Mkuu
JokaKuu
Ingalikuwa vema ukiweka clip nzima ya Othman Masoud kwasababu kuna mengi
Sishangai mtifuano kwasababu, OMO kama wanavyomwita ni mpotoshaji hasa linapokuja suala la muungano.
Angalia interview ya Clouds 360 ina mengi ya kapotosha kwa makusudi au kutojua
Watangazaji 3 wa Clouds hawakuweza kuuliza, kusahihisha au kutaka ufafanuzi kutoka kwa Othman alipoongea . Walimwacha ahutubie badala ya mahojiano. Watangazaji walisikitisha
clip ni kwa hisani ya Clouds media
Dakika 48
Masoud Othmana anasema ''Tanganyika na Zanzibar ziliungana zikiwa sovereign states, baada ya muungano ikawa shared sovereignity. Moja ya matakwa ya shared sovereignty ni kuwa na Policy na kwamba sheria zinatungwa na upande mmoja na baraza la mawaziri la JPM ,Zanzibar haikuwakilishwa''
Hoja: Hoja ya VP Masoud si ya kweli. Katika shared sovereignty Tanganyika impoteza Zanzibar imebaki nayo kupitia SMZ inayoamua mambo yao.
Kuhusu sera kutungwa kwa upande mmoja nalo si kweli.
Zanzibar ina Wabunge na Wabunge kutoka BLW wanaoiwakilisha katika Bunge la JMT.
Kwamba maamuzi yanafanywa kwa kura ni kweli kwasababu Wazanzibar ndani ya JMT wanaamua hata mambo yasiyo ya muungano kwa kura ile ile anayoikataa Masoud Othman, mbona halisemi hilo?
Kamtumhumu JPM kwamba baraza lake la Mawaziri halikuwa na uwakilishi kutoka Zanzibar.
VP othman alikuwa AG anafahamu Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa Cabinet kwa kuapishwa
Kwamba VP alikuwa mjumbe wa Cabinet. Hivi hawa si viongozi wa juu wa Zanzibar, VP alitaka uwakilishi gani?
Lakini pia alikuwepo Waziri Mbarawa akisimamia wizara isiyo ya muungano, hilo anasemaje?
Dakika 53
VP OMO anasema ''resources za muungano zitawanywe ili Zanzibar ipate biashara na ajira.
Akatoa mfano Elimu ya juu ambako Zanzibar hakuna chuo kikuu''
Hoja: Haiwezekani resources za Tanganyika ziwekwe Zanzibar kwasababu mambo makuu ya muungano ni machache sana. VP hakusema gharama za resources hizo anazotaka ziwekezwe Zanzibar zinalipwaje na Zanzibar. Kwasasa Zanzibar haina mchango wowote kwanini resource za muungano zipelekwe huko.
Pili, Masoud Othman aelewe suala la elimu ya juu si la muungano. Ni suala lililoongezwa na akina Marehemu Sitta katika kusiadia Zanzibar hivyo kutojengwa chuo huko ni sawa kikijengwa ni fadhila.
Zanzibar wana wizara ya elimu ya juu sasa anataka ya muungano ifanye nini ? Zanzibar inachangia nini?
Dakika 51 anasema Rais wa JMT anachaguliwa na Tanganyika kutoka na idadi ndogo ya wapiga kura Zanzibar.
Makamu wa Rais othman akatolea mfano Marekani ambako California ina watu milioni 40 na Maine milioni 1.6 na Wyoming milioni 1 akisema mfumo huo unahkikisha hata state ndogo zinapata kauli kwa kutumia kile alichokiita ''Collegiate''
Hoja: Hakuna kitu kinachoitwa ''collegiate'' katika mfumo wa uchaguzi wa Marekani bali electoral college.
States zimepewa idadi ya Wajumbe watakaochaguliwa kwenda kumchagua Rais.
Rais anaweza kuchaguliwa kwa electoral college votes (270) za state chache
Hivyo kuna majimbo yenye wajumbe wanaoweza kufikisha 270.
