Siyo hayo tu, kuna watu hawajaathiriwa moja kwa moja na mfumo mbovu wa uongozi wa magu lakini roho zao zipo upinzani, hata kama hujaguswa ile kuona wapinzani wananyanyaswa na kupewa kesi za kubambikiwa, Mpinzani mmoja amenusurika kuuawa kwa risasi nyingi na uchunguzi haujafanyika hadi leo, kuona watu wakifilisiwa kwa sababu ambazo ni petty ambapo zingetumika njia zisizo na madhara kumuadhibu mhusika (Manji) badala ya kuharibu biashara zake zilizotoa ajira za maelfu ya watu, kuona Rais akiisigina katiba kwa miaka mitano mfululizo, kuona Rais amejigeuza mungu-mtu kila mtu anamwabudu, kuona kuna sehemu zikididimizwa kimaendeleo na zingine zikipendelewa, na madudu mengine mengi, haya mambo yamechosha watu lazima sote tuwe upinzani.
WaTz tuache ubinafsi tujifunze kupaza sauti na kufanya maamuzi kwaajili ya wengine, kwa yanayoendelea nchini haihitaji uathiriwe moja kwa moja ndipo uone upinzani ni mbadala. Yanayoendelea ni machafu tuyapinge kwa nguvu zote hata kama unajiona uko safe kwa sasa.
Tuwachague wapinzani ili tuwadai katiba mpya ambayo itatumika kuwaondoa na wao wakiharibu. Hakuna chama kinachotakiwa kujiona kina hati miliki ya kuiongoza nchi hii pekeyao, CCM hawawezi kutupa katiba mpya kwasababu hawajawahi kuiahidi, Shime watanzania.