Hali Ikiendelea hivi, Nitamuunga Mkono Rais Magufuli

Hali Ikiendelea hivi, Nitamuunga Mkono Rais Magufuli

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
HALI IKIENDELEA HIVI, RASMI NITAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI.

Kwa Mkono wa Robert Heriel

Mimi ni moja ya aina za watu ambao wana misimamo isiyoyumba, wenye kupenda ukweli na kupenda haki na kuitenda. Nimejibainisha hivyo mara nyingi kama sio zote. Ni wale tusio na unafiki na tusio angalia uso wa mtu pale tunapoongea jambo lenye haki au lenye ukweli. Na kama jambo hatuna uhakika nalo huwaga hatulipi nafasi kubwa sana zaidi ya kulitolea maoni tuu.

Mhe. Rais Magufuli ni moja ya Marais ambao wanajitahidi sana, niliwahi kusema kuwa, Mhe. Rais John Pombe Magufuli, ni Rais mzuri ambaye anapambana kuwa Rais bora. Niliwahi andika pia, Rais Magufuli, hawezi kuwa Rais bora ikiwa hatarekebisha baadhi ya malalamiko kutoka mtaani, atabaki kuwa Rais wa kawaida kama walivyo marais wengine. Tena nikaongezea kuwa, kama hatafanya marekebisho kidogo basi hata huo uzuri utaondoka na atakuwa Rais duni kuliko wote waliowahi kupita.

Nina Mkubali sana Mhe. Rais Magufuli kwa sababu kwa kiasi kikubwa tunafanana tabia, mambo mengi anayoyafanya yapo kwenye akili yangu, lakini yapo ambayo bado hajayafanya na nafikiri hatayafanya kabisa.

Ninampenda Magufuli kwa sababu anamisimamo ya Kiume kama mwanaume. Hilo ni jambo la kwanza linalonifanya nimkubali. Kikawaida Mimi ninapenda watu wenye misimamo kwani nafahamu huwaga sio wanafiki.

Ninampenda Magufuli kwa sababu hana shobo dundo. Magufuli hajipendekezi, hana tabia za kujikomba komba kama paka. Hiyo ni tabia muhimu sana kwenye utawala. Yaani Magufuli ajipendekeze kwako kisa wewe ni Polopesa AKA Tycoon, au Profesa kisa una madesa kichwani. Utasubiri sana. Mimi mwenyewe sina shobo dundo, hutaki kaa pembeni, ukijichanganya unapasuka na kusagika kabisa.

Ninampenda Magufuli kwa sababu hachekei upumbavu na uhuni. Leta wizi nikate mkono, kojolea kitanda nikate kikojoleo, lete mdomo nikate ulimi, lete panya road nikuletee paka road, lete ugaidi nikuletee ukaidi na umafia. Hakuna kuchekea kima.

Kilio changu kwa Magufuli katika awamu iliyopita kilikuwa suala la utekaji na mauaji. Niliongea sana kuwa hatua zichukuliwe. Nilisema kuwa Mhe. Rais anao uwezo wa kutoa tamko na kukomesha hicho kilio cha watu walalamikao. Na kama kuna jambo lililonifanya nisimpe kura Magufuli ni hilo. Sisemi nani alikuwa anafanya, bali nazungumzia hatua zilizochukuliwa, hicho ndicho kilikuwa kilio changu.

Awamu ya Pili imeanza kwa utulivu mkubwa, kilio changu nafikiri kimesikika. Awamu hii hakutakuwa na utekaji tena, hakutakuwa na mauaji tena. Na kama yatafanyika basi naamini serikali itachukua hatua madhubuti.

Hali ikiendelea hivi, ni wazi nitakuwa karibu na Rais Magufuli na serikali yake. Nitamuunga mkono kwa nguvu zote, kwa akili zote na moyo wote.

Mhe. Rais, mimi kijana wako ninafurahishwa sana na utendaji kazi wako, kilichokuwa kinakutia doa ni kama nilivyoeleza hapo juu.

Lawama najua zipo lakini zisiwe lawama kubwa zihusuzo uhai wa mtu. Nafahamu kuna changamoto za masuala ya kiutawala, najua mazengwe, njama na hila katika utawala ndio maana sikuwa natoa lawama za moja kwa moja kwani nayajua mambo hayo.

