Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

KigambonI kwa Pili misana alishapelekwa kipind kile mwanzoni kabisa,then akaja kupelekwa Zanzibar, then Bagamoyo, Alivyotoka Bagamoyo kidogo ndo alibadilika kabisa,akapata hadi mwili , ila ndo hivyo amerudi tena kwenye njia yake
Kuna wazee wana dawa za kienyeji...mlevi yoyote akipewa lazima aache ulevi ..iwe bangi,pombe na hata sigara...labda wampeleke huko.

Mengine yanakuwa mapepo machafu yamemkalia mtu kichwani. Kila akijitahidi kujinasua, yanamrudisha upya...mama ake ampeleke akafanyiwe visomo na apewe dawa za mitishamba. Tatizo mtu mwenyewe ni mjuaji
 
Dah haya madawa yametuharibia vipaji vingi sana, Langa alikuja kustuka ikiwa too late, Maleria kali ikamuondoa nafkiri kinga za mwili zilishakua weak sana, Nakumbuka kipindi cha Msiba wa Albert Mangwea alienda FNL kutambulisha video ya wimbo wake wa Rafiki wa kweli, Na Sammisago akamuuliza kuhusu Ngwair jamaa akafunguka kwa upande wake then akawekewa beat afanye freesyle kuhusu Albert ngwea ...then One week later nayeye akafariki ...
Ukweli ni kuwa mateja wengi ni waathirika wa gonjwa la Ukimwi. Na hawajali kuhusu kutumia dozi wala nini. Na wengi ni walevi wa pombe kali , unakuta kashaunguza maini yote kwa pombe kali.
 
Sure mkuu, kama vp muibukie Kikosini Block 41 Kinondoni
Kalapina alishasema Chid benz hawezi kuacha madawa kwasababu anadeka sana. Madawa mtu haachi kwa kubembelezwa ni mpaka aamue kutok ndani ya nafsi yake kutaka kubadilika laa sivyo unamchukua leo kwenda sober house then kesho anakimbia kurudi mtaani.

Mimi nishashuhudia mteja anaacha unga pasi hata ya kutumia methadone. Alienda tu nafsini mwake akaona amechoka sasa abadilike na akabadilika kweli. Sasa hv hataki hata kuyasikia madawa ,sigara wala pombe.
 
Hivi hizi issue za ushoga kwa bongo fleva lina ukweli kiasi gani
Ni habari ya kitambo sana na waliokuwa wanapakuliwa wanajulikana tu, ila baada ya Chidi Benz kuthibitisha ukweli huo, mada imefufuliwa upya na kushangaza vijana waliozaliwa 2010 kuja sasa!
 
Huyu jamaa kwa alipofikia ni vigumu kurudi tena kwenye ubora wake wa miaka ya 2007 - 2011 hiki kipindi alisumbua sana kwa kupata collabo za wasanii wengi,shows, Tuzo, Hadi akaweza kuanzisha Kipindi chake pale East Africa Tv (Eatv) ila kwavile hakua na Management kwa wakati huo + Ujana hakuweza ku maintain kwa muda mrefu, mpaka kufikia 2012 Chidbenz alishaanza kupotea kwenye ramani na hiki kipindi alipata case nyingi za kuwapiga wasanii wenzake, kuanzia hapo ndo akapotea mdogo mdogo mpaka hapo alipo leo
 
Kwa kile kidonda alicho nacho mguu wa kulia, ukimuangalia unaweza ukalia
Mwezi mmoja nyuma alienda kwa mkuu wa mkoa akitokea boma Kota ndio maskani yao na kwao alipokua. Alipewa Laki 2, akaishia kunywa pombe na kuwatoa masela wake. Ndani ya usiku mmoja waliimaliza ile pesa

Kile kidonda kinamtafuna Sana, alafu miguu yote imevimba. Kikimuuma huwa analia Kama mtoto huku akijikuna

Mungu amfanyie wepesi either kwa kumponja au kumchukua mapema
Huyo wanakosea sana kumpa hela mkononi, ili kumsaidia inatakiwa apelekwe kwenye matibabu moja kwa moja na hilo linawezekana Chid bado ana watu wa kumsaidia.
 
Huyo wanakosea sana kumpa hela mkononi, ili kumsaidia inatakiwa apelekwe kwenye matibabu moja kwa moja na hilo linawezekana Chid bado ana watu wa kumsaidia.
Ukiongea na chid ana madini Sana Sana tatizo ni ujuaji na kujiona yupo sawa..

Niliwai kutana nae pale B kinondoni hope alikua ametimba kwa lufunyo kipindi icho anatembea kwa miguu kutoka ilala mpaka MIKOCHENI hii dunia tuikanyage kwa unyenyekevu ukiteleza TU jua ndio ivyo Tena unaingia kwenye uraibu wa milele
 
Hip hop bila madawa ,inawezekana haijashindikana.

Kalapina aliona mbali sana miaka hiyo ya 2006-2007 alipotoa song na kuwataja wasanii wala ngada lakini hatukumuelewa mpaka gari zilipoanza kuwaka.
 
Back
Top Bottom