Hali si Shwari Ndani ya Azam FC, Wachezaji Hawamtaki Kocha Dabo

Hali si Shwari Ndani ya Azam FC, Wachezaji Hawamtaki Kocha Dabo

Mula ugali sukari. Anaendeleza upuuzi huko. Kazi wanayo wauza asikilim.
 
Azamu wamepata dawa yao Dabo.

Niliisoma katika gazeti la Mwanaspoti kuwa, kocha aliwaambia viongozi kwamba, wachezaji hawajitumi na wamekuwa wakidekezwa. Wachezaji walikuwa wanapewa bonasi kiholela holela. Dabo kaweka masharti ya kupata bonasi tofauti na awali.

Dabo kapewa rungu kama vile kule Ulaya ambapo kocha ni Meneja. Dabo kapewa rungu la kuwadhibiti wachezaji wazembe na wakizingua anawakata dirisha dogo la usajili.

Aliishanza na Bajana kuvuliwa ukapteni.

Ila kama mimi ndio ningekuwa mchezaji wa Azam, ningekuwa najituma kwelikweli mama si nalipwa na kazi yangu ni mpira mana sidhani kama kocha ananipa mazoezi ya kunikomoa bali kuniimarisha.

Tazama Feisal tangu awafunge Tabora UTd wakiwa pungufu, hajafunga tena!
 
Alifunga dhidi ya coastal union na ametotoa assist mbili mechi ya juzi

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
🤔🤔
WACHEZAJI WA AZAM FC HAWAMTAKI KOCHA DABO

Hatimaye Jinamizi la Kumkataa la Makocha kukataliwa na wachezaji wa Azam limeibuka tena na sasa ni kwa kocha Dabo.

Habari za Uhakika ni kwamba safari hii ni zamu ya Yousouph Dabo, Taarifa zinasema kuwa Mkasa wa Dabo ulianza siku ya mazoezi kwanza baada ya mechi ya Yanga, Baada ya kichapo, Dabo aliwakosoa wachezaji wake mazoeziniakiwalaaumu kwa kucheza chini ya kiwango na hawakufuata maelekezo yake.

Akaenda mbali akawaambia wachezaji wasijione wako salama, atamuondoa mchezaji yoyote ambaye hatafuta malekezo yake kwenye disrisha dogo la usajili.

Chanzo chetu kinasema kauli hii iliwakera sana wachezaji, na kuanzia hapo walikubaliana kwamba wafanye wanavyoweza kufanya ili kocha huyo afukuzwe.

Chanzo chetu kinaendelea kutujulisha kwamba kabla ya mchezo wao na Namungo wakati wachezaji wakipasha moto misuli Dabo aliwaambia wachezaji wake kwamba watapoteza mchezo kwasababu hawakuonyesha kama wako tayari kwa mchezo huo.

Na kamaambavyo kila mtu aliona ndivyo hali ilivyokuwa, Azam ililala kwa kipigo cha goli 3-1 huku timu ikicheza kwa ari ya chini sana.

Na kwa taarifa za ndani ni kwamba wachezaji wamepanga kundelea na kumuhujumu Dabo kwenye michezo ijayo hadi afukuzwe, Ikumbukwe Azam leo anacheza na Mashujaa kigoma

Wachezaji wa Azam wanalalamika kwamba Kocha Dobo ni Mkali sana na hataki kusikia ushauri wa yoyote ndani ya timu, Wacheaji wa Azam wamekuwa na Malalamiko kwa kocha huyo muda mrefu sasa.

Hivi baada ya Azam kutolewa kwenye Mashindano ya kimataifa ya Shirikishao CAF, Mchambuzi mmoja wa mmoja wa wawachezaji wa Azam aliandika juu ya hali isivyoshwari kwnye chumba cha kuvalia wachezaji, inaonekana mchambuzi huyo alijulishwa na mchezaji wake mkasa huo.

Hata hivyo taarifa zinatanabaisha kwamba pamoja na msuguano huo wamiliki wa Azam FC wamesema wamechoka kufukuza makocha kila mwaka huku mambo yakishindwa kubadilika, safari hii wameamua kuziba masiko juu ya malalamiko ya wachezaji kama itabidi kufukuzwa basi wafukuzwe wachezaji lakini sio kocha.

Source, vyanzo mbalimbali, Mwanaspoti, Mitandao ya kijamii
 
Back
Top Bottom