Hali inatisha, Uswahilini Dar es salaam watu wamepigika na maisha mpaka basi. Nyuso zimekosa nuru

Hali inatisha, Uswahilini Dar es salaam watu wamepigika na maisha mpaka basi. Nyuso zimekosa nuru

Daaah kweli, kuna watu wanaishi maisha magumu sana. Kuna mama mmoja alinivaa hivi majuzi natoka tu nje ya nyumba napoishi akanisimulia mambo mengi ya kuumiza sana.
Akaniomba nimsaidie hata unga nusu akawasongee watoto wake ugali. Hii kitu iliniumiza sana, nilimsaidia kwa uwezo wangu.
 
Wacha maisha yawapopoe hayo mafala ndio yanakata mauno likipita gari la CCM! Kwasasa hakuna masikini waTanzania ambaye namuonea huruma ikiwa kwa kiwango kikubwa wao ndio mtaji mkubwa wa maccm
 
Hivi kwa msuguli ni uswazi? Pale mbna ushuani, nikaweza kuishi maji matitu, ndo nishindwe huko? Lol
😂😂😂😂
Kila mahali huwa kuna uswahilini kwake na ushuani pia haimaanishi wote wanaoishi eneo fulani watakuwa na hali zinazo lingana.
Unaweza ona majimatitu ndio sehemu ya chini kabisa ila kuna sehemu nyengine ukafika ukaona bora kule kuna afandhali.
 
Wee em sema kweli?
 
Dar wanaishi madaraja yote, kuanzia wa level za chini kabisa hadi watu wenye ukwasi wa kutisha.

Kuna vyakula vya kuanzia shilingi mia tano kwa sahani, so kila mtu anamudu lwa level yake.
Dar kila kitu kipo kwa wingi, wapuuuzi kuliko wote kwa wingi wapo Dar and vise versa, masikini kuliko wote kwa Bing wapo Dar, lakini matajiri kuliko wote kwa wingi wapo Dar, Yan iko hivyo
 
Ukiwa na life hiyo,Hama mapema maana utaishia kulogwa maana uswahilini hatupendi maendeleo.
Ila kuishi uswaz ni kazi!! Kuna muda life inakuchapa maskani muda wote unapatikana. Sasa inatokea Mungu anakupa kidogo mwanga wa mafanikio, hapo unaza kupata ubize Fulani hivi, maskani na kitaa haupatikani km mwanzo. Hapo Sasa maneno ya kiswahili yanaza, anaringa siku hizi, amepata mshangazi, wakikuchoka sana wanakuambia umepata basha la kiarabu mjini.
 
Dar wanaishi madaraja yote, kuanzia wa level za chini kabisa hadi watu wenye ukwasi wa kutisha.

Kuna vyakula vya kuanzia shilingi mia tano kwa sahani, so kila mtu anamudu lwa level yake.
Hadi 30000 kwa sahani, hawa wanauziwa madara tofauti
 
Ila kuishi uswaz ni kazi!! Kuna muda life inakuchapa maskani muda wote unapatikana. Sasa inatokea Mungu anakupa kidogo mwanga wa mafanikio, hapo unaza kupata ubize Fulani hivi, maskani na kitaa haupatikani km mwanzo. Hapo Sasa maneno ya kiswahili yanaza, anaringa siku hizi, amepata mshangazi, wakikuchoka sana wanakuambia umepata basha la kiarabu mjini.
Masikin wengi hawataki kuona ukifanikiwa, wanataman kukuona ukibakia hapo hapo kwenye. So ukitoka maneno yanaanza, ni namna yao ya ku cope na ww japokuwa umewaacha
 
Kama kawaida nikatia chimbo Uswahilini nyuma ya JNIA almaarufu airport.

Aisee watu wamechakaa hatari. Vijana kama wazee, wamama na wadada wamekaa vibarazani asubuhi tu ukipita macho yao yote kwako.

Sura zao zinaonyesha hawapati milo 3 kwa siku.

Serikali iangalie, mtu mwenye njaa hawezi kumzaa na kumlea mtoto akafanikiwa.

Reformation of economic policy ni kitu muhimu sana kwa sasa kuliko mauchaguzi yanayomeza mabilioni
Hiyo hali Iko kila mahali,ukienda Kaliakoo aggrey unaona mbele zaidi ya mita 120,hii ni zaidi ya hatari ukienda Mwanjelwa Mbeya ukisimama kwa mfekemo unona Hadi barabara kubwa,ukiwa Kilombero kona ya geti la uwanja unaona mpaka sokoni na ukiwa barabara ya kwenda kiwandani unaona mpaka kwa Mik,sasa Hawa watawala wako ndani ya gari za bilioni Moja hawafanyi hata assessment,hatuwezi kuwa na taifa linaongoza kwa kukosa furaha alafu wajuba wa Lmbmba wanasema mambo safi,jitahidini tupate Traole wetu hali ni Tete,huku kwenye utumishi wa uma bajeti zinaxheza kama MZANI hazijatulia,inakuwaje tulee toto kubwa na zima kama Zanzibar,kibaya zaidi huko Zanzibar nao hali ni Tete,nilikuwa huko,watu hawafanyi Biashara wanakwenda huku na huko hawanunui sababu nao Kuna vitu wanauza havitoki.
Mazao ya wakulima kama avocado,Ndizi ,Kokoa na Mbao bei ni mbovu haya ya msimu hayana shida,wavuvi wanatumia vimtumbwi vya ajabu katikati ya Jiji kama mwanza na hakuna mtu anajari wao wanakimbizwa kwenye gari za mabilioni,Please we need our own Traole for real.
 
Kama kawaida nikatia chimbo Uswahilini nyuma ya JNIA almaarufu airport.

Aisee watu wamechakaa hatari. Vijana kama wazee, wamama na wadada wamekaa vibarazani asubuhi tu ukipita macho yao yote kwako.

Sura zao zinaonyesha hawapati milo 3 kwa siku.

Serikali iangalie, mtu mwenye njaa hawezi kumzaa na kumlea mtoto akafanikiwa.

Reformation of economic policy ni kitu muhimu sana kwa sasa kuliko mauchaguzi yanayomeza mabilioni
Dar ukiishi uswahilini lazima uchanganyikiwe tu. Nyumba ni msingamano hakuna hewa nzuri, kwenye daladala full kupakana jasho, mlo ni miguu na utumbo wa kuku halafu maji ya kunywa hayaeleweki ni ya mtaro au kisima. Dar vichaa ni wengi ila hawajapimwa tu.
 
Ukiwa na uwezo wa kununua utumbo wa kuku na supu za mapupu uswazi utapata wanawake wengi

Kwa nini kupata wanawake wengi? nakushauri badili mtazamo wako .
Kwa nini isiwe kupata nguvu ya kuendelea kujishughulisha zaidi ili kujiongezea kipato
 
Back
Top Bottom