Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Bashiru Ally Kakurwa amekemea vikali tabia za baadhi ya wanachama wa CCM wanaopanga kukisaliti Chama katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu kwa maslahi yao binafsi. Ameahidi kuwachukulia hatua kali watakaobainika kusaliti Chama ikiwemo kuwafukuza Uanachama.

"Wanaohama CCM wakidhani wananguvu, wakitoka wanageuka kama vichaa, wafuatilieni wote waliohama CCM, hakuna mwanaCCM maarufu kuliko CCM, ukijiona maarufu ujue umeazimwa umaarufu na CCM , siku Chama kikikutupa ama ukikitupa umaarufu unakoma. Wapo watakaookota makopo nawahakikishia" Bashiru Ally.



Maoni ya Kada wa CCM.

 
Mwambie Bashiru asitutishe! Nani aliwaambia wafanye ubabe na kutuona wanaCCM ni wajinga? Inakuwaje tunachagua watu wanawakata? Inakuwaje wanachapisha fomu moja ya uraisi na kuzuia watu wasigombee uraisi?

Mwambie pia wanaCCM tuna uhuru kama wananchi wa Tanzania wa kumuunga mgombea urais, ubunge na udiwani wa Chama chochote kile na wala sio dhambi.
 
Wajiulize kwanini wanachama wanasaliti na wakipata jibu wadeal na hiho sababu na si watu. Naamini wapo wanachama wengi wanamapenzi na Lissu na sera zake na watampigia kura hiyo tar 28.
 
jingalao, johnthebaptist Elitwege, stroke, njooni huku kuna ujumbe wenu.
 
Quinine,
Unawatishia wanachama? Waliotia Nia kugombea ccm na kukosa kura au kukatwa majina yao 100% wapo upinzani. Watumishi wa Umma wako upinzani 100% watumishi wa umma walio tia Nia kugombea na kukatwa mishahara yao,kutolipiwa madeni ya bank na kuwachangia uchaguzi fedha zaidi ya milion moja kila mjumbe wako upinzani 100% vyeti feki wako upinzani 100% wafanyabiashara wako upinzani 100% waliokuwa na maduka yakubadilishia fedha wako upinzani 100% walio hitimu vyuo wako upinzani 100% wakulima na wafugaji usiseme. Tafuteni suluhu na haya makundi mkitaka chama kiwe salama. Hali sio shwari.
 
Hali hii ikiendelea Hadi 2025 CCM itakuwa KANU
 
Mbona hawaguzi waZanzibari huko ambako CCM wanakaribia kutowaroho kama washatoana roho, yele yale ya Mwalimu Nyerere ukimaliza kuwabaguwa wengine utaanza kubaguwa hata ndani mwako ndio ilipofikia CCM leo hii.
Mwenyekiti wa CCM Taifa anatokea,Mkoa wa Geita Kanda ya ziwa, jirani na mkoa wa Geita ni mkoa wa kagera anatokea katibu mkuu wa chama, Kanda ya ziwa. Katibu mwenezi anatokea mkoa wa Mara ,Kanda ya ziwa.mnategemea ccm iko salama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…