80% ya shughuli za uchumi ni imports. Kuanzia bidhaa, na huduma vyote ni vya wageni raia wanabakia kuwa wanunuzi na wachuuzi.
Uchumi hauwezi kukua wala kuwa functional kwa style hii.
Pale kariakoo ukitazama ndio kuna mzunguko mkubwa wa bidhaa nyingi tunazotumia kama raia na bidhaa nyingi zinazonunuliwa na raia zinatokea kariakoo.
Kwa style hiyo sasa inamaanisha kuwa uchumi wetu sio productive economy ni consumer economy,tuna export ajira na resources zetu nje.
Wanaichi wanabakia kuwa walanguzi tu na matapeli ili kuishi mjini na mfumuko wa bei unazidi kushamiri na kukausha mifuko ya kaya.
Imagine ili uishi vizuri na kula chakula kinachotakiwa kwa familia ya kisasa kwa siku huwezi acha chini ya 30,000 ikatosha na hapo ndani mahitaji muhimu yapo.
30,000 mara siku 30, ni laki 9. Laki 9 kwa mwezi kwa mshahara gani? Asilimia kubwa ya watz wanamshahara haufiki milioni 1.
Imagine maisha gani haya tunaishi kizazi hiki sababu ya majitu machache, mabwanyenye yasiyoheshimu sheria,kanuni za uchumi na ustawi wa jamii.