Umeeleza vizuri sana, watu wengi wamekua wakiamini hiyo dhana ya uchawi kwa kuihusisha na vitabu vya Mungu.
Tukiangalia kwa upande wa dini kilichoanza kuwepo ni dunia na mazingira yake na viumbe wengine na kisha binadamu. Dhana hii ya uchawi ilikuja kwa mwanadamu wakati alipokosa majibu yanayotokana na mazingira aliyonayo kwahiyo fikra ya uchawi ndio ilianza kabla ya dini.
Dini zilipokuja zilikuta tayari wanadamu wana dhana hii ya kuamini hicho kinachoitwa uchawi ambacho kimsingi ni kukosa majibu ya yale unayoyaona katika mazingira yako, ndipo dini zikazungumzia hilo kwa maana ya kwamba watu wasiamini dhana hizo na badala yake wamuamini Mungu.
Hakuna dini iliyohalalisha uchawi kwamba upo na ufuatwe badala yake dini zinataka watu wasiamini na wasijihusishe na uchawi.
Kama nilivyoeleza hapo mwanzo uchawi ni dhana inayotokana na kukosa majibu ya yale unayopambana nayo katika maisha yako,kwa mfano, hupati ajira, timu yako inafungwa, kifo cha ghafla kwa mtu aliyekua mzima kabisa, umeona paka mweusi, hela zinapotea hovyo, umeona kuna mtu mbele yako ghafla akapotea, umeugua muda mrefu na huponi na hospitali hawaoni tatizo
Katika imani ya dini ukiona tukio lisilo na majibu unatakiwa uamini ni kwa uwezo wa Mungu, na wakati mwingine matukio mengi yana majibu ila huyaoni kwa sababu umeshiba imani ya uchawi.