Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Kwahiyo lengo la huu uzi wake lilikua ni nini? au huu uzi umewalenga wazazi wa Chid ili wamsaidie? wao hawajui hali aliyonayo mtoto wao?
Kwa wanaotaka kumsaidia kwa kupenda wamsaidie, ila huwezi kumlaumu mtu eti kwa nini hajamsaidia...watu mnataka kufanya kama vile kusaidiwa ni haki yenu kwa upuuzi mliochagua kuufanya wenyewe?
The world don't owe you nothing, no matter what you have been through
 
Kwa wanaotaka kumsaidia kwa kupenda wamsaidie, ila huwezi kumlaumu mtu eti kwa nini hajamsaidia...watu mnataka kufanya kama vile kusaidiwa ni haki yenu kwa upuuzi mliochagua kuufanya wenyewe
The world don't owe you nothing, no matter what you have been through
Hujaielewa comment yangu,umekurupuka tu,ndio maana niliyemquote hakunijibu,
Soma tena comment zangu kwa utulivu,

Ni upuuzi gani mimi nimeamua kuufanya? Jiheshimu ili uheshimiwe.
 
Mimi sikuzungumzii wewe, nazungumzia mawazo yako na ya wengine, wanaodhani kuwa wana haki ya kusaidiwa
Kama hii ndio hoja yako basi mpinge mleta mada coz ndio ameleta mada na kuwalaumu wasanii kwa kutomsaidia Chid,ndio maana mimi nikamuuliza,"Kabla ya wewe kuamua kuwalaumu wasanii,je wewe ulimpa msaada gani Chid?"
 
Chidi ni rapa mkali sana ila mfumo wa nchi kwenye mziki wa hip hop haujampa mafanikio kulinganisha na alichotoa(uwezo wake) imepelekea kupata msongo wa mawazo na kutumbukia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Mtu mwingine anayekuja kwa sifa ni Young dee soon kitaumana.
Naona wenge wanasingizia kuwa Sombdy alikuwa mkali sana ,baadae stress za kutopata mafanikio ya mziki akaingia humo. The same ilisema kwa Albert Mangwea , LANGA etc.

Lakin nawaza tofauti,wengine inaweza kuwa wameingia kwa kutest,kuchanganyia tu vijiwe vyao vya bangi, wengine mkumbo tu mtu anaona naweza kaa na wala unga ni marafiki zangu hawawez nishawish, LAKIN MTU HUWEZI SHINDA MAZINGIRA.

Kuna wengi tu game hazijawalipa, wakina Prof Jay hao ni wakal wa All the time ,wamekaa ktk game before Chidbez hajapata fame, But hakuingia ktk drugs.

Kuna wacheza boxer wakali, wacheza mpira na wasaniii wengine waliobaki kuwa under dogs thou wamekaa ktk game long time sanaa.

Kuna hao madogo bado wanahitaji character development, ndani mwao wanaona Shisha, bangi, pombe kali ndio ustaaaaaaaa ( Humo ktk hayo makundi ndo wanajikuta ktk uraibu wa hayo mambo , au ku Upgrade kuingia ktk madawa)

Ishu iliyopo ni kuwa clean plus management inayo eleweka.
 
Hali ya Msanii wa Hiphop Rashidi Makwilo (Chidibenz) inasikitisha sana sana, Siku za hivi karibuni amekua akiishi Msasani (Maandazi road) maskani moja na mateja, Kinachonisikitisha zaidi jamaa anaonekana hayuko sawa kiafya miguu imevimba, anaonekana aliumia na hajapona vizuri,miguu ameifunga bandage na anatembelea ndala, Nimemuona leo asubuhi nikiwa naelekea kazini atembea kwa msaada wa watu wanampa support (Nahisi alikuwa amelewa sana) Uso wake ni kama hauna matumaini

Nitoe wito kwa wasanii wenzake na Familia yake wamfuate pale msasani coz anaishi maskani na hana mtu wa kumuangalia, Sina uhakika ila kuna uwezekano labda amerudi tena kwenye wimbi la madawa ya kulevya

Kwa inavyoonekana ni kama wasanii wenzake wamemsusa, hawana time naye tena Lakini naona sio sahihi coz ni Msanii mwenzao inabidi wakubali kubeba hili jukumu la kumlinda na kumtunza Chidibenz, Juzi kwenye show ya Serengeti pale K/nyama viwanja vya posta, Chidibenz alipanda kwenye show ya Rosa ree lakini hakuchukua mda akashushwa, na alikua amevaa ndala, Wakiendelea Kumtenga hivi depression inaweza ikam-maliza kabisa, Kwa upande wa Familia yake sijui wao wamejipangaje coz inaumiza sana kumuona Ndugu au mtu wako wa karibu akiwa anapitia kipindi kigumu

Vijana tujitahidini sana kuishi kwa nidhamu, Ujana una mambo mengi bila yakua na nidhamu ni rahisi kuanguka
Bongo fleva inalostisha sana wasanii na ndiyo maana wengi wao wanashikishana ukuta kupata fame
 
Langa alikua smart sana upstairs ,bhas tuu ujana una mambo mengi
Kuna kipindi 2009 nilikuwa pale kituoni manyanya ...akapita Langa, mchizi wangu mmoja akanistua umemuona langa...dah aisee sikuamini aisee ...alibaki kichwa tu.!! kaisha mpaka nikamuuliza jamaa, langa ana shida gani ..akanambia kuwa anatumia madawa ya kulevya na hapo alikuwa anaelekea kuvuta huko maeneo ya brazil.

