Sangizi
JF-Expert Member
- Nov 9, 2015
- 1,942
- 4,230
Hakuna uraibu wenye ubora, uraibu ni uraibu tu na wote una madhara kwa mraibu.Bora uraibu wa kamari kulilko UNGA.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna uraibu wenye ubora, uraibu ni uraibu tu na wote una madhara kwa mraibu.Bora uraibu wa kamari kulilko UNGA.
Kuna siku aliingia kitambaa cheupe Ile Tabata akawanyang'anya pombe Na kuwagawia marafiki zake anaowafahamu yeye Na kuondoka zake......ukweli ni kuwa chidbenz hashauliki....Shida ya Chidi habebeki. Mtu kama blue anambeba sana na hujawahi kumtupa ila dk sifuri anaharibu. Kingine u-born town nao unamcost much know, mjanja yeye.
Hana nguvu ila ule ubabe wa Chidi yule Benzino wa miaka Ile ya 1990s mitaa ya Kkoo, ilala bado anauleta kumbe anaharibu
Hata kama ingekua na views milioni mia,hiyo haikupi uhakika kua Chid amepata msaad,ila msaada wako kwake ingekua ni uhakika,Kutoa tuu taarifa inaweza ikawa msaada coz JF ni platform kubwa sana, angalia hii thread sahv ina views zaidi 5k, utajuaje mmoja kati yao akafanya maamuzi ya kwenda kumsaidia?
Walikuwa hawana utaalamu wa huduma ya kwanza.......Hayo ni makosa yake mwenyewe sio masela mavi sijui upumbavu gani, mtu umelewa unashauriwa usiende kuogelea, unalazimisha, unazama unakufaWalienda beach hapo Koko nahisi km sijakosea Kunduchi wakala mitungi sasa Jamaa 'Pancho Latino' akiwa amelewa akawaambia wenzie anataka akaogelee wakamzuia Ila akakomaa basi wakabidi waende kwenye maji Jamaa akaingia vizuri tu kaanza maji ya ugoko akaendelee mbele maji kiunoni akaendelee mbele maji ya SHINGO
Kumbuka hapo amelewa tungi basi vuaaaa mara hawamuoni wakaanza kupagawa Pancho yupo wapi Pancho yupo wapi wakapigwa bumbuwazi Pancho kazama ikabidi wapige kelele ndio wale Beach boys waje kutoa msaada
Beach boys wakazamia huku na huku huku na huku mara Pancho huyu hapa wakamuibua kwenye Maji Pancho hakua amekufa alipoibuliwa alikua kwenye Koma Ila ilibidi apatiwe huduma ya kwanza ya haraka angepona maana Mwili ulikua bado unapapatika wakiwa wamembeba wale beach boys na mapovu yanamtoka mdomoni na puani wakamweka chini kumkamua maji
Steps za kumkamua maji wakakosea wao walikua wanaminya tumbo lake wakati inabidi uminye kifuani na sio tumboni
Kumbe wakati huo maji yashaingia kwenye Mapafu kingine hawakumpuliza Mdomo kumuongezea Hewa kwenye Mapafu ili maji yaweze kutoka mdomoni na puani wala kumminya Pua ili kusudi Hewa ikijaa ndani maji yanamtoka mdomoni na puani wala hawakumpasha Joto Mwili wake maana Mwili unahitaji nguvu alikua kashalegea
Na ilibidi kuminya kifua chake ila wakambeba huku wanalialia kwamba Pancho ameshakufa lakini laiti wangejua pale walipomtoa kwenye Maji hakua amekufa alikua kwenye Koma nahisi ni tungi ndio zilizowazuzua mpaka wanafika hospital too late taarifa inakuja Pancho Latino is dead
Nimekusimulia kwa mujibu wa Clip waliyoirusha wao wenye waliokua nae kipindi cha umauti unamfika kule baharini
RIP Pancho Latino
Amsaidie kwani yule ni mtoto wake? Hakuna mtu anayewajibika kwa maisha ya mtu mzima mwenzake mzeeHata kama ingekua na views milioni mia,hiyo haikupi uhakika kua Chid amepata msaad,ila msaada wako kwake ingekua ni uhakika,
Wewe hukua na uwezo wa kumsaidia? kwanini unawalaumu wasanii kutomsaidia? unaonaje ukaanza kujilaumu wewe kwanza? Be the change that u want to see in the World,usitegemee wengine wafanya kwa ajili yako.
