Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HALI IKIENDELEA HIVI, RASMI NITAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI.
Kwa Mkono wa Robert Heriel
Mimi ni moja ya aina za watu ambao wana misimamo isiyoyumba, wenye kupenda ukweli na kupenda haki na kuitenda. Nimejibainisha hivyo mara nyingi kama sio zote. Ni wale tusio na unafiki na tusio angalia uso wa mtu pale tunapoongea jambo lenye haki au lenye ukweli. Na kama jambo hatuna uhakika nalo huwaga hatulipi nafasi kubwa sana zaidi ya kulitolea maoni tuu.
Mhe. Rais Magufuli ni moja ya Marais ambao wanajitahidi sana, niliwahi kusema kuwa, Mhe. Rais John Pombe Magufuli, ni Rais mzuri ambaye anapambana kuwa Rais bora. Niliwahi andika pia, Rais Magufuli, hawezi kuwa Rais bora ikiwa hatarekebisha baadhi ya malalamiko kutoka mtaani, atabaki kuwa Rais wa kawaida kama walivyo marais wengine. Tena nikaongezea kuwa, kama hatafanya marekebisho kidogo basi hata huo uzuri utaondoka na atakuwa Rais duni kuliko wote waliowahi kupita.
Nina Mkubali sana Mhe. Rais Magufuli kwa sababu kwa kiasi kikubwa tunafanana tabia, mambo mengi anayoyafanya yapo kwenye akili yangu, lakini yapo ambayo bado hajayafanya na nafikiri hatayafanya kabisa.
Ninampenda Magufuli kwa sababu anamisimamo ya Kiume kama mwanaume. Hilo ni jambo la kwanza linalonifanya nimkubali. Kikawaida Mimi ninapenda watu wenye misimamo kwani nafahamu huwaga sio wanafiki.
Ninampenda Magufuli kwa sababu hana shobo dundo. Magufuli hajipendekezi, hana tabia za kujikomba komba kama paka. Hiyo ni tabia muhimu sana kwenye utawala. Yaani Magufuli ajipendekeze kwako kisa wewe ni Polopesa AKA Tycoon, au Profesa kisa una madesa kichwani. Utasubiri sana. Mimi mwenyewe sina shobo dundo, hutaki kaa pembeni, ukijichanganya unapasuka na kusagika kabisa.
Ninampenda Magufuli kwa sababu hachekei upumbavu na uhuni. Leta wizi nikate mkono, kojolea kitanda nikate kikojoleo, lete mdomo nikate ulimi, lete panya road nikuletee paka road, lete ugaidi nikuletee ukaidi na umafia. Hakuna kuchekea kima.
Kilio changu kwa Magufuli katika awamu iliyopita kilikuwa suala la utekaji na mauaji. Niliongea sana kuwa hatua zichukuliwe. Nilisema kuwa Mhe. Rais anao uwezo wa kutoa tamko na kukomesha hicho kilio cha watu walalamikao. Na kama kuna jambo lililonifanya nisimpe kura Magufuli ni hilo. Sisemi nani alikuwa anafanya, bali nazungumzia hatua zilizochukuliwa, hicho ndicho kilikuwa kilio changu.
Awamu ya Pili imeanza kwa utulivu mkubwa, kilio changu nafikiri kimesikika. Awamu hii hakutakuwa na utekaji tena, hakutakuwa na mauaji tena. Na kama yatafanyika basi naamini serikali itachukua hatua madhubuti.
Hali ikiendelea hivi, ni wazi nitakuwa karibu na Rais Magufuli na serikali yake. Nitamuunga mkono kwa nguvu zote, kwa akili zote na moyo wote.
Mhe. Rais, mimi kijana wako ninafurahishwa sana na utendaji kazi wako, kilichokuwa kinakutia doa ni kama nilivyoeleza hapo juu.
Lawama najua zipo lakini zisiwe lawama kubwa zihusuzo uhai wa mtu. Nafahamu kuna changamoto za masuala ya kiutawala, najua mazengwe, njama na hila katika utawala ndio maana sikuwa natoa lawama za moja kwa moja kwani nayajua mambo hayo.
