Katibu Mkuu wa CCM Ndg Bashiru Ally Kakurwa amekemea vikali tabia za baadhi ya wanachama wa CCM wanaopanga kukisaliti Chama katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu kwa maslahi yao binafsi. Ameahidi kuwachukulia hatua kali watakaobainika kusaliti Chama ikiwemo kuwafukuza Uanachama.
"Wanaohama CCM wakidhani wananguvu, wakitoka wanageuka kama vichaa, wafuatilieni wote waliohama CCM, hakuna mwanaCCM maarufu kuliko CCM, ukijiona maarufu ujue umeazimwa umaarufu na CCM , siku Chama kikikutupa ama ukikitupa umaarufu unakoma. Wapo watakaookota makopo nawahakikishia" Bashiru Ally.
Maoni ya Kada wa CCM.
"Wanaohama CCM wakidhani wananguvu, wakitoka wanageuka kama vichaa, wafuatilieni wote waliohama CCM, hakuna mwanaCCM maarufu kuliko CCM, ukijiona maarufu ujue umeazimwa umaarufu na CCM , siku Chama kikikutupa ama ukikitupa umaarufu unakoma. Wapo watakaookota makopo nawahakikishia" Bashiru Ally.
Wakuu, Katibu Mkuu wa Ccm ametishia kuwafukuza wanaccm ambao wamepanga kumpa kura tundu lisu na kufikia mahali Ya kusema kuwa, watafukuzwa na watataifishwa Mali zao.
Unajua watu wanafanya mzaha na siasa za kutisha na kutumia manguvu pasipo ueredi na mwisho kutatokea anguko kubwa lisilotegemewa, siasa inataka akiri sio nguvu, Katibu badala Ya kutumia maneno Ya busara anatishia watu kuwa atawafukuza huku akijua kuwa kupiga kura ni Siri ya mtu mmoja, hupaswi kutisha watu kisa watapiga kura Kwa mtu mwingne huku ukijua kuwa kura ni Siri, Katibu alipaswa kutafuta sababu Kuu Ya wanaccm kupanga kupiga kura upinxani
Nimeshukuru Sana Ccm kugundua kuwa watu wamepanga kupiga kura Kwa upinzani nikiwemo Mimi Mwana Ccm Kada na kuna watu nawajua zaid ya Mia watapiga kura upinzani, Katibu ameshindwa kutambua kuwa kuweka haya hadharani ameshtua wengne waliokuwa wakinyanyaswa na Mwenyekiti kujiunga kwenye huo msafara
Naomba kumuuliza Katibu kuwa Mwenyekiti Alikuwa anachukua wapinzani anawapa vyeo anatuacha sisi miaka Yote, anawachukua anawapa nafasi za kugombea ubunge huku sisi akikataza katakata hata kuwapinga Leo hiii anatutisha? Haingiii akirini Mimi na watu Wangu tulihangaishwa na upinzani Mwaka 2015 hadi tukafanikiwa kumweeka madarakani halafau akatudharau kusema kuwa yeye ni Ccm Mpya akatutenga Halafu tuingie kwenye sanduku la kura tumpigie haiwezekani, tutapiga kura Kwa wingi Sana Kwa upinzani liwalo liwe hata atutishie afanye anachofanya sisi tutaonesha hasira zetu kwenye sanduku