Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Kuna video moja ya kusikitisha sana. Kuna lijinga linajirekodi limnachapa fimbo bibi wa watu. Kisa alikuwa na kifurushi kaingia nyumbani mwao. Eti linadai amekuja kuwaroga. Hawazi labda huyu bibi mgonjwa wa akili au labda amepatwa na ugonjwa wa kuahau unaowapata wazee lenyewe linawaza amekuja kuwaroga. Wanaoamini haya masuala ni wajinga daraja la kwanza.
 
Katika watu wajinga, nafikiri wanaoamini habari za kichawi wanaongoza
Wewe ndio mjinga namba moja, ukisema huamini uchawi inamaana wewe huna dini, na pia huamini km kuna MUNGU yaan wewe unaamini sayansi tu maana wanasayansi hawaamini uwepo wa MUNGU, kwa hio chagua upande mapema usitujazie inzi siku ukisharogwa ndio utaelewa Jambo kwamba MUNGU yupo na katika uumbaji MUNGU aliumba uchawi pia ila wapo binadamu waoutumia vibaya kwa binadamu wengine, na vitabu vya dini vinatambua uwepo wa uchawi

Waislamu kuna Surat Jin kwenye Quran

Wakristu wanakatazwa habari za kuhusu kufanya uchawi kwenye Biblia

Sasa wewe unapinga nini?

Nani amekuroga Mgalatia/Mpagani/Mpagazi?
 
Wallah mimi nilikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa hawaamini ushirikina hata asilimia zero.....lakini kuna point flani nilikutana na mzee wa busara akawa amenifungulia code zote zilizopo hapa ulimwenguni.....nilipoanza kuchukua hatua kila kitu kilibadilika.......endelea kujidanganya uchawi tena kama maofisini watu wanarogana balaa, na siku yakikukuta hutokuwa tofauti na mtu anaejifunika shuka hali yakuwa pamekucha
 
Unaamini kwamba unaweza kufanyiwa dawa za kichawi kiasi kwamba ukipigwa risasi haikuingii?
 
Natamani siku nishuhudie kitu kilichofanyika kiuchawi
Siku moja vijana wangu wa kazi walinipigia simu saa saba usiku. Wakaniambia Kuna watu wanafanya vurugu eneo langu la biashara.
Niliamka na kuelekea huko.
Kufika pale segerea oilcom Kuna Kona Kali kuelekea stand. Mm nilinyoosha kuelekea kwa CDF mstafu. Ile naachha Barabara kuu, nikasikia mlio wa break Kisha kishindo kikubwa. Nilipochungulia nikaona gari kwenye mtaro imepinduka tairi ziko juu.
Nikashuka kwenye gari ili nikatoe msaada. Nilipofika sehemu ya tukio nikakuta Ile gari haipo. Tukio hili tulishuhudia mm na mlinzi wa petrol station.
JE, HUU SI UCHAWI?
 
Nafikiri tungetumia hoja kumpinga mtoa mada, tena kwa mifano aliyoitumia naona kama ingependeza zaidi ili tupate kujifunza kuliko kumpinga tu pasipo kutoa hoja ya msingi na zenye mifano ndani yake na pia kuelezea kwa kina ni vip uchawi upo na vip unafanyika na vip unathibitika kama huo ni uchawi?

Tungeenda hivyo ingepenza sana haswa wengi wetu humu tunaamini sisi ni ma great thinkers
 
Ni saikolojia tu. Hakuna habari ya hivyo, hao wazee wa busara wanahangaika na maisha daily.
 
Tunaita wenge
 
Kumbe wachawi hawana uwezo wa kuiba Bank, inafikirisha sana.
Chakuchekesha Wachawi wengi ni masikini wa kiwango cha lami,

Unakuta mtu na Degree yake anaenda kuabudu kwenye kaburi la Babu yake aliyeishia darasa la 4
Eti Babu yake aliyepo Kaburini ambae imebaki mifupa tu ndio amsaidie kutatua matatizo yake huku Duniani.

🤣🤣
 
Juzi kati nilikuwa nasoma habari za wahindi wekundu walivyokuwa wanapigana na wazungu huko Marekani. Sasa wahindi wale walikuwa wanategemea nyati kama chakula chao, hivyo walikuwa wakiwawinda kwa akili ili wasiishe. Wazungu wao wakawa wanawawinda kupata ngozi, hivyo waliwaua hovyo na kuacha mizoga porini. wahindi wakajianda kwenda kupigana na waharibifu hao. sasa wakaenda kwa mganga wao. mganga akawatengenezea dawa kuwa wakipigwa risasi, risasi zitayeyuka(Kama Kinjeketile tu). walipoenda vitani walipigwa vibaya na wengi wakafa. waliporudi walimghadhabikia sana yule mganga.

Cha ajabu hadi leo kuna watu wanaenda kwa waganga wawape dawa za kuzuia risasi. Haya ni maswala ya watu wajinga.
 
Chuma ulete ipo ila ni uchawi wa kimasikini sana chuma ulete inakusaidia kupata pesa ndogo ndogo tu ambazo huwezi kununua chochote cha maana zaidi ya chakula tena cha kawaida kabisa
Kama ukisoma maandiko vizuri kuna makumi ya aya yanayozungumzia uchawi kama hii kwenye matendo 8: 9-11
Lakini katika mji huo alikuwepo mtu mmoja aitwaye Simoni, ambaye alikuwa mchawi. Kwa muda mrefu alikuwa amewapumbaza na kuwashangaza watu kwa mazingaombwe, akawa anajigamba kuwa yeye ni mtu maarufu. 10 Watu wa tabaka zote, wakubwa kwa wadogo, walivu tiwa sana naye, wakawa wanasema, “Bila shaka mtu huyu ndiye ile nguvu ya Mungu iitwayo ‘Uwezo Mkuu.’ ” 11 Wakamsikiliza kwa makini kwa sababu aliwastaajabisha kwa mazingaombwe yake...
 
Hapana mkuu kuna kitu hakipo sawa kwako .......huenda hujaitembea hii tanzania vizuri....tembea ujifunze ya walimwengu
Mitaa niliyokulia inasifika kwa uchawi mji mzima. Yaani ndiyo top ukitaja uchawi mji mzima. Na mji niliokulia una sifa za kutosha kuhusu uchawi. Lakini sijawahi kuona huo uchawi. Zaidi zaidi ni watu kushutumiana.
 
Hasa kama akisema Anamwamini Mungu lakini haamini katika uwepo wa uchawi
Ukishamwamini Mungu ushaamini Uchawi Upo. Wafuasi wa Yesu na Mohammad wanapenda kujitoa ufahamu sana katika hili tena bora hata wa Mohammad wanaelewa hili wa Yesu kuna baadhi ndio wanajizima data kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…