Hali ni tete katika Shule ya Sekondari Nkuhungu Mkoni Dodoma, Walimu malalamiko, Wanafunzi vilio.
Your browser is not able to display this video.
Shule ya Sekondari Nkuhungu Mkoani Dodoma inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zimelalamikiwa na Wanafunzi na Walimu shuleni hapo.
Shule hiyo ya binafsi ipo Kilometa 10 kutoka katikati ya Mji wa Dodoma, inasemekana awali ilikuwa chini ya Kanisa la RC baadaye ikauzwa kwa mtu binafsi.
Sehemu ya changamoto ambazo zimelalamikiwa ni maji machafu kutokana na kuharibika kwa Kisima.
Madirisha ya kwenye vyumba wanavyolala Wanafunzi mengi yameharibika na wanafunzi wanalazimika kuziba kwa taulo zao, hali ambayo si salama kwao.
Walimu wanadai malimbikizo ya mishahara hali ambayo inasababisha wengi wao kuwa na muda mfupi wa kufundisha huku muda mwingi wakiutumia kwenda kufanya shughuli nyingine nje ya ajira hiyo kwa ajili ya kujiingizia kipato.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Sospeter Mwita kwanza alianza kumlalamikia Mwandishi kwa kitendo cha kwenza kuzungumza na Wanafunzi na Walimu bila kuomba ruhusa kisha akasema:
“Mtu akisema hatuna Walimu nasikia uchungu kabisa, Walimu wanafanya kazi sana, hivi kipindi chote hicho kuwe hakuna Walimu wazazi wawaache Wanafunzi shuleni, taarifa mlizopata mmepata kutoka Wanaharakati.”
Naye, Abdulhabib Jafari Mwanyemba ambaye ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Dodoma amesema “Tunaiomba Serikali itazame shule kama hizi, mambo ni mengi, umeona watoto wamesema vitu ambavyo vinaweza kumfanya mtu akapoteza utulivu wa kusoma na hata Walimu ufanisi wao unaweza kuwa chini.”
Hii ni habari nzuri sana kwa nchi. Inatakiwa ''changamoto'' (kama watanzania tulivyozoea kuita uzembe) kama hizi ziwe nyingi ili wananchi waamke kwenye ujinga wa kuita serikali mbovu ''serikali yetu pendwa''.
🤣🤣Bongo nyoso. Bango linasema kila kitu. Waalim nao ni kama hilo bango. Wanaomba eti ''serikali yao pendwa na sikivu'' iwasaidie kukabiliana na ''changamoto'' zao. Ni mfululizo ule ule wa mtu anazika ndugu aliyeuwa na polisi kwa amri ya serikali huku anaomba hiyo hiyo serikali yake pendwa na sikivu isikie kilio chake!1
Hii shule hata kupanda miti kuboresha mazingira ya shule imeshindikana?? Zamani wanafunzi tulikuwa tunakabidhiwa mti kuutunza mpaka unamaliza shule.... Utamaduni huu ulikoma lini??