DOKEZO Hali ni mbaya sana kwa walemavu tuliosoma, Si Serikali wala kampuni binafsi ambazo ziko tayari kutuajiri. Tunabaguliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Suala la ajira ni janga la kitaifa, ingawa ulemavu unaongeza ugumu. Nakushauri angalia pia namna unaweza kujiajiri kutokana na hali yako. Kama ni mlemavu wa miguu unaweza kufanya shughuli za mikono mfano uandishi, utengenezaji viatu, mihamala ya simu(yas mix, mpesa n.k). Kupata fursa ni mapambano ya survival of the fittest, hakuna atakaekuonea huruma.
Hua wakati mwingi nawaza ni kwa namna gani ntaweza kusaidia hata na wengine!! Siamini bado falsafa ya "survival for fittest" naamin kweny creation ya fittest ili a survive
 
Pole sana mkuu
Nadhani viongozi wataona hii taarifa walifanyie kazi
Pole sana Mungu awasaidie
Siyo kwa viongozi hawa sana sana wataleta kiroba cha unga na debe mbili za maharage mbele ya camera ndio imetoka hiyo, kinyume cha hilo ni vimikopo visivyo na tija.
 
Mtu kakuambia kasoma degree ya Usimamizi Wa Fedha. Ulemavu wa miguu unamzuia kutimiza majukumu yake? Mna mpango wa kumpa ofisi ya ghorofani kwaajili ya kumkomoa?

Ujue Mwafrika anaamini sana kwenye manguvu karibia kila sehemu. Wakati dunia inawabeba kila mwenye potential ili mradi kichwa kinafanya kazi kama kina Steve Hawking. Huku kuna Mwafrika, huanzi shule hadi mkono ushike sikio la upande wa pili, kuvunja matofali kwa kichwa, uwe na futi tano sijui ngapi upate kazi..

Yaani manguvu manguvu.
Kwenye kutoa ajira watu hawaangalii huruma hiyo ni risk kubwa sana.
 
Niende kwenye mada moja kwa moja!!.

Nimekuwa moja ya wahanga wa hili Tatizo kwa muda mrefu sana

Kati ya watu wanaosoma kwa mateso makubwa sana ni watu wenye ulemavu, kuanzia shule za msingi mpaka sekondari, hii inatokana na miundo mbinu mingi kuwa tofauti na Hali zetu watu wenye ulemavu.

Wakati mtu mwenye ulemavu anapambna akiamini kuwa yeye hawez kulima, kutembeza mitumba, Wala kufanya kazi ngumu za ujenzi akitegemea akili yake tu ya darasani angalau impe mwanga wa maisha.

Baada ya ajira huyu mtu mwenye ulemavu anaanza kuzunguka na baiskeli yake au magongo yake kweny interview mbalimbali, wakati mwingine hufanyika mikoani, au kwenye majengo yasiyo na lift.
Wengi wanaishia kukata tamaa sana.

Kuna sehemu niliwahi kataliwa kabisa kisa mimi ni mlemavu kwamba siwezi kufanya hio kazi kwasababu nitakuwa naenda sana hospitali, yaani trip kazini trip hospitali. Wanahisi labda sisi ni wagonjwa fulani hivi,

Inaumiza sana sana, naongea kwa niaba Yao sana.

Wengi walioajiriwa ni sababu za kisiasa, ili ionekane hawabaguliwi hasa kwenye sekta zinazohusiana na walemavu ndio huko wamejazwa!

Nina watu nawajua ni walemavu, wanapitia kipindi kigumu sana lakini wakiwa na elimu Yao kichwani! Yaani huu unyanyapaa huwezi ona kwa jicho la kawaida! Ni dhamira za watu.

Kitanda usicholalia huwezi jua kunguni wake!! We feel pain sana sana

Natimiza mwaka wa saba(7) tangu nimalize digrii yangu ya usimamizi wa fedha..

Serikali haitujali tena, zaidi ya kutulazimisha tukope pesa tuu.

Wadau wapo kimaslahi na kisiasa zaidi wapate attention wakati wanatoa misaada.

Hata vyama vya walemavu sasa hawana la kusema baada ya kulamba sukari

Sisi tukimbilie wapi zaidi yenu wadau wa hapa JF, tusaidieni kupaza sauti sisi walemavu tuliopambana kusoma kwa bidii, tunatamani kubeba tofali angalau tupate mkate wa kila siku lakini Hali zetu hazituruhusu.

Tuliamini katika elimu nayo imetusaliti, nchi imetutenga, tuna hari mbaya sana
Mkuu, angalau mabenk wanajari, nina rafiki zangu walemavu wa viungo wameajiriwa NMB, CRDB japo sijaona kiziwi hata hivyo hawa wamejazana kule kwenye ajira za ualimu.

Kingine ningeshauri pia muangalie mazingira na kazi za kuomba kuendana na hali zenu haya mambo ya usawa na huruma wakati mwingine hayafanyi kazi kila sehemu.
 