Naomba hali iendelee kama ilivyo hivi sasa. Kuhusiana na masuala ya vyama vya upinzani sina usemi, kama hawataki kujishusha hakuna sababu ya kujishusha, kama hawataki kujipendekeza hakuna sababu ya kujipendekeza. Kama hawataki kukaa meza moja hakuna sababu ya kuleta viti vya mazungumzo.
Huwezi kujishusha kwa mtu ambaye anataka kukupandia juu. Huwezi kujishusha kwa vyama vya kipuuzi vinavyoleta kiburi na ujeuri wakati lengo ni kulijenga taifa.
Kuna watu watafikiri kuwa ninatafuta teuzi, hiyo ni kutokana na ujinga na upuuzi wa akili zao. Mimi ni MTEULE tangu siku ya kwanza. Kama mnafikiri mimi ni wale wapuuzi na wanafiki wanaosubiri kusifia na kuimba mapambio ili niteuliwe mtasubiri sana. Mimi sio muimba mapambio.
Ndio maana nilisema, Rais asije kuniteua kama hapendi kuambiwa ukweli. Wala asije niweka kwenye macho yake kama hana ustahimilivu wa kuambiwa ukweli. Kazi itanishinda mapema sana. Mimi sio mtu wa kusifu tuu, bali pia kukosoa bila macho ya kupepesa. Hakuna uoga kwenye kusema ukweli.
Nasisitiza, hali iendelee hivi hivi, lawama za utekaji awamu hii zisiwepo, lawama za mauaji awamu hii zisiwepo.
Labda njama, hila za kuichafua serikali lakini hatua kali zichukuliwe kwa watakaofanya hayo.
No shobo Dundo.
Kabla sijamaliza, niseme, Hii ni nchi yetu sote, lazima tuijenge kwa pamoja. Masuala ya utengano wa kipumbavu pumbavu yasiwepo. Kama siasa ndio zinaleta utengano basi hakuna haja ya demokrasia. Nilishawahi kuandika kuwa, Demokrasia haina maana kwa watu wajinga na masikini. Nafikiri umasikini ungeondolewa na ujinga ndipo demokrasia iletwe, hakuna uhuru kwa watu wajinga na watu masikini, uhuru huo ni machafuko ndani ya jamii.
Nilisema kama ningekuwa Rais, ningefuta dini zote za kigeni, sio ukristo sio uislam, ningefuta kabisa. Na hii nafikiri ni watu wachache wangeifanya hii. Najua changamoto zake, najua upinzani ambao ningeupata lakini ningefuta hayo matamaduni ya kigeni yanayogusa imani na elimu yetu.
Utaniona mjinga lakini, mjinga ni wewe. Hushangai kwa nini hata baraza la mawaziri kutangazwa, utasikia watu wakisema sijui mbona dini fulani wamebaguliwa, yaani wapo wachache.
Masikini na mjinga hana dini. Utakuwaje nchi masikini alafu uwe na dini tena ya kigeni, sijawahi ona popote pale.
Mjinga hana dini, kwani ataabudu vitu visivyoeleweka bila kutumia akili. Atadanganywa, atatapeliwa, na mwishowe lazima awe masikini tuu.
Taifa hili ili liendelee lazima dini zote za kigeni zifutwe, demokrasia iondolewe. Kisha, watu wapewe elimu ujinga uwatoke, wafundishwe kufanya kazi na kuusaka utajiri kwa hali na mali. Wakiupata na kuwa na unafuu wa maisha ndio waletewe hiyo demokrasia na wapewe uhuru wa kuchagua kuabudu dini wazitakazo.
Narudia masikini na mjinga hana dini, na hapaswi kupewa demokrasia na uhuru.
Hata kwenye familia, baba bora hawezi kuiendesha familia yake kidemokrasia ilhali uchumi wake ni duni na elimu ni duni. Kuiongoza familia kidemokrasia wakati ni masikini na wajinga ni kuleta madhara ndani ya familia. Utashangaa vitoto vinapewa mimba za hovyo, mkeo anagaragazwa na wahuni kisa na mkasa hana akili ya kutumia uhuru wake.
Kuna mtu atasema nimechanganya mada lakini wenye akili watakuwa wamenielewa nazungumzia nini, na ujumbe huu unamhusu Mhe. Rais na wale wote wanaotarajia kwenye mamlaka huko mbeleni.
Niwatakie miisho mema ya mwaka, na kheri ya mwaka mpya.
Ndimi,
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Tunduma.