Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Hali ya Msanii wa Hiphop Rashidi Makwilo (Chidibenz) inasikitisha sana sana, Siku za hivi karibuni amekua akiishi Msasani (Maandazi road) maskani moja na mateja, Kinachonisikitisha zaidi jamaa anaonekana hayuko sawa kiafya miguu imevimba, anaonekana aliumia na hajapona vizuri,miguu ameifunga bandage na anatembelea ndala, Nimemuona leo asubuhi nikiwa naelekea kazini atembea kwa msaada wa watu wanampa support (Nahisi alikuwa amelewa sana) Uso wake ni kama hauna matumaini

Nitoe wito kwa wasanii wenzake na Familia yake wamfuate pale msasani coz anaishi maskani na hana mtu wa kumuangalia, Sina uhakika ila kuna uwezekano labda amerudi tena kwenye wimbi la madawa ya kulevya

Kwa inavyoonekana ni kama wasanii wenzake wamemsusa, hawana time naye tena Lakini naona sio sahihi coz ni Msanii mwenzao inabidi wakubali kubeba hili jukumu la kumlinda na kumtunza Chidibenz, Juzi kwenye show ya Serengeti pale K/nyama viwanja vya posta, Chidibenz alipanda Wakimtenga hivi depression inaweza ikammaliza kabisa, Kwa upande wa Familia yake sijui wao wamejipangaje coz inaumiza sana kumuona Ndugu au mtu wako wa karibu akiwa anapitia kipindi kigumu

Vijana tujitahidini sana kuishi kwa nidhamu, Ujana una mambo mengi bila yakua na nidhamu ni rahisi kuanguka
Tumchangie pesa ya matibabu aende India. Mazombi rusheni pesa ya matibabu kwenye namba Ile Ile.
 
Upo sahihi sana. Miaka ile ya 2007 wanakuja kina Jah Rule Tanzania, Chid ndie alikuwa msanii kinara wa hip hop Tanzania anaye-repesent muziki wa hip hop anafanyiwa interview kuhusu ujio wa kina Jah Rule.

Kidogo cha kuongezea, inawezekana hii hali yake ipo upande wa kiroho pia.
It's all about business sababu ni Biashara kwani mshauri wa wasanii ni nani au hii NCHI wasanii hawana mshauri?
 
Shida ya Chidi habebeki. Mtu kama blue anambeba sana na hujawahi kumtupa ila dk sifuri anaharibu. Kingine u-born town nao unamcost much know, mjanja yeye.
Hana nguvu ila ule ubabe wa Chidi yule Benzino wa miaka Ile ya 1990s mitaa ya Kkoo, ilala bado anauleta kumbe anaharibu
Kwa hali yake kumlaumu kwa anavyokuwa kwa sasa ni kumuonea tu, huyo tayari sio mzima/timamu kwahiyo ni ngumu sana yeye binafsi kuona kuwa anakosea.
 
Chid mboni alishapona au wewe unazungumzia nini Chid kinachomsumbua sasa hivi ni tungi anakunywa sana na alishashauriwa na Daktari aache mitungi Ila Mzee anarudi kule kule sababu ni masela wanaomzunguka wale masela wa Ilala wote anabidi awapige chini ndio wanaomrudisha SHIMONI
Kupona uraibu wa madawa sio rahisi hivyo hasa km bado anarudi kwenye kampani ileile iliyomuingiza huko, mtu aliyeshakuwq mraibu wa madawa sasa hivi mraibu wa pombe kurudi kwwnye madawa ni kugusa
 
Inauma sana kwa kweli. Nimewakumbuka Salasala boy, Cowboy, Pancho Latino mafia. Kifo hakina huruma
Chunga wanao na masela Mavi sio watu wazuri

Katika vifo vilivyoniuma zaidi ni KIFO cha Pancho Latino wale Jamaa eti anazama wanamuona wanamuacha tu wanaanza kulialia na clip Video wanachukua Ile iliniuma kishenzi

Weka wanao mbali sana na masela Mavi
 
Chidi ni rapa mkali sana ila mfumo wa nchi kwenye mziki wa hip hop haujampa mafanikio kulinganisha na alichotoa(uwezo wake) imepelekea kupata msongo wa mawazo na kutumbukia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Mtu mwingine anayekuja kwa sifa ni Young dee soon kitaumana.
Mfumo wa nchi hii haujawahii kumpa nafuu kijana yyte yule mpambanaji kwenye seckta yyte ile..
Tunaishi kimachale chale sana..
 
Back
Top Bottom