Hali ya maisha Ethiopia Inasikitisha sana, vibaka wanavamia nyumba za watu kuiba chakula

Hali ya maisha Ethiopia Inasikitisha sana, vibaka wanavamia nyumba za watu kuiba chakula

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuka wanajamvi!

Wa Ethiopia wengi walioko nje Diaspora wanapitia wakati mgumu sana kwasababu ya ndugu zao nyumbani wanayopitia.

Sasa hivi wengi hawajui kama ndugu zao wako hai au wamekufa. Simu zao hazipatikani wala kwenye mitandao ya jamii hawaonekani.

Hali imekuwa ya sintomfaham sasa hivi Addis Ababa. Wale wenye uwezo ndugu zao wako ulaya wanawatumia hela wananunua vyakula kwa jumla 'panic buying'. Licha ya kununua vyakula kwa jumla wananunua kwa kujificha usiku au gizani kwasababu watu wakikuona watakuvamia kwako na kuiba chakula chako.

Addis Ababa sasa hivi imejaa watu waliotoroka kutoka majimbo mengine kwenda kwa ndugu zao kwaajili ya usalama wao. Katika nyumba yenye chumba kimoja na sebule wanaishi watu siyo chini ya saba.

Juzi kati hapa kazini marafiki zangu wa Ethiopia mmoja mtigray na mwengine Amhara walipigana kisa tofauti zao kikabila. Lakini ukiwaonaga kwa sura wanafanana tu kuwatofautisha ni ngumu.

Ila katika uchunguzI wangu wanawatambua WaTigray kwa majina na kitambulisho. Vilevile wa Oromo.

Nimekaa nao hawa watu nakuwahoji sana tukiwa kazini kwa muda mrefu.

Oromo wengi wao ni wasomi sana na maprofesa ila washamba. Yani wanaitwa watu wa porini barbaric. Muoromo anaweza kujenga nyumba akaipaka rangi ya kijani pinki njano toka kwenye paa ukutani hadi chini. Muoromo wanadai hajwajui kuwa smart hata kwa mavazi licha ya hata akiwa amesoma sana. Wan ile inferiority complex. Wakowako kivyako vyao hadi wameanzisha benki zao.

WaTigray ni wachache ila ni wafanya biashara mashuhuri sana na wana hela nyingi na mali. Majumba na maghorofa mengi Addis Ababa yalikuwa yao ila yote wameporwa sasa hivi. Wana madharau sana nakujiona juu.

Hii chuki imedumu miongo na miongo. Mungu asipoingilia kati kutatokea uchinjaji wa aina yake.

Nitawaletea uzi mwengine kutoka Cameroon maisha yao na uhasama.

Source simulizi za wa Ethiopia wenyewe nafanya nao kazi.
 
Ubaguzi ni mbaya, hasa ukitokea kwenye tabaka la watawala. Ethiopia ni mbali, hapa Tanzania lipo tabaka linayafanya hayo kila kukicha.
 
Ubaguzi ni mbaya, hasa ukitokea kwenye tabaka la watawala. Ethiopia ni mbali, hapa Tanzania lipo tabaka linayafanya hayo kila kukicha.
Kweli ubaguzi mbaya sana. Family are displaced. Sasa hivi hadi China inaondoa raia zake ukiacha Marekani na nchi zingine za Magharibi.
 
Ushenzi wanaoufanya CCM visasi vitakuja hata huku
Haa wapi acha kabisa kuwapaka matope CCM hiki chama kimejitahidi kutujengea umoja hasa waasisi wale walitujengea msingi wa umoja ukasukwa na nondo kabisa.

Sisi makabila na siasa sio kipao mbele Sanaa ila dini sasa hapo tuwe makini kweli dini watanzania tunavurugwa kwa wepesi sana
 
Haa wapi acha kabisa kuwapaka matope ccm hiki chama kimejitahidi kutujengea umoja hasa waasisi wale walitujengea msingi wa umoja ukasukwa na nondo kabisa.

Sisi makabila na siasa sio kipao mbele Sanaa ila dini sasa hapo tuwe makini kweli dini watanzania tunavurugwa kwa wepesi Sana ..
Ya Magufuli na Samia huyaoni
 
Ya Magufuli na Samia huyaoni
ukiona nchi vijana hawaangaiki hata kutoka kwenda kukimbia nchi nyingine tena katika kipindi hiki cha utandawazi ujue hapo kuna amani na fursa..ndio tanzania hii sisemi kama tupo 100% peacefull hapana kinachotusumbua watanzania ni kutaka kuwa na maisha flani hivi standard na yanapatikana kama unapambana kweli tofauti na nchi za wenzetu kabisa wanamaisha ya ajabu serikali inawatenga ukanda flani kabisa kisa tofauti ya kikabila au dini au koo haiwajui kwa chochote..

kwa hapa tz sehemu ambayo ingeleta shida kwa mambo ya ukabila na ukanda ni unguja na pemba lakini cha ajabu serikali ya ccm ingawa mara nyingi kama si zote inakosa ushawishi wa kisiasa pemba ila maendeleo na miundombinu mbalimbali vinaendelea kujengwa sawasawa na unguja ndio maana unaona wapemba kadri muda unavyoenda wanazidi kutambua kuwa siasa kumbe sio uhadui.

ukweli ni kwamba nchi nyingi za afrika na duniani zinatakiwa zije kujifunza utawala bora hapa tanzania kutawala nchi yenye watu wa dini na makabila mbalimbali na wakaishi kwa amani na umoja kama ndugu si mchezo ..MUNGU awabariki viongozi wa ccm hasa waasisi wake ndicho ninachoweza kusema.
 
Back
Top Bottom