Naomba hali iendelee kama ilivyo hivi sasa. Kuhusiana na masuala ya vyama vya upinzani sina usemi, kama hawataki kujishusha hakuna sababu ya kujishusha, kama hawataki kujipendekeza hakuna sababu ya kujipendekeza. Kama hawataki kukaa meza moja hakuna sababu ya kuleta viti vya mazungumzo.

Huwezi kujishusha kwa mtu ambaye anataka kukupandia juu. Huwezi kujishusha kwa vyama vya kipuuzi vinavyoleta kiburi na ujeuri wakati lengo ni kulijenga taifa.

Kuna watu watafikiri kuwa ninatafuta teuzi, hiyo ni kutokana na ujinga na upuuzi wa akili zao. Mimi ni MTEULE tangu siku ya kwanza. Kama mnafikiri mimi ni wale wapuuzi na wanafiki wanaosubiri kusifia na kuimba mapambio ili niteuliwe mtasubiri sana. Mimi sio muimba mapambio.

Ndio maana nilisema, Rais asije kuniteua kama hapendi kuambiwa ukweli. Wala asije niweka kwenye macho yake kama hana ustahimilivu wa kuambiwa ukweli. Kazi itanishinda mapema sana. Mimi sio mtu wa kusifu tuu, bali pia kukosoa bila macho ya kupepesa. Hakuna uoga kwenye kusema ukweli.

Nasisitiza, hali iendelee hivi hivi, lawama za utekaji awamu hii zisiwepo, lawama za mauaji awamu hii zisiwepo.

Labda njama, hila za kuichafua serikali lakini hatua kali zichukuliwe kwa watakaofanya hayo.

No shobo Dundo.

Kabla sijamaliza, niseme, Hii ni nchi yetu sote, lazima tuijenge kwa pamoja. Masuala ya utengano wa kipumbavu pumbavu yasiwepo. Kama siasa ndio zinaleta utengano basi hakuna haja ya demokrasia. Nilishawahi kuandika kuwa, Demokrasia haina maana kwa watu wajinga na masikini. Nafikiri umasikini ungeondolewa na ujinga ndipo demokrasia iletwe, hakuna uhuru kwa watu wajinga na watu masikini, uhuru huo ni machafuko ndani ya jamii.

Nilisema kama ningekuwa Rais, ningefuta dini zote za kigeni, sio ukristo sio uislam, ningefuta kabisa. Na hii nafikiri ni watu wachache wangeifanya hii. Najua changamoto zake, najua upinzani ambao ningeupata lakini ningefuta hayo matamaduni ya kigeni yanayogusa imani na elimu yetu.

Utaniona mjinga lakini, mjinga ni wewe. Hushangai kwa nini hata baraza la mawaziri kutangazwa, utasikia watu wakisema sijui mbona dini fulani wamebaguliwa, yaani wapo wachache.

Masikini na mjinga hana dini. Utakuwaje nchi masikini alafu uwe na dini tena ya kigeni, sijawahi ona popote pale.

Mjinga hana dini, kwani ataabudu vitu visivyoeleweka bila kutumia akili. Atadanganywa, atatapeliwa, na mwishowe lazima awe masikini tuu.

Taifa hili ili liendelee lazima dini zote za kigeni zifutwe, demokrasia iondolewe. Kisha, watu wapewe elimu ujinga uwatoke, wafundishwe kufanya kazi na kuusaka utajiri kwa hali na mali. Wakiupata na kuwa na unafuu wa maisha ndio waletewe hiyo demokrasia na wapewe uhuru wa kuchagua kuabudu dini wazitakazo.

Narudia masikini na mjinga hana dini, na hapaswi kupewa demokrasia na uhuru.

Hata kwenye familia, baba bora hawezi kuiendesha familia yake kidemokrasia ilhali uchumi wake ni duni na elimu ni duni. Kuiongoza familia kidemokrasia wakati ni masikini na wajinga ni kuleta madhara ndani ya familia. Utashangaa vitoto vinapewa mimba za hovyo, mkeo anagaragazwa na wahuni kisa na mkasa hana akili ya kutumia uhuru wake.

