Hali ya kutokupenda ujulikane wewe ni kabila gani maofisini ni uzalendo au ni usaliti?

Hali ya kutokupenda ujulikane wewe ni kabila gani maofisini ni uzalendo au ni usaliti?

Wengi wao utakuta wana asili ya nchi jirani malawi,zambia,kenya,burundi na uganda.

Yupo mzambia mmoja alikuwa branch manager wa benki lakini alikuwa anajificha huyo akidai kwao Katavi sijui huwa wanaogopa nini. Lakini kabila la mtu halijifichi utajulikana tuu.
 
Mnaofanya Kazi katika ofisi za Uma na za private lazma mtakubaliana na mim kuwa Kuna watu huwa hawataki wajulikane kuwa yeye Ni kabila gan,mfano watu wa Kanda ya ziwa waliobahatika kusoma na kuajiliwa kwenye ofis za Uma huwa hawapendi wajulikane walikotoka.

Wanawake wa Kisukuma ndo wanaongoza kwa Tabia hii.

Kwa Sasa npo kweny ofis moja ya Uma Kuna jamaa Ni kabila fulan ila hataki ajulikane kuwa yeye Ni kabila Hilo,Kuna ciku alikuwa anaongea na cm kisir kwa kilugha ndo nkajua kuwa kumbe jamaa Ni wa kabila Fulani ila hatak kuongea kilugha na watu wa kabila Hilo hata mkiwa nje ya ofisi.

Swali Ni je yeye anadumisha uzalendo wa kuondoa ukabila au anasaliti kabila lake?
Unamuuliza mtu kabila unataka kutambika ( Julius Nyerere)
 
Kila mtu anapaswa kuwa huru akitaka kujulikana kwa kabila lake sawa na asipotaka kujulikana pia sawa.
 
Mkataa kwao mtumwa, hata wewe kuweka avatar ya mdhungu ni ulofa na kuukataa uafrika wako
Unajua maana ya Uafrika?
Unaangalia movie na kusikiliza music?
Unavaa nguo za vitambaa?
Una dini yoyote?
Unamiliki TV, simu, redio, feni au hata sofa?
Unaishi ndani ya nyumba ya kisasa?
Unapanda gari, pikipiki au hata baiskeli?
Unamiliki smartphone?
Je unatumia Internet?
Je unatumia JamiiForums?

Jibu swali hata moja kati ya hayo, kama hapana kwa yote basi wewe kweli ni Muafrika otherwise ni mtumwa asiyejitambua.
 
Back
Top Bottom