Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Bashiru Ally Kakurwa amekemea vikali tabia za baadhi ya wanachama wa CCM wanaopanga kukisaliti Chama katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu kwa maslahi yao binafsi. Ameahidi kuwachukulia hatua kali watakaobainika kusaliti Chama ikiwemo kuwafukuza Uanachama.

Usidandie treni kwa mbele! Tayari kabla hata ya kura CCM ina ushindi karibu asilimia 50 kutokana na upande wa pili kuuza nafasi zao walizogombea!! Magu anasubiri kuapishwa!! Mtangoja sanaa! Na wale miungu watu imekula kwenu!!! Na wale wapambe wa miungu watu hahaaa! Endeleeni kulamba malimaooo!!
 
Unayo elfu kumi mfukoni kwako muda huu?
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Bashiru Ally Kakurwa amekemea vikali tabia za baadhi ya wanachama wa CCM 1Zaiwanaopanga kukisaliti Chama katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu kwa maslahi yao binafsi. Ameahidi kuwachukulia hatua kali watakaobainika kusaliti Chama ikiwemo kuwafukuza Uanachama.

Zaidi ya nusu wanampango huo je tutafukuzwa wote ?
 
Viongozi ndio wamewasaliti wanachama,haiwezekani tunachagua ambao sisi tunaona wanatufaa kutuongoza afu mnakata majina bila sababu za msingi na hazipo wazi. kwa maslahi yenu.yaaani ukiweza kuwainga viongozi wa chama WILAYA na mkoa wanakupa Alama za juu mnakata tuliwachagua kwanyw Kura za maoni.
Ni Bora mgebadilisha utaratibu wagombea wachukue fomu na kurudisha Kisha mkae na kurudisha mnaemtaka kuliko kutusumbua mnatupandisha malor uja kwenye uchaguzi wa chama,i kumbe kuna wapendwa wenu tayari.
Pamoja na yote hayo.kwa sasa ni nchi halafu chama. Tunaweza kukubali wagombea ubunge "waliobebwa" wajibebe wenyewe mbele ya wananchi lakini kwenye uraisi ni hatari sana kufanya usaliti. Kuna masuala ya msingi ya kuyasimamia kwani angepata fulani ubunge ungenyanyua miguu juu na kuacha kujitafutia riziki? Hawa wanaweza kuadhibiwa kwa kukosa kura lakini kusaliti chama kikakosa uongozi wa kitaifa inaweza kuleta majuto makuu. Ni kama mkatoliki marekani kuchagua democrat ni kuhatarisha wokovu wa roho yako maana imani ya democratic party inapaisha kuzimu sasa pamoja na kasoro zote za Trump ni morally wrong kutompigia kura ukimlinganisha na Biden.
 
Mimi najua kafukuzwa,maana kauli ya Ccm ni hivyo. Sasa labda una hisia zako, maana wewe kila kitu ni hisia.

Hiyo ndio maana ya jicho la tatu. Ww fuata hicho ulichotangaziwa maana ndio uwezo wako wa kuona unapofikia.
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Bashiru Ally Kakurwa amekemea vikali tabia za baadhi ya wanachama wa CCM wanaopanga kukisaliti Chama katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu kwa maslahi yao binafsi. Ameahidi kuwachukulia hatua kali watakaobainika kusaliti Chama ikiwemo kuwafukuza Uanachama.

Mpaka ameamua kusema basi hali ni tete
 
Pamoja na yote hayo.kwa sasa ni nchi halafu chama. Tunaweza kukubali wagombea ubunge "waliobebwa" wajibebe wenyewe mbele ya wananchi lakini kwenye uraisi ni hatari sana kufanya usaliti. Kuna masuala ya msingi ya kuyasimamia kwani angepata fulani ubunge ungenyanyua miguu juu na kuacha kujitafutia riziki? Hawa wanaweza kuadhibiwa kwa kukosa kura lakini kusaliti chama kikakosa uongozi wa kitaifa inaweza kuleta majuto makuu. Ni kama mkatoliki marekani kuchagua democrat ni kuhatarisha wokovu wa roho yako maana imani ya democratic party inapaisha kuzimu sasa pamoja na kasoro zote za Trump ni morally wrong kutompigia kura ukimlinganisha na Biden.

