Hebu tufafanulie, bahati katika utajiri ipoje ipoje?
Kuzaliwa katika familia ya kitajiri, Hiyo tayari ni bahati kwa mtoto. Si kila mtoto anapata bahati ya kuzaliwa kwenye familia tajiri.
Mtu anaye bahatika kuoa au kuolewa kwenye familia za kitajiri, Huyo tayari ana bahati ya kwenda kuukuta utajiri.
Hato hangaika sana kama wale wanao oana wakiwa na hali duni za kimaisha. Hiyo tayari ni bahati.
Kama bahati inaweza kuleta utajiri ni sahihi pia kusema mikosi huleta umasikini.
Bahati huweza kumtokea mtu yeyote yule awe mwema, muovu, mtoto, mtu mzima, mwanaume, mwanamke n.k
Bahati ni kama probability, inaweza kutokea ama isitokee.
Mikosi ni dhana ya kufikirika inayo husishwa na nguvu fulani za kufikirika tu.
Mfano mwanafunzi akifeli darasani, Anaweza kuhisi ana mikosi kumbe hakusoma na kujiandaa vizuri, Au alisoma akasahau alichosoma.
Na si kwamba ni hiyo "mikosi" ndio imemsababisha afeli.
Sasa basi, chanzo cha bahati ni nini
Chanzo cha bahati ni uwezekano wa kutokea jambo, Ambalo katika nafasi ya kutokea lipo tayari.
Mfano kuzaa na kuzaliwa kupo tayari automatically, Na wewe unaweza kuwa ni tajiri na mtoto wako akapata bahati ya kuzaliwa na wewe ukiwa tajiri.
Vivyo hivyo anaweza akazaliwa na wewe ukiwa maskini au kwingineko kwenye familia maskini. Maana bahati ni probability.
na pia chanzo cha mikosi ni nini?
Mikosi haipo, mikosi ni dhana ya kufikirika tu.