Tetesi: Hali si shwari CHADEMA

Tetesi: Hali si shwari CHADEMA

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
1,984
Reaction score
1,405
Chadema sasa inapita ktk mazingira magumu kisiasa kuliko kawaida, taarifa kutoka ndani ya chama icho inaeleza kuwa chama icho iko ktk mgawanyiko kutokana na aina ya siasa wanazofanya. Ukitazama chama hicho kwa jicho la nje unaweza kudhani kuko shwari lkn kihulisia chadema ina ombwe la uongozi sasa. Ombwe ilo linatokana na cdm kukosa msemaji halali wa chama na msuguano wa chini kwa chini ndani ya uongozi na nje ya uongozi.

Kawaida taasisi yoyote lazima kuwa na msemaji mkuu wa chama anayeongea kwa niaba ya taasisi lkn kwa chadema jambo sasa halipo kila kundi linamekuwa na msemaji wake, mfano mh Edward Lowassa akitoa tamko linakuwa na chama, mh Freeman Mbowe akitoa tamko linakuwa tamko la chama, Dr Vicent akitoa tamko linakuwa la chama, Mh Tundu Lissu akitoa tamko linakuwa la chama, Mh Godbles Lema akitoa tamko linakuwa la chama na Tumaini Makene wkt mwingine unajiuliza hiki chama hakina utaratibu kila mtu msemaji hakuna tofauti kati ya wasemaji rasmi wa chama na matamko binafsi ya viongozi.

Kutokana na hili ilibidi nipitie watu wangu ndani Ufipa na Alpha kujua kulikoni ndipo nilipopewa taarifa kuwa ndani ya chama hicho sasa kila kundi linapambana na kundi lingine kujiuza kwa wanachama na wananchi ili 2020 kila kundi ijijengee umaarufu. Chama hicho sasa ina makundi mawili makubwa Cdm Mafisadi inayoungwa mkono na Lowassa na wahamiaji wake, Mbowe, Mashinji na Salum Mwalimu na kundi lingine ambalo sasa limepewa jina la siri kuwa Cdm watukutu linaongozwa na Tundu Lissu, Peter Msigwa, John Mnyika, Fredrick Sumaye na wafuasi wengi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Cdm Dr Silaa.

Tutaendelea next
 
CHADEMA ngangari. Mtaandika sana nyuzi zenu za kusadikika na ushahidi wa kusadikika. Eti, "taarifa kutoka ndani ya chama hicho" Hahahahaha lol! Taarifa hiyo imetolewa na nani!? Au hana jina? Imetolewa lini?
 
Wewe inakuhusu nini kufuatilia mambo ya CHADEMA!? Kama ina msemaji mmoja au elfu moja it is none it business! Mind your own business. Ya Ngoswe mwachie Ngoswe hayakuhusu!
Mbona unakuwa mkali imekugusa nini? Siasa in
Kusema ukweli mkuu siasa siyo uhuni km mnazofanya uko ukuta
 
Siasa ni kusema kweli eeh! Na kusema kweli ni kutafuta mambo ya ndani ya CHADEMA ambayo huna ushahidi wowote na hayana athari zozote kwa Tanzania na Watanzania. Kama unajua ukweli hebu andika kuhusu ufisadi wa Lugumi ambao wahuni ndani ya Serikali ya kifisadi na polisiccm wamechota 37 billion na uchwara hata kuitaja Lugumi anahofia. Hebu andika kuhusu ufisadi wa Salma na Ridhwan Kikwete wa kukwapua UDA mchana kweupe! Hebu andika kuhusu ufisadi wa Magufuli AKA dikteta uchwara kwenda kununua boti lililooza la mwaka 1978 kwa shilingi bilioni 8, andika kuhusu Escrow na wale wote waopokea rushwa Bungeni mpaka Ikulu za mabilioni. Haya yote yana athari kwa Tanzania na Watanzania badala ya kwenda kutafuta uzushi usiokuwa na kichwa wala miguu na ambao hauna athari yoyote kwa Taifa. CHADEMA ikiamua kuwa na msemaji mmoja au elfu moja wewe haikuhusu chochote kutaka kubadili maamuzi ya CHADEMA.

