Wakuu, juzi kati nilipita kwa mguu kwenye daraja la Tanzanite.
Nilishtuka sana kuona kuwa daraja lina nyufa kila sehemu.
Sikuamini kama ningeweza kuvuka salama kabla daraja halijatumbukia.
Baada ya kufanya utafiti wa kina nilionelea kuwa lile daraja limejengwa eneo lenye sesmic waves (mitetemo) ya hali ya juu kitu ambacho kina athiri daraja na kulipunguzia urefu wa maisha.
Nawashauri Tanroads kuchukua hatua za haraka kwa kulifunga dampers daraja la Tanzanite ili kupunguza mitetemo ambayo inaathiri daraja hilo kwa kasi ya mwanga.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.
View attachment 2382330View attachment 2382329View attachment 2382335