Hali ya biashara imekuwa mbaya kiasi gani mpaka kuna makampuni yanapumulia mashine kwa kuajiri interns wa kujitolea ?

Hali ya biashara imekuwa mbaya kiasi gani mpaka kuna makampuni yanapumulia mashine kwa kuajiri interns wa kujitolea ?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Kuna kampuni waajiriwa wake karibia wote ni interns wale wa kujitolea bure au posho ya laki wakiwa na matumaini ya kuajiriwa siku moja. Lakini ahadi hizo huwa ni maneno tu, wakizichoka na kuondoka ni kitendo cha kufumba na kufumbua wengine wanakuja kujaza nafasi zao kana kwamba hakuna kilichotokea.

waajiriwa rasmi ni wachache wa kuhesabika kama muhasibu na meneja
 
Kuna kampuni ilinishangaza sana, waajiriwa wake karibia wote ni interns wale wa kujitolea bure au posho ya laki kwa ahadi zisizo na mwisho wajitahidi wataajiriwa.

waajiriwa rasmi ni wachache wa kuhesabika kama muhasibu na meneja
Bosi hana uwezo wa kuitwa boss ila ana force king tu.
 
Nchi iliyofirisika si rahisi Wafanyabiashara wa halali kufanikiwa
 
80% ya shughuli za uchumi ni imports. Kuanzia bidhaa, na huduma vyote ni vya wageni raia wanabakia kuwa wanunuzi na wachuuzi.

Uchumi hauwezi kukua wala kuwa functional kwa style hii.

Pale kariakoo ukitazama ndio kuna mzunguko mkubwa wa bidhaa nyingi tunazotumia kama raia na bidhaa nyingi zinazonunuliwa na raia zinatokea kariakoo.

Kwa style hiyo sasa inamaanisha kuwa uchumi wetu sio productive economy ni consumer economy,tuna export ajira na resources zetu nje.

Wanaichi wanabakia kuwa walanguzi tu na matapeli ili kuishi mjini na mfumuko wa bei unazidi kushamiri na kukausha mifuko ya kaya.

Imagine ili uishi vizuri na kula chakula kinachotakiwa kwa familia ya kisasa kwa siku huwezi acha chini ya 30,000 ikatosha na hapo ndani mahitaji muhimu yapo.

30,000 mara siku 30, ni laki 9. Laki 9 kwa mwezi kwa mshahara gani? Asilimia kubwa ya watz wanamshahara haufiki milioni 1.

Imagine maisha gani haya tunaishi kizazi hiki sababu ya majitu machache, mabwanyenye yasiyoheshimu sheria,kanuni za uchumi na ustawi wa jamii.
 
Uchumi umekufa, ndio maana nasikitika sana akina Kafulila wanavyopiga porojo
Falulila anatakiwa kuitwa kafulia. Kwa sasa hana sera kabisa amekuwa mtu wa hovyo, chawa mshika bango la mama.

Kipindi kile njaa zilikuwa nyingi na tamaa, anashindwa hata kuongea point za maana za kujenga anabakia kuwa snitch wa taifa.
 
Back
Top Bottom