By MAKOSHNELI 11:20 Today
Wakuu,
leo ntwara tangu asubuhi kila
huduma imefungwa watu wapo
kimakundi makundi wanasikiliza
bunge hasa bajeti ya wizara ya
nishati na madini,ni magari ya ffu
tu ndio yapo barabarani nayo
hupata wakati mgumu kupita
kwasababu ya mawe na magogo
yaliyowekwa na vijana,baadhi ya
watu kadhaa wamechukuliwa na
askari eti kwakuwa walipita jirani
na gari yao,askari wengi waliokuja
si wa hapa ntwara wengi wametoka
Masasi na Lindi.
Kauli mbiu ya huku kwa sasa -
"gesi haitoki hata kwa bomba la
peni"