Tatizo lilianzia kwa wazazi. Ilibidi wajue mbele kunani hivyo wawape elimu ya ujasiriamali
 
Historia ni ndefu San!! Lakn kwasisi wakt mwingne badhi ya wazaz hasa baba... Wanakuwa Kama hawatuamini Kama tutakuja saidia familia kwahio! Sikuwahi kuwa karibu na mzee
 
Mkuu, angalau mabenk wanajari, nina rafiki zangu walemavu wa viungo wameajiriwa NMB, CRDB japo sijaona kiziwi hata hivyo hawa wamejazana kule kwenye ajira za ualimu.

Kingine ningeshauri pia muangalie mazingira na kazi za kuomba kuendana na hali zenu haya mambo ya usawa na huruma wakati mwingine hayafanyi kazi kila sehemu.
Hii jamii ya walemavu ni wachache sana!! Hakukuwa na haja ya kuwapa competition kubwa kweny kutafuta ajira!!! Ingefaa wakitoka chuo wapewe nafasi serikalini
 
Siyo kwa viongozi hawa sana sana wataleta kiroba cha unga na debe mbili za maharage mbele ya camera ndio imetoka hiyo, kinyume cha hilo ni vimikopo visivyo na tija.
Umejuaje kaka!! Yaani mi ni shuhuda wa Hilo!! Japo hata hicho kidog huwa tunashukuru
 
Huko tayari tumepita hakuna mweny jibu!! Wanaishia kuitwa kweny semina ili wapate posho za semina
Sasa hata walemavu pia mnasalitiana kwa kulambishwa sukari Basi hàkuna haja ya kulaumu wasio walemavu kuwabagua, acheni kwanza kubaguana ninyi kwa ninyi ndo muanze kuwalaumu wasio walemavu.
 
Niende kwenye mada moja kwa moja!!.

Nimekuwa moja ya wahanga wa hili Tatizo kwa muda mrefu sana

Kati ya watu wanaosoma kwa mateso makubwa sana ni watu wenye ulemavu, kuanzia shule za msingi mpaka sekondari, hii inatokana na miundo mbinu mingi kuwa tofauti na Hali zetu watu wenye ulemavu.

Wakati mtu mwenye ulemavu anapambna akiamini kuwa yeye hawez kulima, kutembeza mitumba, Wala kufanya kazi ngumu za ujenzi akitegemea akili yake tu ya darasani angalau impe mwanga wa maisha.

Baada ya ajira huyu mtu mwenye ulemavu anaanza kuzunguka na baiskeli yake au magongo yake kweny interview mbalimbali, wakati mwingine hufanyika mikoani, au kwenye majengo yasiyo na lift.
Wengi wanaishia kukata tamaa sana.

Kuna sehemu niliwahi kataliwa kabisa kisa mimi ni mlemavu kwamba siwezi kufanya hio kazi kwasababu nitakuwa naenda sana hospitali, yaani trip kazini trip hospitali. Wanahisi labda sisi ni wagonjwa fulani hivi,

Inaumiza sana sana, naongea kwa niaba Yao sana.

Wengi walioajiriwa ni sababu za kisiasa, ili ionekane hawabaguliwi hasa kwenye sekta zinazohusiana na walemavu ndio huko wamejazwa!

Nina watu nawajua ni walemavu, wanapitia kipindi kigumu sana lakini wakiwa na elimu Yao kichwani! Yaani huu unyanyapaa huwezi ona kwa jicho la kawaida! Ni dhamira za watu.

Kitanda usicholalia huwezi jua kunguni wake!! We feel pain sana sana

Natimiza mwaka wa saba(7) tangu nimalize digrii yangu ya usimamizi wa fedha..

Serikali haitujali tena, zaidi ya kutulazimisha tukope pesa tuu.

Wadau wapo kimaslahi na kisiasa zaidi wapate attention wakati wanatoa misaada.

Hata vyama vya walemavu sasa hawana la kusema baada ya kulamba sukari

Sisi tukimbilie wapi zaidi yenu wadau wa hapa JF, tusaidieni kupaza sauti sisi walemavu tuliopambana kusoma kwa bidii, tunatamani kubeba tofali angalau tupate mkate wa kila siku lakini Hali zetu hazituruhusu.

Tuliamini katika elimu nayo imetusaliti, nchi imetutenga, tuna hari mbaya sana
Hakuna watu wakorofi kazini kama walemavu.

Nimekoma.
 
Pole sana..
Lakini je hata ungekuwa wewe ,ungeweza kumuacha mtu ambaye si mlemavu ukaajiri mlemavu?
Mkuu, kwani huko makazini wanakwenda kupigana mieleka?

Taaluma nyingi walizosoma hawa ndugu zetu wala sio za kutumia akili na nguvu.
 
Pole Mkuu Mungu awasaidie!
Sasa hivi kwa sababu ya uchache wa ajira,kilichobaki ni Strugle of mass for existence! Hii ina result for Survival for the fittest!
 
Back
Top Bottom