Hali ya Maambukizi ya HIV kwenye vyuo vikuu si nzuri na elimu ya kujikinga haitolewi vya kutosha kama miaka ya nyuma 2010 kurudi nyuma

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
1,907
Reaction score
3,560
Kama una mdogo wako wa kike awe makini aache tamaa ya mambo ambayo hana uwezo nayo, kwa sababu mabinti wengi wanaingia kwenye vishawishi vya kutembea na wanaume walio wazidi umri (Sugar dads) ili kupata fedha.

Pia mdogo wako wa kiume wa chuo mwambie afunge zipu asome kwani wengi wa wanachuo wenzao wakike wanakuwa nao lakini pia wanatembea na hiyo mibaba inayowarubuni kisa fedha zao.

Wazazi ni wajibu wa kuwa karibu na mwanao ili ujue anaendeleaje na jitahidi uzungumze nae mare kwa mara.

Serikali nayo inachangia kwa namna nyingine kwa kuto kutoa mikopo kwa wanafunzi wote na pia kuchelewesha kutoa mikopo hiyo kwa wakati.
 
Source of data?
 
Ujumbe ni mzuri ila ni taarifa ambayo ina walakini. Ulivyoeleza ni kama ngoma inapatikana kwa kutembea na watu wazima wakati takwimu zinaonesha kuwa, vijana ndio wanaongoza kwa kuwa na ngoma.
 
Taarifa ya hovyo sana hii
 
Uongo ,hizo takwimu sio sahihi acha kuogopesha watu
 
Kumbuka pia kuna watoto wengi age hiyo ambao walizaliwa na HIV kutoka kwa wazazi, either wa kike au wa kiume. So inawezekana msichana asiwe na sugar daddy lakini akawa na HIV ya kuzaliwa nayo. Vijana wazoee kitumia kinga, iwe ni kitu cha kawaida.

Na wanaume mnaopenda GenZ kuweni makini sana. Wameungua mpaka sio poa, na wanaambukiza makusudi, they don't care.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…