Hali ya kutokupenda ujulikane wewe ni kabila gani maofisini ni uzalendo au ni usaliti?

Hali ya kutokupenda ujulikane wewe ni kabila gani maofisini ni uzalendo au ni usaliti?

Mnaofanya Kazi katika ofisi za Uma na za private lazma mtakubaliana na mim kuwa Kuna watu huwa hawataki wajulikane kuwa yeye Ni kabila gan,mfano watu wa Kanda ya ziwa waliobahatika kusoma na kuajiliwa kwenye ofis za Uma huwa hawapendi wajulikane walikotoka.

Wanawake wa Kisukuma ndo wanaongoza kwa Tabia hii.

Kwa Sasa npo kweny ofis moja ya Uma Kuna jamaa Ni kabila fulan ila hataki ajulikane kuwa yeye Ni kabila Hilo,Kuna ciku alikuwa anaongea na cm kisir kwa kilugha ndo nkajua kuwa kumbe jamaa Ni wa kabila Fulani ila hatak kuongea kilugha na watu wa kabila Hilo hata mkiwa nje ya ofisi.

Swali Ni je yeye anadumisha uzalendo wa kuondoa ukabila au anasaliti kabila lake?

Inabidi tutafute fedha tuweke mabango kila mkoa kuelezea definition halisi ya neno uzalendo, Maana hata wabunge hawajui maana yake!
 
Kuna ofisi nyingine ukitaja kabila lako unadharirishwa kweli kweli.
Ukitaja kabila ambalo ni mkoa ambao uko mpakani utaitwa mkimbizi au mhamiaji haramu!
 
Ni bora kutojua kabila la mtu...maana mtu akishajua kabila lako ndo anaanza kukudefine...
Hata ukifanya kosa dogo utaadhibiwa kulinganishwa na tabia za kabila lako...
Tens zile mbaya zitapewa kipaumbele hasa ukitokea kwenye makabila makubwa yenye mafanikio makubwa mfano wachaga, wahaya, wanyakyusa NK..
Vikabila tofauti na hayo hujifeel inferior mbele ya hizo jamii...so akikutana mtu kutoka jamii hizo tabia zote mbaya hupambikiwa mhusika...


So kuepusha hayo bora ummute Tu kabila lako




Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Wewe umenielewa sana kaka
Maana niliposema atakuwa muhaya wao wakajua nina kitu negative ila nilimaanisha ulichoandika hapo juu kongole
Kubaki ommanye sii.
 
Ukabila ni chanzo cha utenganifu hivyo hauna maana.
Unataka kujua kabila la mtu ili iweje?
Watu walio zaliwa mikoani vijijini sehem moja ndiyo wanatabia ya kuuliza watu makabila yao, lakini watu walio zaliwa mjini huwezi kuwasikia wakiuliza mtu wewe kabila gani tatizo lipo kwa waliotoka mikoani uko maporini.
 
Wengi wanaoficha huwa wanaogopa aibu,Kwan hata ukisema tu mi nmezaliwa sehem fulan Kuna shda gan?
Unaweza ukazaliwa Arusha lakini kabila lako ukawa mzalamu , na unaweza kuzaliwa Dar lakini kabila lako mchaga, kwaiyi kuzaliwa mkoa fulani siyo ndiyo utakuwa kabila la hiyo sehemu, kwanini ungaike na kabila lamtu wakati majina yake la ukoo litakuwa kabila lake, mfano Kaijage, mushi, mwamtobe, Chacha, Masanja, Mapunda, nk utashindwa kujua makabila?
 
Kwani kuna uhusiano wa kabila na mtu anapozaliwa??

Watoto wetu wanazaliwa Amana na Muhimbili haya tuambie kabila gani hao?
Huyu mtoa mada atakuwa kazaliwa vijijini kasomea vijini kaja mjini mtu mzima ndiyo maana anauliza makabila ya wenzake ili ajue Ndungu zake wa mkoani kwao.
 
Kwanza ni uthenge!! Pia kutokujiamini kujua kabila la mtu ili ikusaidie ...nilikuja gundua watu wanafuatilii huu ujinga siku moja Kuna mdada ameniita eti tunaongea ananiuliza unatokea Zanzibar sehemu gani?[emoji26][emoji26][emoji26]binafsi sijawai kukaa hata mwezi Zanzibar na nimeenda hata mara tatu hazifiki nilienda nimekaa siku 4 nimegeuka sasa nikaona anaweza kuwa ananichoka ili apate ukweli.

Siku nyingine Kuna mchaga mmoja anameniita we mdigo mchapakazi katika group la ofisi Tena jamaa ni mtu mkubwa kabisa nilimaindi mi hata kidogo sikijui ila ukweli hawatokuja kujua kabila hata siku moja.
Ukiona hivyo hawa pendi kuona makabila tofauti na makabila yao sehemu ya kaz.
 
Ukiona hivyo hawa pendi kuona makabila tofauti na makabila yao sehemu ya kaz.
Kitu kinaboa watu wananiita kabila ambalo mi sipo kabisa!! Wala hata salamu za hayo makabila bahati mbaya sijawai kuishi kweny kijijini cha kabila baba yangu amezaliwa upareni huko hedaru ila sio mpare na amekulia huko mpaka anaota kazi so anajua kipare tu!!!ila sio mpare maana mpare ni mama ake babaake sio mtu wa huko na hawajui asili yao ila wanatania za kipare coz wangezaliwa huko sasa Mimi nimezaliwa sehemu tofauti ambapo anaishi baba uko kwao alishatoka .

Mtaani kwetu baba anajulikana kama mpare na ndugu upande wa mama ake ni wengi wa huko upareni hapo town, basi watu wanajua ni mpare 😂😂😂😂😂ila jina sio la kipare kabisa
 
Watu kama wewe makazini(ofisini) kwa kuchonganisha watu, umbeya, uchawa kwa boss ni hatari sana.

Fanya kazi yako hayo mambo sjui kabila, unaishi wapi yanakusaidia nini?
 
Soma vizur mada,harafu uchangie upya
Watu kama wewe makazini(ofisini) kwa kuchonganisha watu, umbeya, uchawa kwa boss ni hatari sana.

Fanya kazi yako hayo mambo sjui kabila, unaishi wapi yanakusaidia nini?
 
Back
Top Bottom