Hali ni mbaya, kazi yoyote inahitajika

Hali ni mbaya, kazi yoyote inahitajika

Pale garda wamepakana na kampuni ya wachina ya ulinzi pia kuna nafasi za kazi leo nimeenda nikaona tangazo kampuni inaitwa huayuan security
Hapo huayan kutakuwa na mishahara ya kimasai bila shaka na ubabaishaji mwingi kwenye kulipana hela
 
Yah Mimi mwenyewe nina taaluma yangu lakini nipo kwenye ulinzi nimekosa garda ila Leo nimepata kampuni nyingine ya ulinzi nimetumia cheti Cha kidato Cha 4 na nina familia watoto wataishi vp napiga lindo mwanaume wanangu wanakula lakini mtu yupo single analialia
Binafsi maisha yangu nayajua mimi mwenyewe, hakuna mtu yeyote anaeweza kucontrol maisha yangu.

Maisha ya wabongo wengi bado ni magumu. Nashangaa unakuta mtu anamcheka mwingine eti ni mlinzi wakati ukimwangalia yeye wewe una afadhali.

Mfano huko Garda wanapima urefu, kuna watu wanapimwa wanakutwa wafupi, wiki inayofuata wanaenda tena ( yaani mtu anahisi ameshakua )

Kuna vitu unaweza kuviona ni vya kawaida ila kuna watu wanatumia nguvu sana kuvitafuta, kuvipata au wanaishia kutokuvipata kabisa.
 
Zile za kubid niliona wananiletea habari sijui za kulipia hela ya nini nikaona wezi hawa 🤣🤣🤣 nikakimbiaga
Ela za kununua bids, uwa wanatoa za bure zikiisha ukiwa wataka wanunua kama hutaki zitajiongeza baada ya masaa. Yes kazi za $5 zimekuwa nyingi na wanazigombea. Ndiyo maana nimejikita zaidi kwenye masuala mengine kma subtitling za movies zinazoonyeshwa Netflix
 
Nafasi zipo garda hata Mimi nimetoka huko leo nafasi zipo
Mkuu, nakuthibitishia haya makampuni ya ulinzi leo watu wanadharau ila hii kazi itakuwa ni kimbilio la watu miaka 5 au 10 ijayo.

Mimi leo nina NSSF kama 2.5M kama ningetaka bima ningechukua, likizo ninapewa tena yenye malipo.

Yaani hata kama ni kujiajiri nina kianzio kabisa.
 
Ingia kupitia browser, then search kama guest.

Usikopi na kupaste. Just write in your own way. Chukua idea tu na format.

Hata contents tunazoandika huwa hatutoi kichwani kwa 100%.

Ukishakuwa na keywords unaingiza Google, unaona wengine wanaandikaje.

Then wewe unaandika upya ( rewrite ) in your own way kukwepa plagiarism. Ukiongeza na majibu ya maswali ya watu wanayouliza Google utakayoyaona kupitia search results tayari una maneno zaidi ya 1,000.
Mfano nipo Iringa watanilipa kwa njia gani baada ya kazi? Pia lazima niwe na pc? au simu tu inatosha.
 
Mkuu kumbe na wewe ni mdau wa hizi mambo. Mimi Fiverr siko active sana kule hivyo siwezi kukupa ushauri, mimi zaidi ni Upwork, Freelancer na LinkedIn.
Mkuu kama nina simu tu sina pc nitaweza hizi kazi?
 
Kama we mtalaam, basi ina uhitaji mkubwa sana hasa kwa wanaotengeneza video za YT. Mtu akupe video ya madakika au masaa uedit iwe ya dakika kadhaa ni wengi kwe hizi freelancing platform
Daah sasa pc ndo mtihani
 
Naelewa hilo, kwani kitu gani halali ni rahisi boss? Ni juhudi na Investment. Sema kuwa Translator wa Kiswahili kuna less competition kuliko area nyingi kwa sababu watu wanaojua kiswahili mule ni wachache ukilinganisha na vitu vingine. So chances za ku bump na opportunity ni kubwa zaidi.

Hakuna kitu rahisi halali!
Mkuu umepata kazi ngapi za ku translate to kiswahili huko upwork/fiver/freelancer...?

Me nilikiwa nawaza nikipata muda ni jikite na mambo ya Database...!!
 
Ela za kununua bids, uwa wanatoa za bure zikiisha ukiwa wataka wanunua kama hutaki zitajiongeza baada ya masaa. Yes kazi za $5 zimekuwa nyingi na wanazigombea. Ndiyo maana nimejikita zaidi kwenye masuala mengine kma subtitling za movies zinazoonyeshwa Netflix
Unakuwa unapewa script ? Unaifanyiaje kazi hii mkuu???
 
Back
Top Bottom