Kuna mtu atasema nimechanganya mada lakini wenye akili watakuwa wamenielewa nazungumzia nini, na ujumbe huu unamhusu Mhe. Rais na wale wote wanaotarajia kwenye mamlaka huko mbeleni.

Niwatakie miisho mema ya mwaka, na kheri ya mwaka mpya.

Ndimi,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Tunduma.
 
Hizi namba huwa mnaziandika za kazi gani?

Kazi zake ni nyingi Mkuu.

Mimi ni mwandishi wa Makala, waandishi wanajua umuhimu wa mawasiliano.

Mawasiliano ni biashara
Mawasiliano ni kazi
Mawasiliano ni Connection
Mawasiliano ni elimu
Mawasiliano na Utatuzi wa migogoro n.k

Hizo hoja zinamaelezo yake na ndio sababu ya watu wote unaowaona wakiacha mawasiliano kwenye maandishi wayaandikao.

Nafikiri nimekujibu
 
131409713_1366680437172960_4026059254385485630_o.jpg
 
Unataka teuzi kwa mbinu zilezile ovu za kugawa makundi fulani. Unataka makundi fulani yakose demokrasia na kuwanyang'anya uhuru wa kuabudi kwa kutaka zifutwe dini zao. Kwaandiko hili teuzi sahau mh. Raisi kwa sasa yupo kuondoa mpasuko wa kisiasa na wa kidini uliopo wewe unataka huu mpasuko uingezeke.
 
Dini zifutwe
Demokrasia iondolewe jamii bado masikini na jinga.

Hivi huoni watu wanavyotumia uhuru vibaya?

Huko Ulaya ilipoanzia dini na demokrasia unaijua historia yake?

Embu kasome mada isemayo "Rise of Democracy in Europe"
Utanielewa, vinginevyo hakuna cha maana nitakachoweza ongea na wewe ukiwa huna ujualo kwa habari hizo.

Demokrasia kwa nchi masikini ni mtego
Dini kwenye masikini au familia masikini ni utumwa

Kuhusu Teuzi nimeshakuambia mimi ni MTEULE, ukishaelewa hiyo istilahi huna haja ya kuongea upuuzi wako.
Anayeteuliwa ni mtu ambaye hakuwa mteule na ndio maana wengi huimba mapambio, kusifu na kuabudu na kumfanya jpm kama mungu.
MTEULE hana muda huo

Utawezaje kuuimba wimbo wa Bwana ukiwa ugenini/ Utumwani?
 
Watu kama hawa wakiwepo katika jamii ujue jamii imeumia.....
Unafiki bhana shida sana.....
Unajifanya kama vile hajui watu wangapi wameuawa wamekamatwa na wanaendelea kukamatwa tangu kabla na baada ya uchaguzi....
Tafuta hotuba ya Mh Warioba na Jenerali Ulimwengu usome
Waliitoa siku ya kuadhimisha haki za Binadamu
 
Kwenye DINI hasa nimekuelewa sana kiongozi, unampa mtu kitu hakielewi ili akiabudu, ni kumuongezea kuuchezea umasikini tu.

Je, katika swala la uchumi, rate him from 1 to 10 please!(10 being the highest score)
 
Mkuu, watu wameuawa na wengi hatujui walipo, hivyo waendelee kuuawa au kupotezwa? Mbona unaakili lakini unashindwa kuelewa mantiki ya makala hii?
Nimeshasema kuwa awamu hii isiwe na mauaji, utekaji na kupotezana, hiyo ndio lengo la makala yangu. Na mpaka sasa awamu ya pili naona tunaendelea vizuri, so ulitaka nisiseme?

Kuhusu kukemea mauaji na kujeruhi, nimeshakemea na kupigia kelele jambo hilo tangu awamu ya kwanza, au wewe ndio mara yako ya kwanza kusoma makala zangu?
Kama ndio mara yako ya kwanza sikulaumu, lakini kama umeshawahi kusoma zingine basi nitakuona mwehu
 
Kwenye DINI hasa nimekuelewa sana kiongozi, unampa mtu kitu hakielewi ili akiabudu, ni kumuongezea kuuchezea umasikini tu.

