DOKEZO Hali ni mbaya sana kwa walemavu tuliosoma, Si Serikali wala kampuni binafsi ambazo ziko tayari kutuajiri. Tunabaguliwa

DOKEZO Hali ni mbaya sana kwa walemavu tuliosoma, Si Serikali wala kampuni binafsi ambazo ziko tayari kutuajiri. Tunabaguliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Afadhari hii mada umeweka hapa.

Hii nchi ina mambo ya Ajabu sijawahi ona, yaan mtu ana ajiriwa hadi kwa kuangaliwa Sexual Orientation yake, huu si upumbavu kabisa.

Kazi haiihitaji sexual affairs, inahusu mambo mengine kabisa, lakini hapo utaangalizwa hadi nani una date nae, km si ulofa n nn?

Li nchi ndo maana haliendelei, kutwaa ubaguzi wa kipumbavu usio na tija, una muacha mtu mwenye vigezo na sifa stahiki kwa kazi husika, kisa mapungufu yake, na una mchukua mwingine hata hajui lolote kisa ana ukamilifu fulani, jamani inaumiza hatariii.

Tupaze sauti, kuondoa sintofahamu hii.
Sasahiv ukienda kweny maofis mengi utakuta wadada wazuri wenye mashepu Yao ndo wamejaa!! Lakn wenye kigezo Cha ueledi wachache!! Mtanisamehe naongea nilichokishuhudia
 
Pole sana mkuu.

Umejaribu kupitia ajira portal ?.
Huko private nina-uzoefu nako ni kugumu sana kwa watu wenye ulemavu kukupokea na sometime huwezi kuwalaumu, wale wanaangalia faida zaidi kuliko hali zetu. Na baadhi ya taasisi za serikali hawazingatii kabisa izo 3% na 50% ufaulu za walemavu kwenye ajira zao sijui kwanini.

Kuna group kubwa la whatsap la watu walemavu, nile namba PM wakuunge.
Kiukweli kaka magroup ni mengi lakn hakuna solution ya watu woote!! NtakupM angalau naweza nikapa sehem ya kuegemea
 
Walemavu wanakanuni zao kuwafavour upande wa mambo ya ajira. Mfano kila ajira ya serikali 3% ni nafasi za walemavu, pia kwenye written intervirew mlemavu akifikisha 50% aijilishi cutting point ni ngapi huyo ataenda atua inayofuatia.

Ajabu kuna baadhi ya taasisi za serikali hizo kanuni wao ni kama hawazijui kabisa. Walau ajira portal na wale Tamisemi zamani wanajitahidi sana.

Mfano mzuri kuna izi ajira za mwisho za TRA, sikuaona kabisa suala la 3% kwenye izo ajira zao. Pia kuna walemavu nawafahamu walifikisha 50% kwenye written ila hawakwenda oral kisa hawakufikisha cutting point, na hata walipopeleka malalamiko hawakutoboa.

Sasa kama serikali yenyewe inatufanyia ivyo unategemea nini huko private ?.
Ni kweli Hilo jambo
 
Mkuu,

Shukrani sana kwa kunitoa tongo tongo, ni kweli kama ni wajibu na sheria kupata hizo favors na ikafanyika vinginevyo basi ni ukiukwaji mkubwa sana wa haki, ukizingatia tunatambua namna ndugu zetu mnavyopata changamoto mpaka kufika hatua kubwa za kielimu kutokana na changamoto za miundombinu isiyo rafiki.
Na appreciate comment yako kiongozi
 
Asante mzee wetu kwa nasaha nzurii...nikiwa Kama shuhuda wa ajari barabarani mwaka Jana na kuvunjika mguu so kwa muda wa zaidi ya miezi 7 nimeishi Maisha ya ulemavu..

Nikaanza kutembea kwa kujifunza muda mwingine nilikua nawaonea wivu watu walio kua wanatembea sikujua Kama ntaweza kutembea Tena na kwa Sasa mwezi huu wa pili nafikisha mwaka mmoja..now naweza kutembea Tena

Shukrani sanaa mkuu.
Pole na hongera kuweza kutembea tena

Nimekuwa natembea na hiyo slogan kwamba yeyote aliye mzima wa viungo ni mlemavu mtarajiwa baada ya kuona marafiki zangu wawili ambao walikuwa wazima wa afya kupata ajali na kupoteza viungo vyao baadhi na kuwa Wategemezi sasa.

Kweli hujafa hujaumbika 🙌
 
Unadhani hata wasio walemavu hali zao zipo poa ? Mkuu ni pote tu na sio Afrika tu bali duniani nguvu kazi is no longer required; Ingawa kwa Tanzania yetu tungeweza kutokuwa na shida hii kutokana na kwamba tuna resources za kumwaga..; na sasa hivi nyie walemavu mnalalamika kesho tutakuwa na wazee ombaomba sio kwamba wanalalamika tu bali kila tukipiga tambo watakuwa wanatusimamisha na kutuomba omba

Bora hata wangetupa haki sawa na ambao hawana ulemavu, badala yake sisi hawatutaki sio kwasababu ya ukosefu wa ajira! Ni kwasababu ya kutotaka walemav
 
Hivi hakuna kiongozi yoyote mwajiriwa wa serikali ambaye ni mlemavu?Kama yupo,sasa yeye ndiyo inabidi apaze sauti kuwasaidia walemavu wangine.Sema yana mwisho Mkuu.
Yupo Keisha kule!! Lakn huwezi saidika
 
Ila kama sio mlemavu wa akili bado.una fursa ya kupata ajira na kuleta mabadiliko katika maisha Yako

Pole sana
Ajira hatupewi, si serikalini Wala private!! Nafuu wakati mwingne hata private Kuna watu wanamoyo kidogo, lakn huku sasa ni balaa
 
Pole na hongera kuweza kutembea tena

Nimekuwa natembea na hiyo slogan kwamba yeyote aliye mzima wa viungo ni mlemavu mtarajiwa baada ya kuona marafiki zangu wawili ambao walikuwa wazima wa afya kupata ajali na kupoteza viungo vyao baadhi na kuwa Wategemezi sasa.

Kweli hujafa hujaumbika 🙌
Ni kweli nili ishi ulemavu wa mpito niliona jinsi ILIVYO changamoto niliota sugu makwapani na kwenye viganja vya mikono yote miwili yalikua ni Maumivu Zaid na zaidi nawaheshimu Sana Sana walemavu.
 
Ni kweli nili ishi ulemavu wa mpito niliona jinsi ILIVYO changamoto niliota sugu makwapani na kwenye viganja vya mikono yote miwili yalikua ni Maumivu Zaid na zaidi nawaheshimu Sana Sana walemavu.
Pole sana Mkuu, lakini Mungu wetu ni mwema 🙏🙏🙏
 
Usijihisi mnyonge pambana na interview utabahatika tu siku moja.
 
Back
Top Bottom