Hali ya barabara ya Dumila - Handeni - Korogwe, Je ni barabara ya lami au vumbi?

Hii Imeenda Mdau
 
Maelezo yako yamenisisimua.
Kuna milima iliwahi kunitesa, nilikuwa nimepata ajali jana yake nikanusurika, kesho yake nilitakiwa kuendelea na safari na ilikuwa ni kupandisha milima mwanzo mwisho.

Wenge la ajali lilinitesa sana.

Kuna wakati nilikuwa naegesha gati nasali kwanza.

Ulikuwa wakati mgumu sana na gari pamoja na kutegenezwa lkn ghafla breki zilianza kufeli
 
Pole sana kwa hali iliyokukuta chief! Jamaa yupo detailed vizuri sana kiasi kwamba ukifuata maelekezo yake safari yako lazima iwe ya mafanikio. Na inavyooneka ni dereva mzoefu!

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Duh, kweli watanzania hatuna furaha! Hapo nimekutangazia nini? Pili unaniita kijana, unanifahamu? Kama umeona uzi wangu unashida nyamaza watu wenye msaada wachangie.
Huwezi nipangia humu cha kuandika kwani hukunileta au kunifundisha kutumia jf
 
Hiyo njia ni ya vumbi vinginevyo labda upite chalinze
 
Ongea osie kweli we unaijua hiyo njia sio hao wahuni waliotangulia kucomment wakati wapo Kizuramimba au Buzirayombo hawajawahi hata kufika makao nakuu ya mikoa yao
 
Kama shida ni kukwepa rough road na kupunguza safari nashauri ukiingia kipande cha barabara ya Dumila-Turiani(lami) then Turiani-Mziha-Kibindu-Mbwewe(Vumbi). Then Mbwewe-Segera-Korogwe-Lushoto(lami).

Kipande cha kutoka Turiani-Handeni(Vumbi) ni kirefu sana na service yake siyo ya mara kwa mara kulinganisha na Mziha-Mbwewe Ridhiwani tumpe maua yake anajitahidi sana kukarabati barabara za jimboni kwake.
Kwahiyo nakushauri tumia route hiyo kurahisisha trip yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…