Mbona unakuwa mkali imekugusa nini? Siasa in
Kusema ukweli mkuu siasa siyo uhuni km mnazofanya uko ukutani
 
Tusubr hapo hapo tutakupitia apo tareh 1sept, sawa? Usitoke kabsa
 
Ungekuwa na akili usingekuja kuandika huu upuuzi wako humu. Hebu tuambie athari ya CHADEMA kama ina msemaji mmoja au 1,000 kwa Tanzania na Watanzania. Je, umeshawahi kusikia yeyote yule ndani ya CHADEMA akilalamikia wingi wa wasemaji wa CHADEMA? Ni kwanini unadhani hujasikia malalamiko hayo? Hiyo taarifa ya kutoka ndani ya CHADEMA imetolewa na nani? Juzi tu mmeandika barua na kujifanya inatoka Tume ya maadili kumbe ni uzushi wa hali ya juu, leo tena na wewe unakuja na uzushi wako wa "taarifa kutoka ndani ya chama hicho" Jitathmini kwa kina badala ya kuendelea kukurupuka na kuonyesha ujuha wako hadharani.

Hivi maana ya kusoma? Km kweli wewe una elimu basi wewe ni hasara kwa taifa na familia yako. MTU aliyendesha anaweza kutoa msneno hayo siamini labda uliingia chuo kimakosa ndiyo kundi la wale waliyotajwa kwenye utafiti wa Jambo Leo. Bora mtu asisome kuliko kutoa wasomi dizaini yako
 
Hivi maana ya kusoma? Km kweli wewe una elimu basi wewe ni hasara kwa taifa na familia yako. MTU aliyendesha anaweza kutoa msneno hayo siamini labda uliingia chuo kimakosa ndiyo kundi la wale waliyotajwa kwenye utafiti wa Jambo Leo. Bora mtu asisome kuliko kutoa wasomi dizaini yako

Muache BAK bana. Kala yamini na Mbowe hivyo sio akili yake inayomsukuma bali ya Mbowe (with all due respect BAK, we ni mzalendo). Hivyo ndugu Frey muache BAK hivyo hivyo kama ulivyomkuta.
 
Sasa huo ni uzushi FA. Nakuheshimu sana lakini kuandika mambo ambayo huwezi kuyathibitisha si sawa hata kidogo. Pamoja na kuwa mtetezi wa CHADEMA kwa muda mrefu humu kama mwanachama hai wa CHADEMA sijawahi kula yamini na yoyote yule ndani ya CHADEMA. Mie si mkurupukaji kusema niko CHADEMA kwa sababu ya mtu huyu au yule. Nakuomba uache kuandika kitu chochote kuhusu mimi ambacho huwezi kukithibitisha hata chembe.

Muache BAK bana. Kala yamini na Mbowe hivyo sio akili yake inayomsukuma bali ya Mbowe (with all due respect BAK, we ni mzalendo). Hivyo ndugu Frey muache BAK hivyo hivyo kama ulivyomkuta.
 
Sasa huo ni uzushi FA. Nakuheshimu sana lakini kuandika mambo ambayo huwezi kuyathibitisha si sawa hata kidogo. Pamoja na kuwa mtetezi wa CHADEMA kwa muda mrefu humu kama mwanachama hai wa CHADEMA sijawahi kula yamini na yoyote yule ndani ya CHADEMA. Mie si mkurupukaji kusema niko CHADEMA kwa sababu ya mtu huyu au yule. Nakuomba uache kuandika kitu chochote kuhusu mimi ambacho huwezi kukithibitisha hata chembe.

Nimegusa penyewe. Nakuheshimu pia hivyo nawe uache kuandika usiyokua na uhakika nayo kuhusu Magufuli. Mnadhani ana moyo wa chuma ehh? Kejeli, dharau, kama vile aliingia madarakani kwa mapinduzi. Test joto la kejeli.
 
Magufuli fisadi ushahidi upo, kahonga nyumba alizokwapua ushahidi upo. Dikteta uchwara ushahidi upo. Muongo ushahidi upo mpaka kwenye ripoti ya CAG. Hebu weka kile nilichoandika mimi humu kuhusu Magufuli ambacho si cha kweli.

