Hali ilivyo nchini Somalia

hawa wanaokotwa kwenye mafuso kila siku hawayaoni hayo maisha bora? wewe tu ndo uliyeona?
 
Goja nikuletee ushadi kabisa.maana wengine ni wabishi kuamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku marehemu, Nchi ina watu waoga sana kuliko nchi yoyote chini ya jua
 

Sikuwa na nia ya kukujibu lakini ningeacha kuku-quote usingeona post yangu. Nakiri sikufahamu lakini siogopi kukuita MUONGO na MZANDIKI.

Uko sahahi kuhusu bei za vyakula na bidhaa za mafuta. Ziko chini kwa sababu ya ukaribu na vyanzo vikuu vya mafuta. Kwa ujumla bei za hapa ziko chini kwa sababu nchi haina mfumo imara wa kulipa kodi. Bidhaa nyingi zinaingizwa kimagendo. Sehemu yoyote yenye bidhaa za magendo - bei ziko chini. Hii ndio nchi inayoongoza kwa kuingiza bidhaa feki kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa za hovyo kutoka nchi ambazo sitazitaja hapa!!

Uongo na uzandiki wako uko katika maeneo haya - barabara na umeme. Na kuwa Somalia inaendelea kuliko Tanzania. Nchi isiyokuwa na maji inazalishaje umeme? Wa mafuta au nyuklia? Au umesikia kampuni ya Beco kutoka uturuki yenye majenereta ndio ukadhani ni issue kubwa?? Nchi hii imejaa wazalishaji wa umeme wa jenereta zinazohudumia mtaa mmoja au miwili na mnamlipa mwenye jenereta!! Nchi hii haina barabara za lami kuunganisha states. Njia kuu ya usafirishaji ni kwa njia ya anga. Na kama unasafirisha kwa barabara kwenda mikoani kwenye barabara za vumbi lazima ufanye kipindi cha kiangazi kwa tena kwa kuwalipa alshabab. Hii ni nchi ambayo haina barabara zinazounganisha nchi jirani.

Waambie wasomaji kuwa njia pekee ya mtu kuingia Somalia ni kwa anga tu. Hakuna reli, barabara wala meli kwenda popote nje ya Somalia.

Hospitali. Asilimia 99 ya hospitali ni binafsi. Ndio unalinganisha na Tanzania?? Serikali haina uwezo hata wa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake - inawezaje kuwa na hospitali zinazofanya kazi!! Huwezi kusikia maji ya bomba hapa. Chimba kisima chako.

Ninachukulia post yako kama ni maoni ya mtu anayefika sehemu akawa na dhana zisizokuwa na msingi! Akaondoka na impressions zisizokuwa na facts nyuma yake.

Declaration of interests: Nimeishi nchi hii miaka 11 sasa. Nimeishi hata huko kwenye states, sio Mogadishu tu. Na uliyosema hapa ni uongo mtupu!!
 
Vip Jiji la Mogadishu ni zuri kuliko Dar mkuu?!...just curious to know !

Mkuu, ningekuwa naweza kufananisha na miji yetu ya Tanzania - ungepata picha halisi lakini sitaki watu wa miji hiyo wajione vibaya.

How about this - asilimia 80 ya nyumba za kuishi za wakazi wa Mogadishu ni zile full suit (mabati pande zote). Sasa fikiria hiyo kwenye joto ambalo huenda hadi nyuzi 39!!

Our Dar is heaven compared to this place!! Jamaa kasema uongo mwingi sana!
 
Jiji la Mogadishu ni zuri na limepangika.ila kwa udogo ni dogo ukilinganisha na jiji la Dar

Bro, nimekaribia kukuumbua. Acha uongo!! Nitakuuliza umefika Mogadishu ipi wakati, au AIAA tu. Hata kama ni hapo, hapajapangwa kuliko Dar.

Waambie watu kuwa runway ya uwanja wa ndege wa Mogadishu iko less that 200 meters kutoka private properties!! Halafu unasema huo ni mpangilio.
 

Uko sahihi kabisa kuhusu hili. Ninaishi hapa kwa miaka 11 sasa!! Wanapima viwanja na vinatambulika hata kama havijajengwa.

Mleta mada anasema uongo kuwa Somalia imeendelea kwa umeme, barabara, hospitali nk. Anajenga picha kuwa Somalia inatuzidi kimaendeleo. Je unaona hilo ni sahihi?? Sijajua amefika sehemu gani ya nchi hii inayozidi Tanzania, pamoja na ujenzi wetu holela - vipi quality ya nyumba zenyewe?? Nyumba za mabati ndio zinazidi zetu?
 
Somalia umekwenda mbali mno.

Hapo Zenji tu maisha ni matamu kuliko hapa Tozo kantri.

Majambawaka yamekamata fursa.
 
Naunga mkono hoja yako mkuu.
 
Wajinga watakwambia hamia huko
 
Japo picha kwa karne hii story bila picha sw na takataka tu
 
Vipi totoz za kisomali unakula
 
Kama ni hivyo mbona wasomali wanapita hapa nchini kwetu kuelekea Afrika Kusini? Ni nini kinachowakimbiza huko kwao ambako kwa maelezo yako kunafaa kuishi?
 
Ki ukweli huu ndio ulitakiwa kua utaratibu wa kila mji. Hakuna kuanzisha makazi kabla maeneo hayajapimwa.

Sisi kwetu tunasubiri watu wajenge ndo tuanze kupima sijui kusema hapa bomoa. Haijakaa sawa kabisa.

Ilitakiwa sehemu zipimwe miundo mbinu kama balabala itangulie, hata kama sio kiwango cha rami kabisa inasaidia sna kupanga maeneo vizuri nakupunguza gharama za kubomoleana nyumba na kulipana fidia

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…