Chid benz nae nilikuja kumuona 2015 maeneo ya msasani anaelekea maandazi road akapita maskani kachoka vibaya, chini ana ndala tu, kabaki kichwa mwili wote umeisha aisee..anaelekea kwa mateja wenzake kwenda kupata kete.
 
Wampeleke kwenye sober ya Pili Misana akakae kule mwaka mzima ili awe clean.

Ila kwa jinsi tabia yake ilivyo ni mtu asiyetaka kushaurika. Hata akipelekwa atatoroka tu
 
Kwa wanaotaka kumsaidia kwa kupenda wamsaidie, ila huwezi kumlaumu mtu eti kwa nini hajamsaidia...watu mnataka kufanya kama vile kusaidiwa ni haki yenu kwa upuuzi mliochagua kuufanya wenyewe?
The world don't owe you nothing, no matter what you have been through
Umezungumza fact, msaada sio lazima bali ni utashi wa mtu/watu
 
Naona wenge wanasingizia kuwa Sombdy alikuwa mkali sana ,baadae stress za kutopata mafanikio ya mziki akaingia humo. The same ilisema kwa Albert Mangwea , LANGA etc.

Lakin nawaza tofauti,wengine inaweza kuwa wameingia kwa kutest,kuchanganyia tu vijiwe vyao vya bangi, wengine mkumbo tu mtu anaona naweza kaa na wala unga ni marafiki zangu hawawez nishawish, LAKIN MTU HUWEZI SHINDA MAZINGIRA.

Kuna wengi tu game hazijawalipa, wakina Prof Jay hao ni wakal wa All the time ,wamekaa ktk game before Chidbez hajapata fame, But hakuingia ktk drugs.

Kuna wacheza boxer wakali, wacheza mpira na wasaniii wengine waliobaki kuwa under dogs thou wamekaa ktk game long time sanaa.

Kuna hao madogo bado wanahitaji character development, ndani mwao wanaona Shisha, bangi, pombe kali ndio ustaaaaaaaa ( Humo ktk hayo makundi ndo wanajikuta ktk uraibu wa hayo mambo , au ku Upgrade kuingia ktk madawa)

Ishu iliyopo ni kuwa clean plus management inayo eleweka.
Paragraph ya pili ndio ukweli ulipo wala sio stress, wengi hula mjani na hapo kwenye mjani ndio kunachanganyiwa hayo makitu
 
TUMATAFUTE "KALAPINA" baada ya miezi mitatu atupe mrejesho
 
Kuna kipindi 2009 nilikuwa pale kituoni manyanya ...akapita Langa, mchizi wangu mmoja akanistua umemuona langa...dah aisee sikuamini aisee ...alibaki kichwa tu.!! kaisha mpaka nikamuuliza jamaa, langa ana shida gani ..akanambia kuwa anatumia madawa ya kulevya na hapo alikuwa anaelekea kuvuta huko maeneo ya brazil.

Chid benz nae nilikuja kumuona 2015 maeneo ya msasani anaelekea maandazi road akapita maskani kachoka vibaya, chini ana ndala tu, kabaki kichwa mwili wote umeisha aisee..anaelekea kwa mateja wenzake kwenda kupata kete.
Dah haya madawa yametuharibia vipaji vingi sana, Langa alikuja kustuka ikiwa too late, Maleria kali ikamuondoa nafkiri kinga za mwili zilishakua weak sana, Nakumbuka kipindi cha Msiba wa Albert Mangwea alienda FNL kutambulisha video ya wimbo wake wa Rafiki wa kweli, Na Sammisago akamuuliza kuhusu Ngwair jamaa akafunguka kwa upande wake then akawekewa beat afanye freesyle kuhusu Albert ngwea ...then One week later nayeye akafariki ...
 
Wampeleke kwenye sober ya Pili Misana akakae kule mwaka mzima ili awe clean.

Ila kwa jinsi tabia yake ilivyo ni mtu asiyetaka kushaurika. Hata akipelekwa atatoroka tu
KigambonI kwa Pili misana alishapelekwa kipind kile mwanzoni kabisa,then akaja kupelekwa Zanzibar, then Bagamoyo, Alivyotoka Bagamoyo kidogo ndo alibadilika kabisa,akapata hadi mwili , ila ndo hivyo amerudi tena kwenye njia yake
 
Back
Top Bottom