Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

Mwenyekiti amevuruga sana mambo hakuna idara iliosalama,wakulima,wafanyakazi,wafanyabiashara,wahitimu wa vyuo wote malalamiko.Ndani ya chama nako matatizo matupu.

Katika kipindi ukabila umeshika kasi basi awamu ya tano ni kufuru,huku masanja kadogosa kule ngosha basi tu ilimradi shida tupu.
Eti hospitali kubwa ya kanda kujengwa Chato labda ijengwe kabla ya tar 28.

Huko mabarabarani kila mahali vizuizi maderava ambao walikua wakikuta kamzigo kadogo kanawapa chochote kitu wameambulia za uso kwenye vizuizi vya TRA.Hakuna dereva wa lorry atapigia kura kijani subirini muone haya manyanyaso mwisho tar 28
 
Bashiru anachekesha kweli, hivi anaona ccm ni bonge la chama, eti watamfukuza chama msaliti! Anyway labda kwakuwa wanaccm wengi ni wahalifu na kinga yao ni kuwa ndani ya ccm, hivyo hicho kitisho cha kufukuzwa chama kina maana.
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Bashiru Ally Kakurwa amekemea vikali tabia za baadhi ya wanachama wa CCM wanaopanga kukisaliti Chama katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu kwa maslahi yao binafsi. Ameahidi kuwachukulia hatua kali watakaobainika kusaliti Chama ikiwemo kuwafukuza Uanachama.

Mzee wa jalalani
 
Viongozi ndio wamewasaliti wanachama,haiwezekani tunachagua ambao sisi tunaona wanatufaa kutuongoza afu mnakata majina bila sababu za msingi na hazipo wazi. kwa maslahi yenu.yaaani ukiweza kuwainga viongozi wa chama WILAYA na mkoa wanakupa Alama za juu mnakata tuliwachagua kwanyw Kura za maoni.
Ni Bora mgebadilisha utaratibu wagombea wachukue fomu na kurudisha Kisha mkae na kurudisha mnaemtaka kuliko kutusumbua mnatupandisha malor uja kwenye uchaguzi wa chama,i kumbe kuna wapendwa wenu tayari.
 
Bashiru kwa nini anaendeleza makosa hayo hayo kila siku yaliyowafikisha hapo? Ubabe hauwezi kuendesha chama (hata nyumba yake tu itaparaganyika kama anaiendesha hivi). Hawa watu wakoje? Ndio wanaomshauri Jiwe hawa? Aisee
 
Back
Top Bottom