Huyo anayeulizwa ana hata kampuni yake aliyo isajili kwa jina lake,

Au ndio wale waganga maskini choka mbaya wako kwenye vibanda na matunguli yao wakitafuta wajinga wakuwapiga na kuwadanganya?
Shida stress za home mnaleta jamvini 🙌😂
We endelea kupanick achana na wanaodanganywa na waganga
 
Dunia ina mambo mengi sana, kuna vinavyoonekana na visivyo onekana kwahiyo endelea kujifunza
 
Nilitaka kumjibu hivyo hivyo umeniwahi! Vitoto vya 2000 hivi bwana yani vinajiona vinajua kila kitu kwenye huu ulimwengu, vinadhani kila kitu kinapatikana google
Unathibitisha vipi ni mtoto wa 2000?

Hunijui, sikujui halafu unasema mimi ni mtoto wa 2000?

Au unadhani wewe tu ndio mzee humu JF kwa hiyo akili yako ndogo ya kufikiri?

Jenga hoja acha kuleta Viroja.

Nakwambia hivi kama kuna utajiri wa kishetani nenda kautumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa kama Bakhressa na Mo Dewji.

Ukifanikiwa hilo, uje hapa.
 
Basi kama kuna mtu Huwa namuona ni mpumbavu ni yule anayesema hakuna Mungu. Kuna vitu vonatia hasira sana.

Nimeumia sana kwa ajili yako. Kwa hiyo na wewe unajiweka kwenye kundi la wanasayansi ambao hawaamini kuwa kuna Mungu.

Hao wanasayansi deep down wanaamini Mungu yupo sema wameshindwa kuthibitisha kisayansi ndio maana wanakana.

Aliyekulisha huo upuuzi wa atheist amekosea sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…