Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Katika watu wajinga, nafikiri wanaoamini habari za kichawi wanaongoza. Nimekuja kugundua kuwa mambo mengi yanayoaminika kutokana na uchawi, yanaaminika hivyo sababu ya watu kuwa wajinga. Nitoe mifano.

1. Kuna mtu alikuwa anapata kinyesi cheusi. sasa sababu ya ujinga akawa anaamini amerogwa. Lakini kumbe kile kinyesi cheusi ni dalili ya vidonda vya tumbo, na ule weusi ni madini chuma kutoka kwenye damu inayomvuja tumboni.
2. Mtu mwingine akasema wazungu nao wachawi sana. kuna kijiji watu walikuwa wanakufa kwa radi. Mzungu akaja akasimamisha kamnara tu radi ikaacha kuua watu.
3. Wengi wanaamini vichaa wanaotembea barabarani wamerogwa. Lakini vichaa karibu vyote vinatokana na vichocheo kuyumba au kujeruhiwa kwa ubongo.
4. Watu wanaamini bundi wanatumiwa na wachawi sababu wanatembea usiku. Lakini tunajua uwezo wa bundi kuona usiku ndiyo unamuwezesha kufanya mawindo yake usiku.
4. Watu kwa ujinga wa kushindwa kupiga hesabu za mapato na matumizi, na kuweza kutunza pesa wanasingizia chuma ulete.
7. Magonjwa mengi hapo zamani yalidhaniwa kuwa yanatokana na kurogwa. Lakini sababu zake hasa zimekuja kufahamika. ujinga ndiyo ulifanya watu waamini kuna kurogwa. Kuna mchezaji amefariki juzi mguu unaoza yeye anasema ametupiwa jini.
8.Kanuni za kilimo zinajulikana lakini unakuta kuna watu wanaamini mtu anaweza kuroga apate mazao mengi, au akakuroga usipate mazao ya kutosha.
9.Madini yanapopatikana na jinsi ya kuyachimba huwa inafahamika, l;akini watu huwa wanaamini yanapatikana kwa uchawi.
10. Mara kuna uchawi wa kuleta mvua na hali habari ya ujio wa mvua na kutokuja zinajulikana.
11. Wengine wanaamini uchawi unaweza kukusaidia kwenye uvuvi.
12. wengine wanasema kuna wachawi huwa wanaingilia watu kingono!!1!

Kiufupi, wajinga wakishindwa kuelewa kitu wanasingizia uchawi. Hakuna kitu kinafunua ujinga wa mtu kama imani yake juu ya habari za kichawi. Jinsi ilivyo kali ndivyo ujinga wake ulivyo mkali zaidi.
Subiri yakukute ndo utajua
 
Sasa yeye na wewe unayeamini kuwa radi huwa inataga mayai nani kichwa maji?
Acha upimbi nani amesema kuhusu hayo masuala ya radi onyesha nilisema kuhusu habari za radi, kumbe hapa najadiliana na bogus bila kujua, sawa endelea na ujinga wako stupid one,
 
Yani wewe ni mpuuzi kweli, hasa ulipoanza kutoa mifano yako ndo umeharibu kabisa
 
Acha upimbi nani amesema kuhusu hayo masuala ya radi onyesha nilisema kuhusu habari za radi, kumbe hapa najadiliana na bogus bila kujua, sawa endelea na ujinga wako stupid one,
Kama huamini kuwa radi ikipiga huwa inaacha yai halafu wachawi huja kulichukua na kuliangua kwaajili ya kudhuru watu, basi huamini uchawi.
 
Fuatili story za akina nimrodi wa babeli , akina farao wa misri, mwambie mchungaji wako akusimulie sisi wengine hatutoweza
Umeeleza vizuri sana, watu wengi wamekua wakiamini hiyo dhana ya uchawi kwa kuihusisha na vitabu vya Mungu.

Tukiangalia kwa upande wa dini kilichoanza kuwepo ni dunia na mazingira yake na viumbe wengine na kisha binadamu. Dhana hii ya uchawi ilikuja kwa mwanadamu wakati alipokosa majibu yanayotokana na mazingira aliyonayo kwahiyo fikra ya uchawi ndio ilianza kabla ya dini.

Dini zilipokuja zilikuta tayari wanadamu wana dhana hii ya kuamini hicho kinachoitwa uchawi ambacho kimsingi ni kukosa majibu ya yale unayoyaona katika mazingira yako, ndipo dini zikazungumzia hilo kwa maana ya kwamba watu wasiamini dhana hizo na badala yake wamuamini Mungu.

Hakuna dini iliyohalalisha uchawi kwamba upo na ufuatwe badala yake dini zinataka watu wasiamini na wasijihusishe na uchawi.

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo uchawi ni dhana inayotokana na kukosa majibu ya yale unayopambana nayo katika maisha yako,kwa mfano, hupati ajira, timu yako inafungwa, kifo cha ghafla kwa mtu aliyekua mzima kabisa, umeona paka mweusi, hela zinapotea hovyo, umeona kuna mtu mbele yako ghafla akapotea, umeugua muda mrefu na huponi na hospitali hawaoni tatizo

Katika imani ya dini ukiona tukio lisilo na majibu unatakiwa uamini ni kwa uwezo wa Mungu, na wakati mwingine matukio mengi yana majibu ila huyaoni kwa sababu umeshiba imani ya uchawi.
 
Una orodha yao wote? Maana mchawi hajitangazi wala hajitambulishi.. By the way ni sawa na kusema wote wanaoenda hospital lazima wapone
Sina orodha lakini tungeshasikia hata hizo stories kuwa inawezekana lakini hazipo.
 
Back
Top Bottom