Hali ni mbaya, kazi yoyote inahitajika

Hali ni mbaya, kazi yoyote inahitajika

Upo wap mkuu
Kutoka hapo ulipo tafuta namna ufike iringa town......
Kisha ingia stend ya zamani
Zama kwenye ndinga yoyote inayofika migori
Kisha njoo kuna watu wanamitumbwi huku haina watu wakuvulia samaki
Nb kilo ya samaki kwa sasa ni 4500
Nb kwenye maji kuna KIBOKO NA MAMBA WAKUTOSHA!
Hahahahaha hio sentensi ya mwisho ya wadudu hao ndio sababu ya mitumbwi haina watu!
 
Pale garda wamepakana na kampuni ya wachina ya ulinzi pia kuna nafasi za kazi leo nimeenda nikaona tangazo kampuni inaitwa huayuan security
Boss sisi wengine ni wageni mikocheni, naomba Location vizuri ili nifike
 
Nina rafiki yangu ni kijana wa kiume 24-25 nidaktari akienda jkt akarudi nyumbani connection ngumu,Kama yupo mwenye uhitaji wa mtu huyu clinical officer plz pm tumsaidie hata apate pesa ya kula na kuvaa.yupo Arusha.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Kazi yenye demand kubwa sana huko ambayo ni rahisi kupata ni content writing.

Ukienda Fiverr, ukajisajili unaandika makala. Pricing weka hata $5 kwa 500 words na $10 kwa 1,000 words.

Utapata orders mpaka ushindwe mwenyewe.

Muhimu ujue English na namna blog posts zinaandikwa, na ni kitu rahisi tu.

Kwa mwezi unaweza kujikuta unakunja mpaka $500 kirahisi tu.
Mkuu hua una positive comments sana kwny issue za fiver na upwork. Hua nafatilia sana comment zako na za Nafaka. Hongereni
 
Back
Top Bottom