Mfano California 55, New York 29, Texas 38, Florida 29, Pen state 20, Michigan 16, Georgia 16, N.Carolina 15, Maryland 10, Tenn 11, Illnoi 20, virginia 13, S.Carolina 9. State 12 zinaweza kumchagua Rais wa Marekani kwa kura 270 zinazohitajika.
Mfumo huo unawafanya wagombea wasipoteze muda na pesa za kampeni huko Montana wajumbe 3, Wyoming 3, au Vermont 3. kwa mantiki hiyo VP alipotosha au hakujua mfumo unafanyaje kazi
Hata Tanzania bado kuna suala la mikoa. Mfano mikoa ya kanda ya ziwa inaweza kumchagua Rais
Tukifuata mfumo wa Marekani bado Zanzibar itakuwa na viti vichache kwasababu katika constituents za Tanzania Zanzibar ni ndogo sana Wabunge wake wakichaguliwa na watu 2,500 lakini wanakura sawa pale Dodoma. Hivi Makamu wa Rais halioni hili kweli.!!!
Wamarekani sasa hivi wanataka popular vote kwa kujua mfumo wa electoral college si mzuri. Hillary Clinton alishinda popular vote kwa kura milioni 3 lakini Trump alimshinda kwa electoral college na kuwa Rais
Pengine alichokusudia kusema ni kwamba states zimepewa Maseneta 2 bila kujali ukubwa ili maamuzi yazingatie hata zile ndogo. Kinyume cha hivyo OMO alipotosha sana
Bank kuu:
VP othman anasema Karume aliona tatizo hakukubali kuingia BoT hadi Salimini. Kwamba Zanzibar ilikuwa na PBZ baada ya kuvunjika EAC currency board
Hoja: Hapa VP anatueleza kwamba yale madai ya Zanzibar kuingiza pesa BoT yanayowapa 4.5% ya pato la Tanganyika ni uongo na kwamba pesa hizo hawakupaswa kupewa bali ni hisani.
Lakini pia VP othman hakueleza nini kilimfanya Salimin akaingiza nchi BoT? Hakueleza je ZPB ambayo ipo hadi leo inamilikiwa na nani?
Dakika 23
OMO anasema Zanzibar ingesaidia muungano kutokana na historia yake na kwamba kuna KM 200 za bahari zenye mafuta na gesi katika vitalu 9, 10.
Hoja Historia ya Zanzibar ni ya biashara ya pembe za ndovu na utumwa, haina manufaa kwa Tanzania leo hii. Pili, mafuta na gesi yameondolewa na Zanzibar katika mambo ya muungano kupitia katiba ya 2010.
Ingawa Zanzibar inafadika na mapato ya gesi na madini yenyewe haitaki kuwa mshiriki.
Makamu wa Rais anapotosha sana
Dakika 24
OMO anasema Singapore ilikuwa katika muungano na Malaysia nailipojitoa uchumi wake ni mkubwa kuliko wa Tanzania na inaweza kufadhali bajeti
Hoja: VP Masouda anawaambia Wazanzibar kuwa wakitoka nje ya muungano watakuwa matajiri kama Malaysia. Hilo halina tatizo kwasababu ni mtazamo wake, anachotakiwa kufanya ni kuendelea kuchochoea kuni muungano uvunjike ili Zanzibar iwe kama Malysia
Katika video hii anazungumzia Zanzibar kunyimwa fursa ya kukopa akitolea mfano wa milioni 200 kutoka China
Anasema Tanganyika ipo hoi na Zanzibar ikitaka kupita Tanganyika inaweka vikwazo
Hoja: Mataifa yanakopesha kwa kuangalia uwezo wa nchi kulipa. China walisita kukukopesha wakijua kuwa mdhamini lazima awe chumi kubwa. Hata hivyo makamu wa Rais aelewe Zanzibar iliruhusiwa kukopa na hilo ni jambo jema kwani litapunguza mzigo kwa Tanganyika. Anachotakiwa ni kuendelea kusisitiza tu waende kukopa bila kutumia jina la JMT, walipe wenyewe na watafute wadhamini wenyewe!