Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Hali ya Msanii wa Hiphop Rashidi Makwilo (Chidibenz) inasikitisha sana sana, Siku za hivi karibuni amekua akiishi Msasani (Maandazi road) maskani moja na mateja, Kinachonisikitisha zaidi jamaa anaonekana hayuko sawa kiafya miguu imevimba, anaonekana aliumia na hajapona vizuri,miguu ameifunga bandage na anatembelea ndala, Nimemuona leo asubuhi nikiwa naelekea kazini atembea kwa msaada wa watu wanampa support (Nahisi alikuwa amelewa sana) Uso wake ni kama hauna matumaini

Nitoe wito kwa wasanii wenzake na Familia yake wamfuate pale msasani coz anaishi maskani na hana mtu wa kumuangalia, Sina uhakika ila kuna uwezekano labda amerudi tena kwenye wimbi la madawa ya kulevya

Kwa inavyoonekana ni kama wasanii wenzake wamemsusa, hawana time naye tena Lakini naona sio sahihi coz ni Msanii mwenzao inabidi wakubali kubeba hili jukumu la kumlinda na kumtunza Chidibenz, Juzi kwenye show ya Serengeti pale K/nyama viwanja vya posta, Chidibenz alipanda kwenye show ya Rosa ree lakini hakuchukua mda akashushwa, na alikua amevaa ndala, Wakiendelea Kumtenga hivi depression inaweza ikam-maliza kabisa, Kwa upande wa Familia yake sijui wao wamejipangaje coz inaumiza sana kumuona Ndugu au mtu wako wa karibu akiwa anapitia kipindi kigumu

Vijana tujitahidini sana kuishi kwa nidhamu, Ujana una mambo mengi bila yakua na nidhamu ni rahisi kuanguka
unga ni kitu kibaya sana.
 
Uko sahihi. Na mbaya zaidi tunajifanya hatuoni. Sijui ni kwa nini msanii akijikwaa watu wanajifanya kusikitika sana wakati kuna wakulima, wafugaji, wamachinga na kila aina ya makundi wanapitia hayo hayo. NB: sisemi watu wasimjali ila nataka tuwe tu aware kuwa wananchi tunakitakiwa kupigana kumwondoa huyu adui wa taifa letu anayeitwa CCM kama tunataka future nzuri.
CCM ndo ilimtuma ale ngada?
 
Back
Top Bottom