Nimegusa penyewe. Nakuheshimu pia hivyo nawe uache kuandika usiyokua na uhakika nayo kuhusu Magufuli. Mnadhani ana moyi wa chuma ehh? Kejeli, dharau, kama vile aliingia madarakani kwa mapinduzi. Test joto la kejeli.
 
Magufuli fisadi ushahidi upo, kahonga nyumba alizokwapua ushahidi upo. Dikteta uchwara ushahidi upo. Muongo ushahidi upo mpaka kwenye ripoti ya CAG. Hebu weka kile nilichoandika mimi humu kuhusu Magufuli ambacho si cha kweli.

Khaa! Weka facts and figures za ufisadi, udikteta na uongo wa Magufuli, then nitaleta ushahidi wa uongo wako dhidi yake ambao ni kama kumsukuma mlevi as upo humu humu jamvini na nimeshauvuta.
 
Tatizo lako unadhani mimi natunga ninayoandika humu kuhusu Magufuli dikteta uchwara. Haya yamo katika ripoti za Serikali zimeandikwa na watu walioaminiwa na kupewa wadhifa mkubwa Serikalini. Kama haya yote yaliyomo katika ripoti za Serikali kuhusu ufisadi na uongo wa Magufuli Dikteta uchwara ni ya uongo basi si uongo wa BAK bali ni uongo wa waliomo Serikalini ambao waliandika ripoti hizo.

Ufisadi wa Magufuli:


ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Uongo Wa Magufuli:

Dar es Salaam. Machungu ya Watanzania yakiwa hayajapoa kutokana na kashfa ya Sh306 bilioni kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ufisadi mwingine wa zaidi ya Sh252 bilioni umeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ndani ya wizara ya ujenzi.

Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.

Kutokana na ufisadi huo, habari zilizolifikia Mwananchi zinasema CAG amependekeza hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika wa wizara ya ujenzi na wakala wa barabara ili kuleta imani na uwazi katika bajeti kwa jamii na wahisani.

“Wizara (ya ujenzi) ililidanganya Bunge kuwa kuna ujenzi wa barabara hizo wakati wakijua kwamba walikusudia kulipa madeni ya wakandarasi na washauri wa ujenzi wa barabara...mpango mkakati wa wakala wa barabara wa mwaka wa fedha 2011/12 pamoja na manunuzi ulioidhinishwa havikuonyesha utekelezaji wa mradi huo,” chanzo cha habari kilikariri ripoti ya CAG.

Matumizi hayo yasiyo sahihi yaliibuliwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Novemba 22, 2013 baada ya kutilia shaka kiasi hicho cha fedha na ofisi ya CAG kuagizwa kufanya ukaguzi.

Katika kikao hicho ambacho wizara ya ujenzi iliwakilishwa na Katibu Mkuu wake wa wakati huo, Balozi Herbert Mrango alihojiwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa CAG mwaka 2011/12.

Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo Sh348.1 bilioni zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililokuwa limetajwa kuwa ni la mradi maalumu hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.

“Ni vizuri leo (ilikuwa Novemba 22 mwaka 2013) uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975 bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto.

Tatizo lako unadhani mimi natunga ninayoandika humu kuhusu Magufuli dikteta uchwara. Haya yamo katoka ripoti za Serikali zimeandikwa na watu walioaminiwa na kupewa wadhifa mkubwa Serikalini.

Kumdharau mkewe: Sikiliza hii link kuanzia dakika tatu kuendelea na mengineyo mengi hadi mkewe kugoma kumfanyia kampeni.

Mama Janeth Magufuli agoma kukampeni, acharuka




Khaa! Weka facts and figures za ufisadi, udikteta na uongo wa Magufuli, then nitaleta ushahidi wa uongo wako dhidi yake ambao ni kama kumsukuma mlevi as upo humu humu jamvini na nimeshauvuta.
 
Chadema ipo moja haijagawanyika.
Yote ni chadema mafisadi tundu lisu,msigwa walipata mgao wao kutoka kwa mbowe baada ya kuuza chama kwa fisadi lowasa bilioni 10.
Wote sasa ni watetezi wa mafisadi.
 
Back
Top Bottom