Mwenye macho haambiwi tazama. Hali si shwari. Hali ni mbaya. Kampeni haziendi. Na wakizifosi ziendelee basi itabidi wavunje bank maana recurring costs zimekuwa kubwa kuliko ilivyotegemewa.
Wajumbe hawakuwa wapumbavu kuwakata vichwa hao mlowachagulia. Mkadhani labda watamwogopa Mwenyekiti lakini ndio kwanza wanamchomolea betri waziwazi. Na akiwafosi sana wanaenda kumkata hata Mwenyekiti mwenyewe.
Mama Maria nahisi kashukiwa na mume wake Mwl. Nyerere aje awaambie kwamba muache kufosi watu waje kuongeza idadi kwenye mikutano yenu. Mama Maria anaumwa hana muda na kampeni kajuaje mnasafirisha watu kuja kujaza viwanja, ni wazi atakuwa katumwa na malaika wa bwana kuja kuwagutua toka usingizini.
Mwanza leo mmesitisha masomo ili tuu muonekane mmejaza uwanja. Huku na kule Warioba naye kawapiga chembe kidevu. CCM amkeniiiii.
Ni muda muafaka wa kusitisha kampeni zenu mkajipange upyaa. Tena mtafute mzungumzaji kwa niaba ya mgombea wenu sababu ndipo penye ufa mkubwaaa.
Wakati ni ukuta huwezi kupambana nao.