Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Sharti kuu ni ibada. Kama upo tayari kumsujudia shetani nenda kamsujudie upate utajiri wake lakini utaishia Jehanamu. Kanuni za Mungu ni kutoa Sadaka kwa kazi ya Mungu ya Injili na kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Nisujudie kitu ambacho hakipo? Jehanam pia haipo hizo ni imani tu kabla ya wakoloni kuja hiyo dhana ya shetani na jehanam haikua vichwani mwa watu na watu waliishi tu kwa imani zao tu nyingine.
 
Hata shetani hataki watu wavivu, wazembe na wasio na Siri.Maskini wengi wana sifa hizo, hivo sio Mungu wala shetani anayewataka.
 
Imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho wa jambo au kitu fulani.

Mimi siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yeyote ile.

Sihitaji kuamini Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.
Kujua na uthibitisho ndio Imani!
 
Bado unasafari ndefu sana.

NINAISHIA HAPA.
Usije hapa kuongelea vitu ambavyo huna uthibitisho navyo.

Hizo stori zenu za utajiri wa kishetani danganyaneni huko kijiweni na vilabuni.

Ukisema kuna utajiri wa kishetani, Eleza na thibitisha ni tajiri gani mkubwa duniani alifanikiwa kwa uchawi na ushirikina?

Ukisema kuna utajiri wa kishetani, Eleza na thibitisha ni nchi gani ilitajirika kwa uchawi au ushirikina?

Unless otherwise, Don't come here to advertise your ignorance.
 
Kujua na uthibitisho ndio Imani!
Hapana.

Nitakupa mfano,

Ukishajua mwanzilishi wa JF ni Maxence Melo, Huihitaji tena imani kwamba Jamii forums ilianzishwa na Maxence Melo.

Maana tayari unajua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho kwamba mwanzilishi wa JF ni Maxence Melo.

Kitu ambacho hukijui ndio unakua na imani nacho maana huna uhakika wala uthibitisho wa kitu hicho.

Hivyo imani si kujua.

Imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho.
 
Nawatakia kila la heri mnaoweza kuendeleza mjadala na mtu anayetukana, kejeli na kudhihaki wengine
Mimi situkani mtu wala kumdhihaki mtu, Akija kwa hoja.

Ila ukija kwa lugha ya matusi na kejeli utapata stahiki zako vilevile.

A fool must be answered according to his or her foolishness.
 
Mtoa post wewe ni mjinga sana. Kila kitu kina limit yake. Unapaswa kujua aina za utajiri
1. Utajiri wa Maombi +Bahati+bidii yakazi +Maarifa
2. Utajiri wa nguvu za giza+Juhudi+maarifa+Juhudi ya kazi.
Nipe mfano wa tajiri aliyetajirika kupitia hoja namba 2 hapo juu kwa hapa tz au nje ya tz kwa ushahidi
 
Siwezi kukupinga mr. Maana hata akija mtu akasema ametajirika kwa kutoa kafara bado huwezi kuamini. Upande wangu nmejaribu kutoa mwanga wa uhalisia wa nguvu zisizoonekana zinavyotenda kazi Sasa Ni juu yako kuunganisha dot au kubaki na imani yako. Japo kwa ninavyoelewa mama angetibu kwa mitishamba peke yake bila nguvu flani kusingekuwa na masharti ya usigeuke nyuma, Wala usiongee na mtu. Ni hayo tu.
Kwahiyo kupitia hiyo tiba ya mama na hayo masharti ndio ukahitimisha kuwa kuna utajiri wa nguvu za giza
 
Mnataka uthibitisho gani
Wakati hamtaki kuingia kwa ground mka pate uthibitisho?

Inawezekaje utake watu waamini experience yako na hutaki kuamini yao,
 
Hata shetani huwa hapotezi muda na watu wazembe, wavivu na wasioweza kutunza Siri.
 
Mnataka uthibitisho gani
Wakati hamtaki kuingia kwa ground mka pate uthibitisho?
Kwa ground wapi?

Niambie na thibitisha ni tajiri gani mkubwa duniani alifanikiwa kwa uchawi au ushirikina?

Niambie ni nchi gani duniani ilifanikiwa kwa raia wake kuwa wachawi na washirikina?
Inawezekaje utake watu waamini experience yako na hutaki kuamini yao,
Mimi siamini kwenye kuamini.

Sihitaji kuamini Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Wewe njoo na ushahidi au uthibitisho wa tajiri mkubwa duniani aliyetajirika kwa uchawi na ushirikina.
 
Back
Top Bottom