Hali ya barabara ya Dumila - Handeni - Korogwe, Je ni barabara ya lami au vumbi?

Hali ya barabara ya Dumila - Handeni - Korogwe, Je ni barabara ya lami au vumbi?

Kama kutokea huko magharib safar yako itakufikisha singida basi pita manyara, arusha kilimanjaro then waingia korogwe
Habari wakuu,

Mwezi wa kumi na moja nina safari ya kwenda Lushoto kwa kutumia usafiri binafsi. Kiufupi mimi ni mgeni katika mkoa wa Tanga na sijui hali ya barabara mkoani humo. Ninaishi kwenye moja ya mikoa ya kanda ya magharibi mwa Tanzania.

Barabara ninayotaka kutumia ni ile ya kutoka Dodoma kwenda Morogoro. Ningependa kupita njia fupi pindi nitakapofika Dumila, yaani nitumie barabara ya Dumila - Handeni - Korogwe (wastani wa kilomita 230 kwa mjibu wa google map).

Kwa wenyeji wa mkoa huu au wale waliowahi kutumia barabara hiyo, ningependa kupata maelekezo yenu yatokanayo na uzoefu wenu, je barabara hii Dumila - Korogwe ni lami? Kama ni ya vumbi, inapitika wakati wa masika?

Asanteni sana.
 
Maelezo yako yamenisisimua.
Kuna milima ilowahi kunitesa, nilikuwa nimepata ajali jana yake nikanusurika, kesho yake nilitakiwa kuendelea na safari na ilikuwa ni kupandisha milima mwanzo mwisho.

Wenge la ajali lilinitesa sana.

Kuna wakati nilikuwa naegesha gati nasali kwanza.

Ulikuwa wakati mgumu sana na gari pamoja na kutegenezwa lkn ghafla breki zilianza kufeli
Aisee pole sana I can feel your situation there, Huwa Haya mausafiri muda mwingine yakiamua kuzingua huwa ni tatizo kubwa sana, unaweka rehani uhai yaani. Mi kuna siku kutoka Nara kufika Dodoma Mjini ilitumia masaa 5 gari ilikuwa inachemsha
 
Most welcome, Lushoto is till vargin land, full of greenish everywhere
Mkuu asante sana.
Nimezunguka sana nchi hii karibia kila wila lkn Lushoto sijafika naiona juu milimani nikipita Mombo.

Sifa zake zinanivutia.

Navutiwa na baridi la huko, utulivu na mazingira jinsi inavyosifiwa.

Panapo majaaliwa mwaka huu natanani kuja
 
Ongea osie kweli we unaijua hiyo njia sio hao wahuni waliotangulia kucomment wakati wapo Kizuramimba au Buzirayombo hawajawahi hata kufika makao nakuu ya mikoa yao
Honga mgoshii, nzenze??
 
Mkuu ukifika turiani weka kituo kidogo tupate kuku wa kuchoma[emoji3][emoji3]

Kama unatokea dodoma pita njia ya Turiani-handeni njia ni nzuri na ni fupi sana
 
Ni lami tupu kutokea hapo Dumila-Turiani-Mziha-Negelo-Handeni mpaka Korogwe. Ila uwe makini kuna maeneo kadhaa yana kona sharp.
Mimi huwa nalima Kijiji kinaitwa Dihinda, ukitoka Madizini Turiani unavuka shamba la mitiki la Mtibwa then unaingia hapo Dih. Miezi 2 iliyopita nilikuwa huko lami ambayo imetoka pale Feri (mbele kidogo ya Dumila ukiwa unaelekea Dakawa) imeishia pale njia panda ya kwenda Madizini au Mtibwa Sugar factory... Huko mbele pote ni vumbi tuu...
 
Asante sana kiongozi kwa maelezo yaliyojaa nyama za kutosha! Uzuri gari langu ni Harrier hivyo inaweza kupita rough road sema tu comfortability baada ya kuendesha safari ndefu kwenye lami inapungua na inahalibu ladha ya safari.

Nitaona muda ukifika na ukizingatia msimu huu TMA nao wanasema kuna el nino sasa sijui kama haitakuwa na shida sana hasa hivyo vipande vya vumbi.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Nakushauri ukifika Dumila nyoosha mpaka Morogoro mjini, pale Msamvu ingia Terminal Pub ugonge menu, wana nyama, kuku, samaki fresh sanaa, huku gari ikioshwa kwenye car wash yao... Baadae nyoosha mguu mpaka njia panda ya kwenda kwa mzee wa Msoga, lami tupu unakuja kuibuka mbele huko unaungana na barabara ya Chalinze - Segera...
 
Back
Top Bottom