Sasa ndo nimemfunga.Kama wewe ni komeo la chuma, yeye ndio chuma mwenyewe. Bahati mbaya tu maisha yamembadilikia kabisa
Kwahiyo lengo la huu uzi wake lilikua ni nini? au huu uzi umewalenga wazazi wa Chid ili wamsaidie? wao hawajui hali aliyonayo mtoto wao?Amsaidie kwani yule ni mtoto wake? Hakuna mtu anayewajibika kwa maisha ya mtu mzima mwenzake mzee
Young Dee vp ,si alishaacha madawa
Mkuu si amesemwa hapo kuwa ni chid...msanii wa muziki au unataka maelezo gani?!Mnaongea kwa mafumbo. Na sisi wengine tunataka kumjua. Ni nani huyo?
Mkuu,Mkuu Chidibenz angekua kaka ako ,sidhani kama ungemuacha aendelee kuishi maisha anayoishi sasa
Mwehu ashauriki mkuuKuna siku aliingia kitambaa cheupe Ile Tabata akawanyang'anya pombe Na kuwagawia marafiki zake anaowafahamu yeye Na kuondoka zake......ukweli ni kuwa chidbenz hashauliki....
Huo ndo ukwelimadawa atumie yeye kuumia uumie wewe..chid alikua miyeyusho utoto wa mjini mwingi
hasaidiki. dk 2 mbele anakuchenjia. yeye aishi tu akifa tunazika. ndio maisha.
Siku zote binadamu huwa tunavuna tulichopanda, Chidi Benz kitakachomsaidia kubadilika ni yeye mwenyewe kuamuakuwa anatakiwa kubadilika na niwajibu wake na siyo watu au sisi mashabiki tumsaidie kubadilika maana ni mtu mzima. Kingine aache kudeka na kujiona yeye si mtu special anaehitaji huruma, dunia haipo hivyo. Ila kwa wengine ambao tunaona mbali tatizo kubwa la Chidi limeanza kwenye familia na tatizo hilo "Fatherlessness" , mkubalinau mkatae Baba ninkiungo muhimu sanaa kwenye malezi ya mtoto wa kiume.Hali ya Msanii wa Hiphop Rashidi Makwilo (Chidibenz) inasikitisha sana sana, Siku za hivi karibuni amekua akiishi Msasani (Maandazi road) maskani moja na mateja, Kinachonisikitisha zaidi jamaa anaonekana hayuko sawa kiafya miguu imevimba, anaonekana aliumia na hajapona vizuri,miguu ameifunga bandage na anatembelea ndala, Nimemuona leo asubuhi nikiwa naelekea kazini atembea kwa msaada wa watu wanampa support (Nahisi alikuwa amelewa sana) Uso wake ni kama hauna matumaini
Nitoe wito kwa wasanii wenzake na Familia yake wamfuate pale msasani coz anaishi maskani na hana mtu wa kumuangalia, Sina uhakika ila kuna uwezekano labda amerudi tena kwenye wimbi la madawa ya kulevya
Kwa inavyoonekana ni kama wasanii wenzake wamemsusa, hawana time naye tena Lakini naona sio sahihi coz ni Msanii mwenzao inabidi wakubali kubeba hili jukumu la kumlinda na kumtunza Chidibenz, Juzi kwenye show ya Serengeti pale K/nyama viwanja vya posta, Chidibenz alipanda kwenye show ya Rosa ree lakini hakuchukua mda akashushwa, na alikua amevaa ndala, Wakiendelea Kumtenga hivi depression inaweza ikam-maliza kabisa, Kwa upande wa Familia yake sijui wao wamejipangaje coz inaumiza sana kumuona Ndugu au mtu wako wa karibu akiwa anapitia kipindi kigumu
Vijana tujitahidini sana kuishi kwa nidhamu, Ujana una mambo mengi bila yakua na nidhamu ni rahisi kuanguka
Ndio uhalisia wa maisha mkuu, tutasaidiana sana ila lazima kila mtu aishi maisha yake.Chief hili neno sana aisee.
Mkuu usichojua ni kwamba kina chidi benz tunaishi nao hata huku mtaani kwetu, ndugu zetu, watoto wetu, marafiki zetu. Nimesema hivyo kwa sababu nimeshawahi ishi na ndugu mwenye changamoto kama ya chidi, sio kwamba hatuwajali ila kuna muda hawasaidiki kutokana na hali zao.Mkuu Chidibenz angekua kaka ako ,sidhani kama ungemuacha aendelee kuishi maisha anayoishi sasa