Ni kweli bora umewaonya mboga mboga wenzake, maana siku ccm inapoteza dola, itaendwa kuzikwa kaburi la pembeni ya KANU ya Kenya. Na vile wanaccm wamezoea mbeleko kwenye maisha, wote mtaolewa.
 
mvurugano wa ccm huchangiwa pakubwa na mchakato wa kuteua wagombea maana kuna watu wanakatwa ajili ya matakwa ya watu akati kura za wajumbe zimewabeba

kuepusha usaliti wabadili mfumo wa kupata jina la mgombea, wawe wanaandika vikaratasi vya majina yote ya wagombea kisha vinakunjwa na kutiwa kwa box alafu atakaebahatika kusomwa mwanzo ndo anakua kabahatika, hii italinda umoja na mshikamano
 
Hali hii ikiendelea Hadi 2025 CCM itakuwa KANU
Na haiwezi kubadilika kwa sababu Magufuli anaongozwa na hulka ya ubabe uliopelekea kujibatiza jina la Jiwe. Hawezi kukomaa kisiasa na kiutawala. Angaa mwenzake, Kikwete, wakati anaingia muhula wa pili alikuwa amekomaa kiasi na ndio maana aliweza kusikia kilio cha Watanzania wote (waCCM na wasio waCCM) cha kutaka katiba mpya na akaamua kukifanyia kazi. Kama sio ubishi wa wahafadhina wa ccm, leo hii tungekuwa na katiba mpya ambayo ndio dawa pekee ya mfumo uliochoka, mfumo ambao ndio wenyewe mfumo fisadi. Watu wanawanyooshea vidole watu kama Lowassa nk kuwa ni mafisadi, lakini mfumo tulionao ndio wa kifisadi - maamuzi ya Magufuli ni ya kifisadi, mfumo wa bunge na marupurupu wanayopeana ni ufisadi - haishangazi unaona mama wa watu anaacha heshima zake zote za u-first lady mstaafu anatamani kwenda bungeni kugonga meza! Katiba mpya ya wananchi ingebadilisha upuuzi wote huu!!
 
Imefika ukingoni
 
Wakuu, Katibu Mkuu wa Ccm ametishia kuwafukuza wanaccm ambao wamepanga kumpa kura tundu lisu na kufikia mahali Ya kusema kuwa, watafukuzwa na watataifishwa Mali zao.

Unajua watu wanafanya mzaha na siasa za kutisha na kutumia manguvu pasipo ueredi na mwisho kutatokea anguko kubwa lisilotegemewa, siasa inataka akiri sio nguvu, Katibu badala Ya kutumia maneno Ya busara anatishia watu kuwa atawafukuza huku akijua kuwa kupiga kura ni Siri ya mtu mmoja, hupaswi kutisha watu kisa watapiga kura Kwa mtu mwingne huku ukijua kuwa kura ni Siri, Katibu alipaswa kutafuta sababu Kuu Ya wanaccm kupanga kupiga kura upinxani

Nimeshukuru Sana Ccm kugundua kuwa watu wamepanga kupiga kura Kwa upinzani nikiwemo Mimi Mwana Ccm Kada na kuna watu nawajua zaid ya Mia watapiga kura upinzani, Katibu ameshindwa kutambua kuwa kuweka haya hadharani ameshtua wengne waliokuwa wakinyanyaswa na Mwenyekiti kujiunga kwenye huo msafara

Naomba kumuuliza Katibu kuwa Mwenyekiti Alikuwa anachukua wapinzani anawapa vyeo anatuacha sisi miaka Yote, anawachukua anawapa nafasi za kugombea ubunge huku sisi akikataza katakata hata kuwapinga Leo hiii anatutisha? Haingiii akirini Mimi na watu Wangu tulihangaishwa na upinzani Mwaka 2015 had tukafanikiwa kumweeka madarakani halafau akatudharau kusema kuwa yeye ni Ccm Mpya akatutenga Halafu tuingie kwenye sanduku la kura tumpigie haiwezekani, tutapiga kura Kwa wingi Sana Kwa upinzani liwalo liwe hata atutishie afanye anachofanya sisi tutaonesha hasira zetu kwenye sanduku
 
Alitishia wapi ?
Atajuaje kuwa kura umepigia nani?
Kura mwaka huu haitakuwa ya siri?
 
Back
Top Bottom