Je, katika swala la uchumi, rate him from 1 to 10 please!(10 being the highest score)

Kuhusu uchumi bado sana, naona anahangaika sana, nafikiri mbinu anazotumia hazitamsaidia sana zaidi ya kuumiza Watanzania.

Nilishawahi kumuandikia waraka, nikasema, ili nchi tuondoe umasikini kwenye taifa hili lazima tujue umasikini huu tutaupeleka wapi, huwezi kuondoa umasikini bila kunyonya watu, sasa ni lazima achague kunyonya watu wa nchi yake au tuvamie nchi za wenzetu. Nilipendekeza tuvamie nchi za wenzetu tuwapelekee umasikini wetu, ujinga wetu na maradhi.

Wazungu wasingeendelea kama wasingetuletea umasikini wao, maradhi yao na ujinga wao.

Mimi ni mdogo lakini hayo mambo madogo sishindwi kung'amua
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu,hakika wewe ni mkweli.
Ukileta uzi wowote wa kumsifu JPM ama serikali kuna watu watakudhihaki na kejeli nyingi,pia ukileta uzi wa kumponda Magufuli na serikali yake utapewa na cheo kabisa cha ukamanda.
Ila penye ukweli usemwe hata kama kuna watu watachukia.
Madhaifu yapo sio kwa Magufuli pekee hata mimi na wewe atujakamilka kwa 100%.
Changamoto ni nyingi na duniani hapa uwezi kuridhisha watu wote,na hata ukitatua baadhi ya changamoto bado kuna masnitch watazitia kasoro ili tu uonekane bado hujafanya kitu.
Nyuzi zako za kumkosoa Magufuli na serikali yake ni nyingi lakini mwisho wa siku zina dira ya kuonyesha njia sahihi.
 
Mimi ni Mkweli
Nilishasema simmpigii Kura Magufuli na sikumpigia.

Nikimsema Magufuli kuna vimtu vipuuzi vinanifuata inbox na vingine kunipigia simu vikinitisha, wengne wakinipongeza.

Ninachojaribu kusema, mimi sio mfuasi wa yeyote, sio mtumwa wa Yeyote, sina chama, dini, club ya mpira, au mfuasi wa kundi lolote. Mimi ni tu huru, nafurahishwa na yeyote akifanya vizuri, na nachukizwa na yeyote anayefanya vibaya. Hilo pekee linanifanya nijivunie
 
Watu kama hawa wakiwepo katika jamii ujue jamii imeumia.....
Unafiki bhana shida sana.....
Unajifanya kama vile hajui watu wangapi wameuawa wamekamatwa na wanaendelea kukamatwa tangu kabla na baada ya uchaguzi....
Tafuta hotuba ya Mh Warioba na Jenerali Ulimwengu usome
Waliitoa siku ya kuadhimisha haki za Binadamu
Teuzi inatafutwa.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kuhusu uchumi bado sana, naona anahangaika sana, nafikiri mbinu anazotumia hazitamsaidia sana zaidi ya kuumiza Watanzania.

Nilishawahi kumuandikia waraka, nikasema, ili nchi tuondoe umasikini kwenye taifa hili lazima tujue umasikini huu tutaupeleka wapi, huwezi kuondoa umasikini bila kunyonya watu, sasa ni lazima achague kunyonya watu wa nchi yake au tuvamie nchi za wenzetu. Nilipendekeza tuvamie nchi za wenzetu tuwapelekee umasikini wetu, ujinga wetu na maradhi.

Wazungu wasingeendelea kama wasingetuletea umasikini wao, maradhi yao na ujinga wao.

Mimi ni mdogo lakini hayo mambo madogo sishindwi kung'amua
Huwa nasoma sana mabandiko yako, haupo upande wowote na kama muandishi wa makala unafanya vizuri sana. Wale wanaotaka uponde kila siku, au wanaotaka usifu kila siku nadhani wanaumia.

Magu anazingua mengi, naamini anaharibu uchumi pia coz ni kweli kuwa purchasing power ya wengi imeshuka mno, biashara nyingi mi haziendi.
 
Walioua na kuteka wamechukuliwa hatua gani kwanza bila kusahau waliopiga risasi mbunge dodoma?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom