Hali ngumu sana mtaani, unaweza kuuawa kwa sababu ya Elfu 20

Hali ngumu sana mtaani, unaweza kuuawa kwa sababu ya Elfu 20

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2019
Posts
2,338
Reaction score
5,271
Tukiacha kundi dogo la Viongozi wa Kisiasa wa Chama kilichojimilikisha madaraka, kwa kweli hali ya maisha kwa Wananchi ni ngumu sana huku mtaani,tuache kuvunga..

Hela hakuna wakuu, Ukitoka nyumbani na sh. laki moja unarudi huna hata sh. 100...bila shaka hali hii hainikabili mimi peke yangu

Hela hakuna mazee, Mishahara haitoshi na vimiradi vya kijasiriamali tunayojaribu pia vinakufa katika mazingira ya kustaajabisha sana

Ukikutana na Vijana waliomaliza Vyuo miaka miwili-mitatu iliyopita Utawaonea huruma, wamechoka, wamekonda, hawana tumaini...

Wafanyakazi wa Sekta ya Umma wako hoi

Wafanyabiashara taabani

Saivi unaweza kuviziwa getini kwako ukala shaba kisa tu Sh. elfu 20...

Hali ni ngumu sana, sema inaelekea wengi tumeamua kufa na tai shingoni..
 
Miaka ya 90 nilikuwa pale Tanga mjini. Siku moja rafiki yangu wa kizungu alinialika pale Mkonge Hotel. Tulikaa Kule uani tukiburudika na upepo wa bahari ya Hindi. Akaja muhudumu, akaniambia niagize chakula ninachotaka, nikaagiza naye akaagiza chakula chake.
Akaniuliza kuhusu kinywaji, nikamwambia ninachokunywa, akaniagizia na yeye akaagiza cha kwake.

Tukaendelea. Ikafika round ya tatu, nikaona siyo uungwana, nikaita: "Waiter tafadhali njoo" Mzungu wangu kala ganzi tu anasubiri kitakachofuata. Nikamwambia Waiter: "Hebu tuletee mbilimbili hapa" Daaa!! Ile waiter anageuka tu, Mzungu wangu alisimama juu taap!!

"No no no no!! Camoon!!! It's me who invited you! What are you doing? Kusema kweli Mzungu wangu alikasirika sana. Nikamwomba msamaha sana.

Somo: Kuna usemi unasema: " Pesa bila daftari hupotea bila habari"
Nadhani nimeeleweka.
 
Hahahahaha.. nimecheka kinomaa..bt u have point..sometimes hadi mtu unahisi n chumaulete kumbe fweza tu haielewek..elaa tunatafuta sana..ukiipata na yenyew haikui..daah
 
Mi mwenyewe sielewi elewi

Nachojutia sijujipanga na wakati huu maana ilitakiwa tu niangalie Hali mbele inakuwaje halafu niwekeze , nikahisi mambo yatakuwa yale yale kumbe doh
 
Miaka ya 90 nilikuwa pale Tanga mjini. Siku moja rafiki yangu wa kizungu alinialika pale Mkonge Hotel. Tulikaa Kule uani tukiburudika na upepo wa bahari ya Hindi. Akaja muhudumu, akaniambia niagize chakula ninachotaka, nikaagiza naye akaagiza chakula chake.
Akaniuliza kuhusu kinywaji, nikamwambia ninachokunywa, akaniagizia na yeye akaagiza cha kwake.
Tukaendelea. Ikafika round ya tatu, nikaona siyo uungwana, nikaita: "Waiter tafadhali njoo" Mzungu wangu kala ganzi tu anasubiri kitakachofuata. Nikamwambia Waiter: "Hebu tuletee mbilimbili hapa" Daaa!! Ile waiter anageuka tu, Mzungu wangu alisimama juu taap!! "No no no no!! Camoon!!! It's me who invited you! What are you doing? Kusema kweli Mzungu wangu alikasirika sana. Nikamwomba msamaha sana.
Somo: Kuna usemi unasema: " Pesa bila daftari hupotea bila habari"
Nadhani nimeeleweka.
Unataka kusema wewe peke yako ndo uko makini na matumizi unayofanya? Hali ni ngumu Wacha kujikuta
 
Back
Top Bottom